Kwanini Mwalimu Nyerere alifanikiwa kupambana na Ukabila, Udini na Ujimbo?

Gogovivu

Member
Apr 21, 2009
9
1
Taifa letu tangu anga'atuke Baba wa taifa na hatimae kufariki katika mwaka 1999 maradhi ya kijamii ya ukbila,udini na ujimbo yamezuka kwa nguvu na kwa kasi kubwa sana,kiasi ya kutishia amani,usalama na umoja wa nchi yetuSasa swali ambalo linalojiuliza hapa kwa nguvu ni hili,Je kwa nini Mwalimu Nyerere alifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kupambana na magonjwa haya ya balaa ya kutishana kuhatarisha usalama,amani na umoja wa taifa; ukabila,ujimbo, na udini ambapo wamefeli viongozi wote waliofuatia?

Kwa kujibu swali hili ni kwamba Mwalimu Nyerere alikua ni kiongozi msomi(intelectual),kiongozi ambaye alikuwa na haiba(charisma),kiongozi ambaye aliipenda nchi yake na wananchi wake.Mwalimu Nyerere ukiachilia mbali changamoto zilizokuepo mbele yake kwa wakati wake za kujikomboa bara la Afrika na nchi nyingi kutoka katika mikono ya wakoloni na kutafuta umoja wa Afrika au wa Waafrika ambapo alishiriki kikamilifu kwa wakati na nguvu zake zote.

Swala la changamoto la nchi yake hakulifumbia macho hata kidogo,alijua kwamba wananchi wake ni masikini sana, ni watoto wa wakulima na wafanyakazi(kwa bango la siasa ya kijamaa)kwa hiyo alipambana na umasikini,ujinga na maradhi na ndiyo mabalaa na hatari kubwa kwa wananchi masikini,na alifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kama si njama za nguvu za kipebari na wasiopenda maendeleo ya nchi changa kumlenga Mwalimu kutofanikiwa x aliyopigania kwa nchi yake na wananchi wake.


Mwalimu Nyerere,kama msomi( intelectual)alijua matatizo gani au maradhi gani ambayo jamii yake inayo udini,ukabila na uzoni na yanaweza yakawa ni hatari sana na kikwazo kikubwa cha maendeleo ya nchi yake, na kwa kuyajua maradhi hayo alikabiliana nayo kwa nguvu zake zote bila ya kuchoka,na kitu cha kwanza alichokiona Mwalimu na kuaanza kupambana na maradhi hayo ambayo yanayohatarisha amani,usalama na umoja wa taifa ni kuondoa nguvu za machifu au kuufuta uchifu ambao ni moja ya mizizi jizatiti ya nguvu za kisiasa ndani ya nchi,ukabila na uzone hili nalo alifanikiwa-lakini ajabu ya mambo,leo hii kuna viongozi wengine utwasikia wakijiita au kujinasibisha na uchifu-.Jambo lingine alilolipigania ni kwa taifa kutumia lugha moja kwa mawasiliano ya kijamii na nyanja zake zote za kitaifa,hili nalo alifanikiwa kwa kutosogeza wananchi kuwa kitu kimoja popote pale tulipo ndani ya nchi au nje ya nchi.

Kwa majuhudi yake hayo alifanikiwa kwa hili, wakati mtanzania anaweza kuoa au kuolewa popote pale ndani ya nchi yake bila kujali ukabila udini au ujimbo-jambo hili watanzania tunaliona ni la kawaida lakini moja ya mafanikio makubwa sana ya Mwalimu kutufanya na kutuunganisha wananchi wa nchi hii kuwa wamoja na kulifaharia-lakini nina shaka kwamba zimeshaanza kujitokeza hata katika ndoa udini,ukabila na ujimbo vanachukua nafsi yake kuliko ZAMANI.

Mwalimu Nyerere kama msomi (intelectual) alijua kwamba swala la dini ni hatari sana kwa umoja,amani na usalama wa nchi,na alijua kwamba ni bomu la kutegwa linahitaji wakati,sababui na vichocheo tu kuweza kulipuka.Kwa hiyo hakulifumbia macho hata kidogo, alijitahidi kwa nguvu zake zote kuondoa sababu zote na mbolea zote za kututumuka kwa udini katika nchi yetu,kwa kutaifa mashule za makanisa,kufunga taasisi za kidini kama taasisi ya kiisilamu ya Agha khan,na kuhakikisha nchi inasimamishwa kwa muhimili wa kisekula (secularism) kwamba serikali haina dini isipokuwa wananchi wake ndio wafuasi wa dini mbalimbali, na dini yako ibaki kanisani,msikitini au mzimuni mwako ukitoka huko watanzania wote ni sawa.

Nakumbuka hata kuna mzee mmoja mkereketwa wa kiisilamu(Tabora) baada ya Tanganyika kupata uhuru wake alimtaka Mwalimu awape waisilamu nafasi kubwa katika madaraka kwa vile mchango wao ni mkubwa katika kupigani uhuru wa Tanganyika,Mwalimu alimjibu kwa upole na utulivu kwamba "siwezi kuigawa Tanganyika kama ilivyogawiwa India na Pakistani."Lakini leo hii udini umerudi kwa kasi na nguvu zote na viongozi wa dini wanjiingiza kwa nguvu zote katika serikali na kuikanganya, mpaka wengine wanataka mahakama ya kadhi itiwe katika katiba ya nchi ya kisekula(secularism)!

