Kwanini Mnipangie Bei ya Kuuza Sukari?

Basi hii itakuwa biashara nzuri sana tuache kuhangaika na kulima vanilla na matikiki tulime miwa na kuagiza sukari kutoka nje to infinity sababu kwa logic yako kuna soko la sukari ambalo halina kikomo
Kweli kabisa mkuu na ndo maana Sukari huwa wanaamua Kuuza bei wanazotaka..
Ila kwa sheria hiyo ya Soko Huria la.sukari kidogo itasaidia
 
Ukiruhusu biashara huria kwenye sukari hamna nguruwe atanunua sukari na kufungia ndani.
Yani useme kila anayeweza anunue, Mhindi gani huyo atanunua na kufungia? Akifungia si inanunuliwa nyingine, nchi jirani kibao sukari ni cheap kuliko Tanzania, hata Pakistan, Brazil, India wataenda watu.

Yani leo hii uanze kushindana na mahindi utaweza? Tununue kilo na gharama nyingine jumla kwa 650 na wewe ulipe 700 ili uyafiche si utakufa. Tunachofanya tunanunua na kukuuzia, kisha yakiisha tunaenda nje tunanunua na kukuuzia, na hao raia unaotaka kuwauzia juu ya 700 na wao tunawauzia chini yake sababu tunapata faida ila wewe ukishusha unakula hasara.
Mimi NimeMpongeza sana Bashe kuruhusu Soko la Sukari Kuwa Huria Huenda Itapunguza kama sio Kuua Tatizo kabisa la Mabwenyenye Kufungia sukari.

Sahizi ukifungia Sukari Tunaenda kununua Zambia au Zanzibar
 
Mimi NimeMpongeza sana Bashe kuruhusu Soko la Sukari Kuwa Huria Huenda Itapunguza kama sio Kuua Tatizo kabisa la Mabwenyenye Kufungia sukari..
Sahizi ukifungia Sukari Tunaenda kununua Zambia au Zanzibar
Bashe ni slow learner na kenge asiyesikia mpaka atokwe damu. Hili halikuwa suala la kusubiri watu wapige kelele na kulaani, ndipo achukue hatua.

Sukari wanaifanya iwe kama tukio la ghafla.
 
Haya mambo ya ajabu sana Tuliowapa kazi wameshindwa wanamtupia lawama mtu anayecheza na fursa....

Kama mtu ali-gamble akachukua shehena ya sukari fingers crossed kwamba bei zitapanda na yeye ajipatie bahati kwanini tumpangia bei ya kuuza wakati bei labda zikishuka (Mkeka wake usipotiki) hatumsaidii kumpa pole na kumwambia "Keep Change"!!!

Tupeleke lawama panapohusika Wizara ya Kilimo / Biashara na / Viwanda kwa kutokuona kujua demand inakuwa vipi na mizigo ipo vipi Uhaba wa Supply ni kosa la hawa watumishi wetu serikalini na sio jirani yangu ambaye anaona angalau haka ka-stock kake kamsaidie kupeleka mtoto shule....
we bwege subiri sheria zibadilishwe mlilindwa sana dhidi ya sukari ya nje. Hizo sukari zenu mnazoficha mtawauzia mama zenu. Huoni hata aibu, kima dhulumaji wewe
 
Mimi NimeMpongeza sana Bashe kuruhusu Soko la Sukari Kuwa Huria Huenda Itapunguza kama sio Kuua Tatizo kabisa la Mabwenyenye Kufungia sukari..
Sahizi ukifungia Sukari Tunaenda kununua Zambia au Zanzibar
Karuhusu lini na Wapi ?

Bei elekezi imefutwa ? Anao uwezo wa kufanya hivyo ?!!!; Hawa jamaa awamu hii ni waharibifu tu wameweka na bei elekezi kwenye bundle za simu (na wenzao TCRA) matokeo yake tunayajua....

we bwege subiri sheria zibadilishwe mlilindwa sana dhidi ya sukari ya nje. Hizo sukari zenu mnazoficha mtawauzia mama zenu. Huoni hata aibu, kima dhulumaji wewe
Na kwa akili kama zako ndio maana mwanasiasa anawatumia na kuwadanganya kama watoto na nyie kukubali (Kwahio kupanda kwa bei kunaletwa na watu kuficha sukari na sio Supply Ndogo)

Na hizo sound za kubadilisha Sheria ana-buy time anashindwa nini kusema kuanzia dakika hii mwenye sukari guru au chochote kile popote pale aagize na kuleta ? Na unadhani hata wakileta Kodi itakuwa kiasi gani ?

