hata kidogo; nilishasema nilichotaka kusema kabla hawajafanya hayo na utaona sikuwa miongoni mwa watu walioshangilia tukio lile. Msimamo wangu toka mwanzo haujabadilika.
yale yale ya edwin mtei- "waislamu ni wengi kuliko wakiristo", Kama nikiunga mkono, naunga mkono aina ya tume itakayozingatia usawa wa haki na wajibu wa raia na si usawa wa idadi ilimradi idadi-tukianza kudai usawa wa kinamba namba basi sijaona mzanaki hata mmoja kwenye hiyo tume, je wazanaki maslahi yao yatawasilishwa na nani?
Wananchi tumefungwa "goli la kisigino" na CCM.
Mwanakijiji,
Msome pia Jenerali Ulimwengu kwenye makala zake ndani ya RaiaMwema. Hoja zenu zinafanana. Nisichokifahamu mimi ni kwa vipi na kwa namna gani mchakato huu ungeikwepa CCM, serikali yake na hata Bunge lake. Tungeanzia wapi? Hebu ngoja tuuanze mchakato wenyewe hivyo ulivyo. Naamini mpo watu kama ninyi, vipo vyama makini vya upinzani, zipo asasi makini zisizo za kiserikali na above all wapo WATANZANIA makini wengi tu kwa sasa. Tupate KATIBA MPYA. Mengine yote ikiwemo Tume huru ya uchaguzi yatatokana na KATIBA hii. Ilikuwa ni ndoto mwaka 1995 chama cha upinzani kushinda uchaguzi mdogo kama ule wa AruMeru Mashariki lakini sasa kwa Katiba hii mbovu imewezekana! Tusijikatishe tamaa.
Nikushukuru ndugu yangu M. M. Mwanakijiji, umewafungua wengi sana, japo wanaona tumechelewa kutamka bayana lakini naamini ujumbe utawafikia wote!
Mkuu, kinachotokea ni kama kile kilichotokea Kenya. Kama unakumbuka Boma commission na Wako commission na jinsi zilzivyoleta msuguano na wananchi.Mwanakijiji,
Msome pia Jenerali Ulimwengu kwenye makala zake ndani ya RaiaMwema. Hoja zenu zinafanana. Nisichokifahamu mimi ni kwa vipi na kwa namna gani mchakato huu ungeikwepa CCM, serikali yake na hata Bunge lake. Tungeanzia wapi? Hebu ngoja tuuanze mchakato wenyewe hivyo ulivyo. Naamini mpo watu kama ninyi, vipo vyama makini vya upinzani, zipo asasi makini zisizo za kiserikali na above all wapo WATANZANIA makini wengi tu kwa sasa. Tupate KATIBA MPYA. Mengine yote ikiwemo Tume huru ya uchaguzi yatatokana na KATIBA hii. Ilikuwa ni ndoto mwaka 1995 chama cha upinzani kushinda uchaguzi mdogo kama ule wa AruMeru Mashariki lakini sasa kwa Katiba hii mbovu imewezekana! Tusijikatishe tamaa.
Unajua ukifikiria sana utaona kuwa CCM iliwazidi kete CDM; pale Rais Kikwete "alipokubali" kuwa kutakuwa na Katiba Mpya basi baadhi ya wapinzani wakiwemo ndugu zangu wa CDM wakawa kama mbwa mbele ya chatu; wakalainika. Matokeo yake hata sasa ni vigumu kabisa kwa wao kujenga hoja kuwa mchakato ni mbaya.