anasubiri wakati wa kampeni usidhani ye mjinga unadhani kwa nini ccm wenyewe wamefyata mkia kwa EL????Hivi EL ataendelea kuteseka na kinyongo moyoni mpaka lini? Kwani asije front akawambia watanzania A-Z ya maroroso yoooote ya JK na walivyokuwa wakifanya madudu yao. Hiyo pekee ndiyo itatuthibitishia kuwa EL ni msafi na kupata tena kura yangu
<br />anasubiri wakati wa kampeni usidhani ye mjinga unadhani kwa nini ccm wenyewe wamefyata mkia kwa EL????<br />
there is something behind
<br />Kuliko kikwete,sita yaani ndani ya ccm lowasa is the best candidate,seriously i say,wengine wote wanafiki
Jenga hoja sio kukimbilia kusema anasafishwa,jenga hoja hapa,hii sio Forum ya Udaku!
Kila mtu ana haki ya kutoa maoni yake kwa mujibu wa mawzo yake kwakuwa ana utashi wake binafsi so naomba nitoa mtizamo wangu na sitatoa maoni ili kumfurahisha mtu humu ndani ya Forum ni maoni yangu na nina haki ya kuwa tofauti au sawa kimawazo na mtu yoyote.EL anaifaa Tanzania kwa sababu zifuatazo:-
Ni Kiongozi huyu shupavu,jasiri na mwenye ushawishi mkubwa ndani ya chama na serikali kwa upande wa serikali hili linadhihirika aliposhika nyazfa mbali mbali kama:-
a.Kusimamia Sekta ya Elimu ambayo ndiyo Uti wa mgongo wa maendeleo ya Taifa lolote hapa Duniani.Alisimamia kwa ukakamavu kutekeleza mpango wa kupanua Elimu ya Sekondari na alihimiza kwa nguvu zake zote ujenzi wa Shule za Kata Nchi nzima ili kuwapa Fursa Mamilioni ya Watanzania wenzetu waishio Vijijini kupata Fursa ya Elimu.
Zoezi hili lilihitaji uwekezaji mkubwa sana na Tukumbuke kwamba Taifa letu ni Maskini sana,changamoto zilizo ikabili Sekta ya Elimu kama Ukosefu wa vifaa vya maabara,Nyumba za Walimu,Madarasa ya Kutosha na upungufu wa Vitabu si kosa la mtu Fulani bali umaskini wa Taifa letu ndio maana WB na IMF hutoa misaada kwa nchi maskini kusaidia maendeleo ya Elimu kwakuwa ni Sekta inayohitaji uwekezaji mkubwa kifedha na Rasilimali zingine.
EL ni mtu anayeamini katika Elimu ndi maana motto wake ni tofauti kidogo na Motto wa Chama chake na anasema '' ELIMU KABLA,KILIMO KWANZA'' Ni kweli kabisa kwamba hakuna linaloweza kufanikiwa bila Elimu,Unaweza kuwaambia watu wasio na Elimu ya kutosha Walime Kilimo cha Kisasa?Me I agree kwamba Elimu KABLA na Kilimo Kwanza.
Mataifa Makubwa yaliondelea leo Duniani yalifanya uwekezaji Mkubwa kwanza katika Elimu,hasa Elimu ya Msingi(Kwa mfano China,Brazil na USA) na Baadaye kufanya Mapinduzi Makubwa ya Kilimo,baadaye Viwanda Vidogo na baadaye Viwanda vikubwa ambavyo vilichochea kukua kwa kasi kwa Sekta za Huduma na kupelekea mfumuko wa nafasi kibao za ajira kwa Vijana!!!
b.Kuwafukuza bila woga hadi kuwasindikiza Airport wawekezaji wababaishaji wa Kampuni ya City Water hadi kuwapandisha ndege uwanja wa
Taifa:
Akiwa Waziri wa Maji na Maendeleo ya Mifugo ,EL alitekeleza wajibu wake kwa umahili mkubwa na bila uwoga na moja ya mambo ambayo yatakumbukwa ni kufukuzwa kwa wawekezaji wababaishaji wa Kampuni ya Kitapeli ya City Water ambao walishindwa kutekeleza wajibu wao,aliwatimua na kuwasindikiza hadi Airport!EL ni Kiongozi Shupavu sana na asiyeogopa mtu!
