Kwanini Mnipangie Bei ya Kuuza Sukari?

Logikos

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
12,558
19,606
Haya mambo ya ajabu sana Tuliowapa kazi wameshindwa wanamtupia lawama mtu anayecheza na fursa....

Kama mtu ali-gamble akachukua shehena ya sukari fingers crossed kwamba bei zitapanda na yeye ajipatie bahati kwanini tumpangie bei ya kuuza wakati bei labda zikishuka (Mkeka wake usipotiki) hatumsaidii kumpa pole na kumwambia "Keep Change"!!!

Tupeleke lawama panapohusika Wizara ya Kilimo / Biashara na / Viwanda kwa kutokuona kujua demand inakuwa vipi na mizigo ipo vipi Uhaba wa Supply ni kosa la hawa watumishi wetu serikalini na sio jirani yangu ambaye anaona angalau haka ka-stock kake kamsaidie kupeleka mtoto shule....
 
Ziweke ndani unywe chai mwenyewe, mshapewa option, uzen kwa bei elekezi au lalen
Ndio hapo hatujui tunachotaka - Duniani hakuna Taasisi iliyoweza kupanga Bei - Ukipanga bei unaleta ulanguzi ukitaka bei ishuke wewe ongeza supply hakuna zaidi ya hapo.....

Ila ndio hivyo wanasiasa wanawalisha matango pori kwamba wao hawana tatizo tatizo ni Mangi mtaa wa pili kumbe wewe na yeye nyote ni wabangaizaji...
 
Ziweke ndani unywe chai mwenyewe, mshapewa option, uzen kwa bei elekezi au lalen
Na hizi ngonjera mtapewa tena muda kama huu mwaka kesho haya ni marudio ya kila siku.... hakuna jipya

Kwanini wasiongeze supply / uzalishaji au waachie huo mzigo kutoka nje ? Nani amewakataza ? Au kama vipi kwanini tusipange bei kila kitu Kama Supply and Demand imetushinda
 
Ndio hapo hatujui tunachotaka - Duniani hakuna Taasisi iliyoweza kupanga Bei - Ukipanga bei unaleta ulanguzi ukitaka bei ishuke wewe ongeza supply hakuna zaidi ya hapo.....

Ila ndio hivyo wanasiasa wanawalisha matango pori kwamba wao hawana tatizo tatizo ni Mangi mtaa wa pili kumbe wewe na yeye nyote ni wabangaizaji...
Tatizo la Tanzania Ukiongeza Supply bado watanunua supply yako.yote uliyonunua Ili tatizo libaki pale pale..

We humjui mbongo wewe..

We ongeza Tani 28 za sukari atakuja Mdosi atanunua Tani 20 ataweka ndani
 
Sidhani kama ni sawa kununua bidhaa na kuificha ndani uku unasubiri bei ipande, wakati uliuziwa Ili ukauze,
Kama haujui hio ndio biashara yenyewe kununua kwa bei rahisi iwezekanavyo ili uuze bei kubwa iwezekanavyo enzi za Ujamaa au Duka la Kaya ungeitwa Mlanguzi ila kwa sasa soko Huria ndio faida inavyopatikana...

Kama tunataka Huduma ni rahisi sana kama vile ilivyo Soda (wanafanya marketing na kila kitu) bei 600/= hivyo viwanda vya UMMA vizalishe na kuweka bei elekezi wanazotaka wao ila pia wampe mfanyabiashara option ya kununua popote mteja achague mwenyewe
 
Shida mnatengeneza tatizo mkidhani bei itapanda,
Kina nani ?
Mangi Mtaa wa Pili ? au Wenye Viwanda ? Kama wenye viwanda na kila mwaka hizi shida zinatokea kwanini Serikali isiruhusu mzigo kutoka nje kutokea mwanzo (wanakumbuka shuka wakati kumeshakucha)..