Na leo hii viongozi wa kidini wanaungurumiana utadhani wana siasa na hata kuwaagiza wafuasi wao wawe na muono au maamuzi fulani kwa kuipinga au kiunga mkono serikali!!!

Naam,Mwalimu Nyerere alikuwa ni kiongozi imara shupavu mwenye haiba na mwenye visheni na kwa wakati wake wenye maradhi hayo ya ukabila,udini na ujimbo wote walivyata mikia yao kwa unafiki, lakini baada ya kuondoka Mwalimu Nyerere yale aliyoyapigania yote yamekuwa yanapeperushwa kwa hewa kwa nguvu za wenye kupenda udini,ujimbo na ukabila.

Kwa hiyo tatizo la kimsingi linalalia kwa viongozi kuanzia awamu ya pili hadi hii ya nne wamekuwa ni viongozi wenye kuyumbishwa na nguvu zote za udini,ukabila na ujimbo na kutojali au kuliona kama ni tatizo kama alivyoona Mwalimu Nyerere aidha kwamba wao wenyewe wana maradhi hayo ya udini,ukabila na ujimbo au kuathiriwa na matakwa ya nchi za nje.

Sasa kama viongozi wanayumbishwa kwa nguvu hizo tusitarajie kamwe kuona kwamba tutapata amani,usalama na umoja wa taifa letu hili.

Kwani inasikitisha kuona leo kwamba wanasiasa wetu wanaegemea kupata ofisi ya urais kupitia maradhi haya ya kijamii;udini,ukabila na ujimbo.Wanasiasa hao na viongozi hao kama watafumbia macho maradhi haya kwa tamaa zao za kisiasa,au kwa maradhi yao au kwa taathira za nje basi watanzania tujiandae tu matokeo ya Afrika ya kati,Burundi,Rwanda,Iraq na Syria.

Kwa hali halisi ilivyo hotuba,mawaidha, vikao kwa ajili ya kuongelea maradhi haya hayatotupatia ufumbuzi.Je wananchi wa taifa hili tushirikiane kwa pamoja kutafuta ufumbuzi wa bomu hili la kutegwa ,JE NINI CHA KUFANYA?

Wenye hekema walisema nchi ni mwananchi yeye ndiyo anaeijenga nchi na yeye ndie atakaeibomoa,watanzania tunahitaji kuwa macho sisi wenyewe na kuwa na hadhari na kujitibu kutokana na maradhi haya ambayo yatakayotubomolea nchi yetu,amani yetu na usalama wetu.

 
Ukabila na Udini vinaingizwa kwenye Siasa na baadhi ya Viongozi wetu wa Kisiasa na

hiyo yote kwa sababu kuna baadhi ya Viongozi wa Kisiasa wanataka kuongoza kwenye Siasa

Milele. Kuna baadhiya Viongozi wa kisiasa ni wabinafsi ndio wanaoleta hizo chokochoko za Ukabila na

udini wakati baba wa Taifa Mwalim Nyeree alipiga vita hilo suala wao baadhi ya

Viongozi wa kisiasa wanawatumia walala hoi udhaifu wao ili wapate kura kwenye uchaguzi na

kushinda Mkuu.@
Gogovivu
 
​Kwa faida ya kuelimishana ingekua vyema kutupa ushahidi wako jinsi gani Mwalimu Nyerere alivyoiacha nchi katika janga la mfumo kristo hii si kwa ajili yetu tu bali ni kwa faida pia kwa kizazi kijacho.Hii tuhuma ni hatari sana kwa kiongozi kama Baba wa taifa lete ushahidi wako ili tupate kuelimika.Na kila neno au msamiati una maana yake au tafsriri yake ningekuomba kwanza utuelimishe kwa kina na undani je nini maana ya Mfumo Kristo?
 
Hakuna jambo linaloweza kuota siku moja na kukomaa. Haya mnayoyaona leo ni matunda aya mbugu zilizopandwa muda mrefuuuu sana na viongozi wenu wa awamu za mwanzo.

Enzi za awamu ya kwanza watu walikuwa waoga na system iliwabana kuhoji mambo kwa upana wake kama ilivyo hivi sasa.
 
Kusoma hatutaki na tukisoma hatutaki kuelewa au tunajifanya hatuelewi.Hapa tunaongelea maradhi ya kijamii ambayo yanailfanya taifa kukosa amani usalama na hata kubaguana na swali je nini tufanye ili bomu hili la kutegwa lisije likapasuka?je ilikuwa tumuulize Mwalimu Nyerere kwa nini unapiga vita udini,ukabila na ujimbo?Mbona awakati wa Nyerere maradhi haya yote haayakuwa na nguvu ya kuathiri jamii,nchi na hata siasa?Sasa sijakuelewa nini tungehoji au kumuhoji mwalimu katika mapambano yake haya ya udini,ukabila na ujimbo.​
 
Back
Top Bottom