No problem; ni mchakato wa CCM wa katiba mpya, wacha uendelee. Na kwa kuwa mchakato huu right from the begining ulishaonesha hautaleta katiba iliyokusudiwa, suala la Katiba Mpya ni endelevu regardless mchakato huu utazaa 'katiba mpya' ya aina gani. Itabaki kuwa ajenda ya kudumu hadi hapo Katiba Mpya ya Wananchi itakapopatikana na hili wala halizuiliki.
Haikuwahi kuwa kwenye Ilani wala ajenda za CCM, serikali nzima kuanzia mawaziri, Jaji Mkuu na watendaji wakuu wa CCM walikuwa wanapinga suala la katiba mpya mara ghafla kama vile wamekurupuka ndotoni wakaidaka ajenda na 'kuongoza' mchakato. Unategemea kuna kitu hapo? Another wastage of time and resources.
....Haikuwa ajenda ya CCM, JK wala serikali yake (Ushahidi upo). Hoja hii ni pandikizi kutoka kwa watu fulani wanaotaka kuutumia uwepo wake madarakani kuweka mambo yao sawa. Wamemtumia JK kwa sababu wanammudu. Dalili zote zipo wazi. Angalia mtiririko wa matukio tu utagundua. walianza na part one - kupitisha katiba ya Zanzbar inayoitambua Zanzbar kuwa ni nchi. part two tume iwe na wazanzbari na watanganyika nusu kwa nusu. Kuna strategy hapa - tusubiri part three. Ninachotabiri ni kuwa tume hii haitawagombanisha CCM na wapinzani, nahisi huko mbele hoja hazitakuwa CCM au CDM kwa kuwa naamini baadhi ya wanaCCM wataungana na wanaCDM na baadhi ya wanaCDM wataungana na wanaCCM hapo ndipo tutajua uamuzi wa ghafla kukubali kuunda katiba mpya ulikuwa wa nani, maana kwa hakika haukuwa wake.