Issue lawama zinakwenda kwa mtu ambaye sio (Mangi na Muha Mtaa wa Pili) wakati wanaosababisha haya mambo kila mwaka ni watu wa porojo tu (Divide and Rule) its about time lawama apelekewe mchawi mwenyewe (Serikali) na Dawa sio kutishiana na kupangiana Bei... Mfano mimi nimenunua Sukari kwa kupanga foleni siku nzima nikifika home jirani yangu akisema anipe bei mara mbili nikatae ?!!
 
Tatizo la Tanzania Ukiongeza Supply bado watanunua supply yako.yote uliyonunua Ili tatizo libaki pale pale..

We humjui mbongo wewe..

We ongeza Tani 28 za sukari atakuja Mdosi atanunua Tani 20 ataweka ndani
Basi hii itakuwa biashara nzuri sana tuache kuhangaika na kulima vanilla na matikiki tulime miwa na kuagiza sukari kutoka nje to infinity sababu kwa logic yako kuna soko la sukari ambalo halina kikomo
 
Hoarding haikubaliki kwenye biashara.Huwezo kuficha bidhaa na kufanya kuwe na uhaba ili upandishe bei.
Nina tani zangu za mahindi nimelima nasubiri msimu wa mavumo uishe ili niuze..., hapo unasemaje ? Na kweli tatizo ni hao kina Mangi wanaoshikwa mtaani au ni uzembe wa Wizara kutokujua uhitaji na uzalishaji (being pro-active na sio reactive)
 
Tatizo la Tanzania Ukiongeza Supply bado watanunua supply yako.yote uliyonunua Ili tatizo libaki pale pale..

We humjui mbongo wewe..

We ongeza Tani 28 za sukari atakuja Mdosi atanunua Tani 20 ataweka ndani
Ukiruhusu biashara huria kwenye sukari hamna nguruwe atanunua sukari na kufungia ndani.
Yani useme kila anayeweza anunue, Mhindi gani huyo atanunua na kufungia? Akifungia si inanunuliwa nyingine, nchi jirani kibao sukari ni cheap kuliko Tanzania, hata Pakistan, Brazil, India wataenda watu.

Yani leo hii uanze kushindana na mahindi utaweza? Tununue kilo na gharama nyingine jumla kwa 650 na wewe ulipe 700 ili uyafiche si utakufa. Tunachofanya tunanunua na kukuuzia, kisha yakiisha tunaenda nje tunanunua na kukuuzia, na hao raia unaotaka kuwauzia juu ya 700 na wao tunawauzia chini yake sababu tunapata faida ila wewe ukishusha unakula hasara.
 
Unapangiwa uache uhuni na ulanguzi.

Mnawakosesha watu Utamu.

Kwa kifupi mmezoea kutesa watu nyie Bigboyz Wafanyabisahara wa Sukari.
Last time I checked Mangi Mtaa wa Pili sio Big Boy wala kumuita Mlanguzi ni kosa Sababu Sukari alikuwa analetewa mlangoni sasa hivi anaifuata kule mjini na anapanga foleni siku nzima....

Ila ndio hivyo Mwanasiasa amekuhamisha kwenye Hoja (uzembe wake) anamsingizia an invisible enemy... Sijaona Big Boy yoyote ameshikwa zaidi ya walalahoi wenzangu kitaa..

Na kama vipi kwanini tusiongezee mzigo ushuke hata tshs 2,000/=
 
Kama haujui hio ndio biashara yenyewe kununua kwa bei rahisi iwezekanavyo ili uuze bei kubwa iwezekanavyo enzi za Ujamaa au Duka la Kaya ungeitwa Mlanguzi ila kwa sasa soko Huria ndio faida inavyopatikana...

Kama tunataka Huduma ni rahisi sana kama vile ilivyo Soda (wanafanya marketing na kila kitu) bei 600/= hivyo viwanda vya UMMA vizalishe na kuweka bei elekezi wanazotaka wao ila pia wampe mfanyabiashara option ya kununua popote mteja achague mwenyewe
Wanaogopa viwanda vyao vitakufa.
 