c.Kiongozi Mwajibikaji na asiyeogopa kufanya maamuzi magumu hata kama yatamuuza
Kujiuzulu kwake kutoka katika Wadhfa wake wa Uwaziri Mkuu kufuatia Kashfa ya kampuni ya kufua umeme ya Richmond inachukuliwa na wengi kama kuhusika kwake katika Saga hilo.Napenda kuwakumbusha Watanzania wenzangu kwamba Waziri Mkuu ndiye mtendaii Mkuu wa Shughuli za Serikali na mtekelezaji wa Maagizo ya Baraza la Mawaziri ambacho kimsingi ndicho chombo kikubwa cha Utendaji wa serikali (Govt. Machine) na hivyo kama kuna Kosa linafanyika basi Linatosha kuiangusha Serikali nzima so katika SAGA ile ilibidi Serikali Nzima akiwa ni Pamoja na Rais wajiuzuru lakini EL akubali mwenyewe kwa ajili ya kulinda heshima ya Chama chake na Serikali, huu ni mfano mzuri wa kuigwa kwa Waafrika wote.
Siku zote tatizo letu waafrika ni kukosa kuwajibika pale inapobainika uzembe umefanyika,ukweli umebaki kuwa wazi mpake leo hii NCHI IPO GIZANI migao ya Umeme inaendele kama kawaida na dada wa Richmond ambaye ni Dowans Mitambo yake inawashwa na tumerudi pale pale!! Mimi nasema kwa kosa la Richmond,Serikali nzima ilikuwa imeanguka.
d.Mfuatiliaji na asiyechoka kufuatilia kero za na hakai ofisini kungoja taarifa
Wakati wa janga la Njaa lilisababishwa na ukame kwa msimu wa mwaka 2007/08 ni huyu EL alikuwa akishirikiana na Wakuu wa Wilaya zote zenye njaa na wakati mwingine alishiriki yeye mwenyewe kupita nyumba kwa nyumba kusimamia zoezi la ugawaji wa chakula kwenye Familia zenye njaa ili kuhakikisha kwamba azma ya serikali ya kwamba hakuna mwananchi atakayekufa kwa njaa inatimizwa ni huyu huyu EL.
Mtu hawezi kukosa mapungufu hata siku moja,nakubali ana mapungufu yake lakini EL ni embe dodo lililoiva tayari kuvunwa na Watanzania Mwaka ukifika 2015.
Nawaleteeni EL
Sasa kazi imeisha kukamilika,Habari zilizotufikia zinasema,Kundi la Wabunge wafuasi wa EL wamekamilisha Ushahidi na Nyaraka zote kuhusu Sakata linalomkabili aliyewashi kuwa Spikaaaa wa Bunge letu la Tanzania Mhhhh.Pyuuusi Msweeekwa na zitawsilishwa kwenye kikao cha NEC mwezi Ujao.Wabunge hao wakiongozwa na Mbunge mwanamke aliyetokea kuwa machachari sana wameapa kwamba siku ya kikao Hicho na Mh.Msweeekwa nayeye atang'olewa madarakani kabla hajaanza kuendesha kikao Hicho.
Wachunguzi wa masuala ya Kisiasa wanasema,Kutakuwa na MALUMBANO makali kati ya Wafuasi Wabunge ambao ni Wafuasi wa EL na Kambi ya Wavua Magamba inayoongozwa na '' Naye Huyooo Peke yakeee'' na wamemwonya Mwenyekiti kujiepusha Mbali na Makamu wake huyo ili kuzuia Malumbano makali ya Kambi hizo.
EL ,Moja ya Wanasiasa Jabali na Kisiki ndani ya Sisiema,ameapa kwamba atafichua kile kinachosemwa na wengi ''SIRI NZITO'' na huenda pakatokea Patashika na Ghasia kubwa sana siku ya kikao hicho..
Karibuni