MTAZAMO
JF-Expert Member
- Feb 8, 2011
- 19,644
- 33,451
- Thread starter
- #41
Safi ni mwendo wa nondozz ndio raha ya JF ....Huo ni uchambuzi wako wa kitaalamu kiuchumi au nawe unasukumwa na hisia za kisiasa.
Moja ya vichocheo vya kukua kwa uchumi ni ubora, uimara na uwezo wa miundo mbinu. Mali yoyote haina thamani kama jinsi ya kuifikia ni shida.
Kwafano kilimo hakitakuwa na tija kama mazao hayataweza kuondolewa mashambani na kufikishwa sokoni kwa wakati na ubora ule ule. Vivyo hivyo mbuga zetu hazina thamani kama hakuna njia rahisi (kwa gharama ndogo na uhakika, nk) ya kuzifikia. Mfano ni Kisiwa cha Rubondo, Ziwa Victoria, Mkoa wa Geita, ambacho kina kila aina na sifa za utalii wa samaki na ndege. Je, nani anakifahamu. Na anayekifahamu kufika huko ni shida. Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Chato unabezwa, kwa sababu tu ndio kwao na Rais!
Sent using Jamii Forums mobile app