Masanilo
Platinum Member
- Oct 2, 2007
- 22,286
- 4,493
Nimekuwa nikifatilia kwa miongo mingi sasa viongozi wengi madikiteta wakipinduliwa huwa wanatafuta hifadhi za kisiasa Saudi Arabia. Nitatoa mifano michache hapa
- Waziri mkuu wa zamani wa Pakistani Nawaz Sharif baada ya kuangushwa alikimbia Saudi Arabia
- Waziri mkuu wa Syria 1951 bw Ma'ruf al-Dawalibi Alikimbilia Saudia hadi alipokufa mwaka 2004
- Idd Amin dada raisi wa zamani wa Uganda aliyeangusha na majeshi ya Nyerere na yeye alikimbilia huko mwaka 1980 kuishi huko hadi kifo chake mwaka 2003
- Raisi wa zamani wa Tunisia Mh Zine el-Abidin Ben Ali naye baada ya kukimbia nchi Jan 16, 2011 amekimbilia Saudi Arabia
- Mzee mzima Pervez Musharraf baada ya kulazimishwa kujiuzulu naye alikimbia Saudi Arabia tangia 2008