Gang Chomba
JF-Expert Member
- Feb 29, 2008
- 20,301
- 4,681
Kwa wageni wa Soka na watoto waliouvamia mchezo huu kwa kusukumwa na shetani la kamari ndio wanaweza kushangazwa na umwamba wanao wekeana nyota wa klabu ya PSG Edinson Cavani raia wa Uruguay na Neymar jr raia wa Brazil.
Lakini kwa wenyeji wa mchezo huu, ambao tulianza kuufuatilia mchezo wa soka yapata miongo miwili na miaka ipatayo nusu ya mwongo mmoja, waala hatujashtushwa na ubabe wa kila mmoja kati ya wawili hao.
Kule bara la Amerika ya Kusini kila nchi ni temi. Japo wengi huhisi kuwa watemi wa bara lile ni Brazil na Argentina.
Umwamba wa wachezaji wa bara lile, tena wenyewe kwa wenyewe haukuanza jana wala juzi…
Hivi mnakumbuka sakata la Ronaldo de Lima raia wa Brazil na Ivan Zamorano raia wa Chile, pale walipogombea jezi nambari 9 mgongoni kiasi kwamba uhasama ulipelekea kuigawa klabu ya Inter Milan kwani washabiki walisimama upande wa Zamorano ambae ndie alikuwa na jezi hio, lakini uongozi wa klabu ukiongozwa na milionea wa visima vya mafuta ambae ndie alikuwa mmiliki klabuni hapo Masimo Moratti ulitaka jezi hio apewe mchezaji ghali alienunuliwa kwa dau la kuvunja rekodi ya Dunia karne iliopita?
Nani ambae hakuwahi kuona jezi ikiwa na namba ya tofauti ambayo Zamorano aliamua kuivaa ili kumuachia De Lima namba 9?
Hivi ni nani asiekumbuka aina ya ushangiliaji alioitumia Ivan Zamorano baada ya kufunga goli huku akiwa kavaa jezi namba 1+8 ambayo ilikuwa na jawabu la 9?
Je ilimaanisha Inter walikuwa na jezi mbili zenye nambari 9 mgongoni?
Je nani kasahau ugomvi wa De Lima na Alvaro Recoba wa kugombea mipira mfu iliopatikana katika mechi za klabu hio?
Kuna sababu ya matukio haya kutokea.
Kwa sasa endelea kunywa Mtori, Nyama utazikuta chini…
Nitarudi…