Last time I checked Mangi Mtaa wa Pili sio Big Boy wala kumuita Mlanguzi ni kosa Sababu Sukari alikuwa analetewa mlangoni sasa hivi anaifuata kule mjini na anapanga foleni siku nzima....
Hawa wakuu ndio wanatuaminisha hivyo. Mvua kubwa kweli kweli Ngoja tuone panapovuja sasa
Ila ndio hivyo Mwanasiasa amekuhamisha kwenye Hoja (uzembe wake) anamsingizia an invisible enemy...
Labda?

Sijaona Big Boy yoyote ameshikwa zaidi ya walalahoi wenzangu kitaa..
Sasa wale anaoenda kuwatungia sheria ni kina nani? Manake kwa maelezo mafupi pale ni kama anasema kuna ka monopoly fulani...kumbe ni wakina mangi! ...walio chini ya mfumo mkuu
Na kama vipi kwanini tusiongezee mzigo ushuke hata tshs 2,000/=

Kama sijakosea wamesema wanataka kufanya marekebisho ya sheria kuruhusu ushindani zaidi, na kwa kufanya hivyo kutachochea hizo bei kushuka bila ya Bodi(Serikali) kutoa "bei elekezi"..
 
Hawa wakuu ndio wanatuaminisha hivyo. Mvua kubwa kweli kweli Ngoja tuone panapovuja sasa
Mwanasiasa always anachukua credit hata pasipomuhusu na kila baya kuna mtu wa kusingizia
Sasa wale anaoenda kuwatungia sheria ni kina nani? Manake kwa maelezo mafupi pale ni kama anasema kuna ka monopoly fulani...kumbe ni wakina mangi! ...walio chini ya mfumo mkuu
Wakati anangoja kutunga sheria watu waendelee kunywa chai ukwaju ?; Anajua by the time wamekaa na kubishana weee huenda atakuwa sio Waziri tena au wakaleta sheria za kutoa vibali kwa wachache kuagiza nje (wachache hao kumbe ni kampuni zao kwa mgongo wa muwekezaji)
Kama sijakosea wamesema wanataka kufanya marekebisho ya sheria kuruhusu ushindani zaidi, na kwa kufanya hivyo kutachochea hizo bei kushuka bila ya Bodi(Serikali) kutoa "bei elekezi"..
Kweli hio inahitaji Sheria Bungeni ? Kwanini wakati mambo ni magumu wasiseme haya kwa sasa kabla hatujatunga hizo so called sheria kila mwenye mzigo wake na auweke mezani kwa bei anayotaka (hata kama ni kugawa bure kama vile tshirt za matangazo)
 
Haya mambo ya ajabu sana Tuliowapa kazi wameshindwa wanamtupia lawama mtu anayecheza na fursa....

Kama mtu ali-gamble akachukua shehena ya sukari fingers crossed kwamba bei zitapanda na yeye ajipatie bahati kwanini tumpangia bei ya kuuza wakati bei labda zikishuka (Mkeka wake usipotiki) hatumsaidii kumpa pole na kumwambia "Keep Change"!!!

Tupeleke lawama panapohusika Wizara ya Kilimo / Biashara na / Viwanda kwa kutokuona kujua demand inakuwa vipi na mizigo ipo vipi Uhaba wa Supply ni kosa la hawa watumishi wetu serikalini na sio jirani yangu ambaye anaona angalau haka ka-stock kake kamsaidie kupeleka mtoto shule....
Nyie ngedere ndio tunaowatafuta sana.
 
Nyie ngedere ndio tunaowatafuta sana.
Wakati mnatafutana ngedere na kupigana na kushikana uchawi ; Wachawi wenyewe wanaosababisha hii sintofahamu wanapeta kwa kuwaambia adui yako ni mwenzako na sio uzembe wao...

By the way kwanini tuishie tu kwenye Sukari ? Mfano nilikuwa naletewa sukari mpaka mlangoni. Sasa hivi nafunga genge na kwenda kupanga foreni siku nzima; nalipia bajaji na hilo gunia nalonunua limepanda bei (hio difference ni nani ananilipia) ?

Kwahio unaamini bei ya sukari kupanda inatokana watu kuficha na sio uhaba wa sukari ?
 
Back
Top Bottom