Kwanini madawa ya tiba mbadala yana gharama kubwa sana?

tindikalikali

JF-Expert Member
Jan 14, 2011
4,855
1,117
Wakuu,

Nimekuwa nikijiuliza sana kuhusu hawa watu wanaojinadi kutibu watu kwa kinachoitwa tiba mbadala!! Gharama za dawa zao ni kubwa sana, alafu packaging mbovu na sijui kama huwa zinathibishwa na TFDA!

Utakuta dawa ya vidonda vya tumbo eti laki 3, mara kisukari mil 3! Hizi gharama zote ni halisi au utapeli tu na kutaka mafanikio ya fasta fasta?

Majuzi hapa nimesumbuliwa na tumbo, kwenda kwa hawa jamaa naambiwa et dozi 240,000... dozi miezi minne! Nililipa 60,000 nikapewa maunga hata hayaeleweki... wiki 3 nakunywa hakuna lolote! Yani yote nimeshayatupa!!
 
Ni kweli kabisa gharama ni kubwa halafu ukiangalia vizuri hizo dawa sidhani kama zinagharam kubwa wanachukua miti shamba kusaga kupata unga, kuchemsha kupata maji kutia kwenye vyupa , nenda kaulize bei utaambiwa laki. Wakati matengenezo ya dawa hata elfu ishirini haijafika, wezi wakubwa sana.
 
Tiba Si Tatizo Tatizo Ni Watoa Tiba Hawana Elimu Ya Afya, Serikali Itoe Vibali Kwa Waliosomea Kwa Kiwango Cha Diploma Na Ana Ujuzi Huo Wa Dawa Za Asili Ili Kuleta Ufanisi.
 
Ni kweli kabisa gharama ni kubwa halafu ukiangalia vizuri hizo dawa sidhani kama zinagharam kubwa wanachukua miti shamba kusaga kupata unga, kuchemsha kupata maji kutia kwenye vyupa , nenda kaulize bei utaambiwa laki. Wakati matengenezo ya dawa hata elfu ishirini haijafika, wezi wakubwa sana.
Mkuu unajua mi huwa najiuliza sana...hivi hiyo miti na mizizi vina gharama gani sana mpaka dawa tuuziwe kwa malaki?
 
Back
Top Bottom