Mzee wa Twitter
JF-Expert Member
- Nov 5, 2023
- 1,427
- 2,229
Wadau nawasabahi. Chama kikuu cha upinzania Tanzania Chadema kimetangaza kufanya maandamano ya amani tarehe 24 Januari 2024 ili kufikisha hoja zake kwa serikali na CCM ili ziweze kutekelezwa kwa haraka kwani serikali na ccm zimekuwa au hazitaki kutekeleza.
Baada ya tangazo hilo vyombo vya habari na baadhi ya watu ktk mitandao ya kijamii wamekuwa wakiilaumu chadema kuwa inataka kumwaga damu.
Najiuliza kama chadema wamesema wanafanya maandamano ya amani hiyo damu inamwagikaje? Nani atafanya vurugu ktk hayo maandamano hata damu imwagike?
Binafsi naamini vyombo vya habari na baadhi ya watu wanatumika kuyatafsiri hayo maandamano kuwa yatakuwa na umwagaji damu kama propaganda za kuwatisha wananchi wasiandamane.
Kwa uzoefu wa nchi hii vurugu za maandamano huanzia pale vyombo vya ulinzi na usalama vinapotumia nguvu kubwa kuyazuia badala ya kuyalinda na kuhakikisha yamemalizika salama kwa mujibu wa sheria kwani haki ya kuandamana ipo kwa mujibu wa katiba ya nchi. Kwa mfano maandamano yaliyofanyika wakati wa uchaguzi wa marudio jimbo la kinondoni na kumuua binti akwilina ni jeshi la polisi lililofyatua risasi na kupelekea yale mauaji. Wakati waandamanaji walikuwa hawana hata fimbo mikononi.
Ushauri kwa CCM iache siasa za kizamani za kuwatisha wananchi na kueneza hofu na uogo kwa waandamanaji kuwa maandamano yatamwaga damu. Atakayesababisha damu imwagike ni yule atakayeyazuia haya maandamano kwani ni ya amani.
Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app