Wewe endelea kulishwa porojo na Mwanasiasa matokeo yake wanapeta scot free
 
Sidhani kama ni sawa kununua bidhaa na kuificha ndani uku unasubiri bei ipande, wakati uliuziwa Ili ukauze,
Wenye majenereta wamemwaga maji kwenye mabwawa wametengeneza mgao sasa wanapiga hela, na bashe nae kaona fursa kwenye sukari nae anapiga hela, haiwezekani makamba ale peke yake.
 
Karuhusu lini na Wapi ?

Bei elekezi imefutwa ? Anao uwezo wa kufanya hivyo ?!!!; Hawa jamaa awamu hii ni waharibifu tu wameweka na bei elekezi kwenye bundle za simu (na wenzao TCRA) matokeo yake tunayajua....

Katunga Sheria ambayo kwa sasa ni mswada anaupeleka Bungeni Ili ukajadiliwe ili Kuruhusu Soko Huria

View: https://youtu.be/u0YFd78I2lc?si=cHbeik_2xy9W1Bw5
 
Karuhusu lini na Wapi ?

Bei elekezi imefutwa ? Anao uwezo wa kufanya hivyo ?!!!; Hawa jamaa awamu hii ni waharibifu tu wameweka na bei elekezi kwenye bundle za simu (na wenzao TCRA) matokeo yake tunayajua....

Sheria soon Itapitishwa
 
Katunga Sheria ambayo kwa sasa ni mswada anaupeleka Bungeni Ili ukajadiliwe ili Kuruhusu Soko Huria
Kitakachotokea ni kuruhusu viwanda / mzigo kutoka nje ambapo watachaguliwa watu wachache sio soko huria per se.....

Hizi ndio zilezile danadana mara sipangii wakulima bei wala siwazuii kuuza nje ya nchi...., Mara paap sio kwamba ninawakataza lakini wakiuza wawe na vibali (sasa tangu lini mkulima / peasant akawa na vibali) huyo si ni mfanyabiashara...

In short siasa ni mbaya sana watu wanakuwa busy kwenye kujitetea na kutunga utetezi kuliko kutenda...; Yaani kutokuwepo kwao nina uhakika kungekuwa na unafuu kuliko huku kuingilia wanakukofanya....
 
Haya mambo ya ajabu sana Tuliowapa kazi wameshindwa wanamtupia lawama mtu anayecheza na fursa....

Kama mtu ali-gamble akachukua shehena ya sukari fingers crossed kwamba bei zitapanda na yeye ajipatie bahati kwanini tumpangie bei ya kuuza wakati bei labda zikishuka (Mkeka wake usipotiki) hatumsaidii kumpa pole na kumwambia "Keep Change"!!!

Tupeleke lawama panapohusika Wizara ya Kilimo / Biashara na / Viwanda kwa kutokuona kujua demand inakuwa vipi na mizigo ipo vipi Uhaba wa Supply ni kosa la hawa watumishi wetu serikalini na sio jirani yangu ambaye anaona angalau haka ka-stock kake kamsaidie kupeleka mtoto shule....
Kuna logic Hujaielewa hapa.

1. Serikali imepiga marufuku kuleta Sukari nje ili kulinda viwanda vya ndani (Hapa Tayari sio free market)

2. Viwanda vya ndani kwa kusaidiwa huku ina maana pia wa natakiwa bei kuithibiti sababu hawana competition.

Kwa logic yako hio Serikali nayo ikisusa na kufungua mipaka tegemea viwanda vya ndani vife na hao wanaojiona wababe wa Sukari wote watapotea.
 
Kuna logic Hujaielewa hapa.

1. Serikali imepiga marufuku kuleta Sukari nje ili kulinda viwanda vya ndani (Hapa Tayari sio free market)
Hilo pia ni kosa kuanzia mwanzo kama watu hawana capacity kwanini uzuie kutoka pengine... kama wengine wana comparative advantage ya kuweza kutengeneza sukari kwa bei ndogo sana kuliko sisi basi na tununue kwao tujikite kwenye jambo ambalo tuna advantage zaidi (hata kama ni kutengeneza ugoro)

It is the maxim of a every prudent master of a family, never to attempt to make at home what it will cost him more to make than to buy.
2. Viwanda vya ndani kwa kusaidiwa huku ina maana pia wa natakiwa bei kuithibiti sababu hawana competition.

Kwa logic yako hio Serikali nayo ikisusa na kufungua mipaka tegemea viwanda vya ndani vife na hao wanaojiona wababe wa Sukari wote watapotea.
Kama uwezo hawana hili lingefanyika mwaka juzi na sio mwaka kesho na ifike wakati hivyo viwanda viwaze na kupeleka nje sio ndani tu (zidisha production maradufu) : Hizi porojo ni za Mwanasiasa tu na kama inajulikana kabisa miezi gani kuna uhaba (haya mambo hutokea mara kwa mara).

