Kwanini mtu akishinda uchaguzi unahesabika wa haki na hauna makosa yoyote ila akishinda mpinzani wake inakuwa vinginevyo?

Tlaatlaah

JF-Expert Member
May 18, 2023
8,170
11,572
Hususani kwenye chaguzi za kisiasa na kesi mahakamani, kwamba ukishinda wewe uchaguzi kwenye sanduku la kura au ukishinda kesi mahakamani, basi hapo haki imetendeka na uchaguzi ulikua wa wazi, huru na haki na kura hazijaibwa wala kuibiwa.

Hulalamikii chochote, unanyamaza na kutulia tulia tuli, kama barafu, unafurahi, unashangilia ushindi wako mwenyewe na kujipanga way forward.

Ikitokea sasa umeshindwa wewe uchaguzi huo kwenye sanduku la kura na pengine umeshindwa pia kesi mahakamani hapo ndipo uchaguzi unakua haukua wa wazi, huru na wa haki, ndio kura zimeibiwa na mahakama zinakua sio huru?

Jambo hili huwa linanichanganya sana mimi nisiestahili ndugu zangu wana JF.

Nadhani ni vuzuri kujifunza ustahimilivu na kukubali kushinda na kushindwa, panapo ushindani.

Ifike mahali wadau wa siasa waathirike vizuri na demokrasia ya kweli akilini mwao mpaka mioyoni ili kusudi, zinapoisha chaguzi nchi haikwami mahali, bali inasonga mbele.

Tusiwacheleweshee wananchi maendeleo kwa kuzubaa kwenye hisia na mabishano ya kwamba eti fulani kaiba au kaibiwa kura, tunachelewa bure na kupoteza muda na uelekeo na kujenga utamaduni wa kudumu wa kulalamika.

Kuendelea mbele tunaweza kuanzia kwenye msingi huu wa Resilience, Reconciliation, Reforms and Rebuilding na kwa hakika tukiamua tunaweza.

Wasaalam.
 
Tumewachoka mturudishie Bandari yetu... Hakuna cha 'R' nne Wala 'R' moja....! Bandari irudi
 
Back
Top Bottom