Kwanini Magufuli aliwakumbatia Machinga?

Machinga ni mtego mbaya wa kisiasa.

Rais atapata tabu kuendesha serikali yake.

Hawa watu ni wengi sana kuliko wenye ajira na biashara rasmi na wana wategemezi.

Kuna hitajika busara kukaa nao.
Kwani hawa Machinga wameanza leo au kwenye utawala wa JPM ?..... hawa walikuwapo na wataendelea kuwapo pia asilimia kubwa ya vibanda vilivyo wekwa barabarani ni wafanyabiashara wenye kipata kikubwa na sio MACHINGA halisi wanaojulikana kwa miaka yote ukweli lazima usemwe huwezi kuufanya mji kama namna ile ya vibanda banda kila corner uli ni UTAHIRA .
 
Machinga ni mtego mbaya wa kisiasa.

Rais atapata tabu kuendesha serikali yake.

Hawa watu ni wengi sana kuliko wenye ajira na biashara rasmi na wana wategemezi.

Kuna hitajika busara kukaa nao.
Kukaa nao ni kama kulea kidonda ndugu ambacho kitatuua wote..., dawa ni kuacha kuwazalisha..., Thus Serikali ifanye kazi zake kwa kuleta Sera za kumaliza tatizo na sio Shortcut na kupiga dana dana..., (yaani machinga ambao wangekuja kesho na keshokutwa badala ya kuwa machinga wawe jambo lingine)

Hio itawezekana watu wakiwa na plan B ya kufanya vitu vya kuwapatia Malazi, Mavazi na Chakula
 
Machinga ni mtego mbaya wa kisiasa.

Rais atapata tabu kuendesha serikali yake.

Hawa watu ni wengi sana kuliko wenye ajira na biashara rasmi na wana wategemezi.

Kuna hitajika busara kukaa nao.
Umeliongelea kwenye angle ya kijamii hasa mahitaji na umuhimu wake.

Je hali itakuwaje baada ya Machinga kuswagwa?
 
Katika mfumo wa demokrasia angalia kundi ambalo ni kubwa katika jamii. Hilo kundi litakuweka madarakani kama kuna haki ya kikatiba. (Pawe na haki bila kuchakachua matokeo)
 
Wanabodi,

Hebu tujuzane hapa sababu zilizopelekea Rais wa awamu ya 5 hayati Magufuli kuwalinda Wamachinga hata kwa kutengua teuzi zake mbalimbali.

Je, sababu hizo zina msingi wowote au ni huruma zake tu?

Naomba tuelimishane hapa pls

Seems Magufuli's legacy is so entrenched to the fabric of our politics that it'll take years to forget him. No day passes without any mention of him from across all walks of life in Tanzania
 
Sawa nakubali wamebomolewa lakin Tanzania/ Dar usiilinganishe na Uingereza/London hapa , Hapa anachofanya Samia just short solution for the very long coming more problems , Vijana wengi hawako na ajira especially hao graduates ipo siku atatamani kuwarudisha wamachinga kwenye maisha yao ya kawaida, labda kwa kuwa CCM haitegemei kura za wananchi powa
yVibanda vimebomolewa mji leo umekuwaq mweupe kabisa, Kweli machinga waondoke tu na JPM
 
CCM haipogo madarakani kwa sababu ya kura ya mtu yeyote yule toka mfumo wa vyama vingi uanze. Kura zake inapatikana kwa namna isiyoelezeka
Sasa huoni unapingana na wazo la kwamba alikuwa anafanya mtaji wa siasa?
 
Ile ni zuga ya JPM kuwa ana watu. Lakini kiuhalisia kura yao haina nafasi ktk ushindi wake. Sanasana angewatumia kama kichocheo cha kubadili Katiba ili atawale milele.
Kama kwenye kura ccm huwa haitegemei kura za watu, kwani kwenye kubadili katiba watu wangekuwa na umuhuimu upi?
 
Kama kwenye kura ccm huwa haitegemei kura za watu, kwani kwenye kubadili katiba watu wangekuwa na umuhuimu upi?
Wangeingia barabarani wakipaza sauti kuwa JPM aongezewe muda Kwa visingizio vya uzalendo almradi Dunia ione kuwa ni support ya watanzania kumbe ulaghai tu. Mungu aliona hila hii mapema akaona aweke rekodi sawa kablq haijaja siku iliyombaya.
 
Back
Top Bottom