Matokeo yake unataka Mangi aendelee kuuza buku tatu wakati huenda zamani alikuwa analetewa gunia sasa hivi analifuata tena kwa kupanga foleni (Hapo kosa la nani ? , Mangi au Serikali kwa kutokuwa Pro-active)
 
Bashe ni slow learner na kenge asiyesikia mpaka atokwe damu. Hili halikuwa suala la kusubiri watu wapige kelele na kulaani, ndipo achukue hatua.

Sukari wanaifanya iwe kama tukio la ghafla.
Usimlaumu Bashe, hii issue ya sukari ni kila awamu, si kipind cha Magu au JK kumekuwa na drama hzi hizi
 
Usimlaumu Bashe, hii issue ya sukari ni kila awamu, si kipind cha Magu au JK kumekuwa na drama hzi hizi
Nilimlauma aliyekuwepo then na nitamlaumu atakayekuwepo....; Ila kwa Bashe namlaumu nimeona anatabia ya kuchonganisha wananchi kwa shortcomings zake / zao... mfano Sakata la Mkulima kutokuuza na kuuza nje

Haya mambo ya ajabu sana Tuliowapa kazi wameshindwa wanamtupia lawama mtu anayecheza na fursa....

Kama mtu ali-gamble akachukua shehena ya sukari fingers crossed kwamba bei zitapanda na yeye ajipatie bahati kwanini tumpangie bei ya kuuza wakati bei labda zikishuka (Mkeka wake usipotiki) hatumsaidii kumpa pole na kumwambia "Keep Change"!!!

Tupeleke lawama panapohusika Wizara ya Kilimo / Biashara na / Viwanda kwa kutokuona kujua demand inakuwa vipi na mizigo ipo vipi Uhaba wa Supply ni kosa la hawa watumishi wetu serikalini na sio jirani yangu ambaye anaona angalau haka ka-stock kake kamsaidie kupeleka mtoto shule....
hujui mifumo ya uchumi ilivyo serikali isipoingilia kati utahama nchi
 
hujui mifumo ya uchumi ilivyo serikali isipoingilia kati utahama nchi
Wewe unayejua mifumo niambie ni wapi nchi / uchumi ulifanikiwa kupanga bei elekezi ?

Serikali inabidi iingilie kati (sio kwa kupanga bei) bali kwa kuhakikisha kwamba supply haishuki kama hivi inavyoshuka; na kuhakikisha kwamba kama supply ya ndani haitoshi wanaacha watu itoke nje mapema

Kupanga bei wakati supply ni ndogo kunaleta ulanguzi dawa pekee ni kuzidisha supply au kuwaachia watu wazidishe supply
 
kuna kitu kinaitwa price ceiling na price floor kama umesoma uchumi utanielewa kuna muda serikali ina interfere the market ili kubalance demand and supply bila kuumiza upande wowote , na unatakiwa uelewe hakuna nchi ambayo ni perfect capitalist nchi zote duniani wanaplly hii njia pindi price ikimove above or below equilibrium.
 
Nani ameongelea Capitalist ? Kwamba Hakuna kitu kinaitwa Social Markets?....

Narudia tena price setting has never worked out (Serikali kuingilia mara zote huwa inaharibu) history has taught us that...; Wameshindwa kuingilia na ku-set minimum wages na zimebaki kwenye makabrasha (sababu its impossible; they are no longer big employers na demand hugely our weighs supply) what happens setting up prices always unajikuta too late (the market moves very fast) na money chasing products is the only way ya kujua price gani ipo vipi... Kumbuka hii sio bidhaa kama umeme au Maji (ambayo supplier ni mmoja) au ni kazi kuachia supplier wengi waingie mzigoni...

Option kwenye sukari wana uwezo wa kuacha itoke nje (after all nje ni bei rahisi kuliko hata ndani); Narudia tena kwa Serikali ku-interfere with the market by setting up prices is bound to fail...;

Unampangia mtu Mangi bei auze buku tatu (huenda alikuwa analetewa mpaka mlangoni sasa hivi anachukua kwa bajaji ambazo petroli bei imepanda) unategemea huyo Mangi atauza buku tatu kwako au Buku nne usiku wa manane kwa watu kumgongea na kupitia mlango wa nyuma (na hadi watu wapite mlango wa nyuma tambua hawana alternative and at such time they are ready to pay that amount (only solution increase supply)
 
Back
Top Bottom