Kwanini Magufuli aliwakumbatia Machinga?

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,732
29,988
Wanabodi,

Hebu tujuzane hapa sababu zilizopelekea Rais wa awamu ya 5 hayati Magufuli kuwalinda Wamachinga hata kwa kutengua teuzi zake mbalimbali.

Je, sababu hizo zina msingi wowote au ni huruma zake tu?

Naomba tuelimishane hapa pls

2ojspt.jpg

 
... in brief ni "usanii wa wanasiasa". Actually, kilichopelekea kufanya hivyo kwanza ni kwa sababu kulikuwa na walakini mkubwa uchaguzi wa 2015 so, ili kujaribu kutafuta support of the mass, machinga ilikuwa kimbilio la kwanza.

Pili, Lowasa kupanda dalala kwenye kampeni za mwaka ule kwa CCM ilionekana kama inapoteza ushawishi kwa watu wa chini, so the best option kwa CCM kujionesha bado kipo na watu wa chini na sio chama cha matajiri na viongozi kama ambavyo ilikuwa inaonekana machoni pa umma, ni lazima hadaa za kila namna ilikuwa zifanyike kujaribu kuboresha "image ya chama" na kimbilio again ilikuwa machinga, bodaboda, na makundi ya aina hiyo.

Nirudie tena, zote hizo zilikuwa hadaa tu ili kupata support ya kisiasa bila kujali athari za approach hizo! Matokeo yake umaskini umezidi kuongezeka nchini kwa kiwango cha kutisha, gharama za maisha usiombe, miji imekuwa shaghalabagala, diplomasia imevugwa kwa kwango ambacho hakikuwahi kufikiriwa, just to mention few.
 
Easier than the Alternative....

Endelea kulea tatizo miaka kumi ikiisha hilo ni tatizo la mwingine, kuliko kutatua tatizo ambalo huenda utatuzi ukachukua muda na kuja kutengemaa huenda ushaondoka, lakini maumivu na lawama zikabaki kwako...

Moral of the Story; Tatizo hili ni vigumu kutatuliwa na wanasiasa
 
Back
Top Bottom