Kwanini gharama za maisha hazijawi kushuka ni kupanda tu?

TRABSOH

JF-Expert Member
Jun 9, 2023
339
546
Habarii.

Tuliondoa makabila na jamii ndogo tuwe Taifa ili kuwa na nguvu lakini hiyo nguvu iko wapi leo ndani ya miaka 61 ya uhuru na watu million 60 plus?, nasikia wanasemeaga nguvu kazi ikiwa kubwa ndo na Taifa linaimarika zaidi sisi hawa watu million 60 wanachagiza ukuaji wa nini? Nini maana ya kuwa Taifa ikiwa maisha kila siku hayana matumaini? Hata chakula changamoto kwa baadhi ya watu, nishati changamoto, usafirishaji changamoto hata mental health changamoto! Machizi ni wengi kuliko wazima. Ama ndo wingi si hoja?

Wataalamu wa uchumi mnisaidie kwanini Tanzania kila awamu gharama za vitu inapandaa tuu bila balance na maisha ya wanachi kupanda pia , graph aijawai kushuka hii toka nipate akili.

Miaka miwili tu ya mama samia nauli ,sijui vyakula, sjui gharama za mawasiliano vyote vimeenda juu, hakuna pa kushika jua kali sana tumboni na mifukoni.

Hivi I haliii ni lazima itokee na haiwezi kuzuilika? Huko mataifa ya wenzetu mambo ni haya haya au wao wanabalance veep maisha ya watu na gharama za maisha,

Haiwezekani Taifa letu kufikia siku vyakula na gharama zingine zikashuka kwenye kiwango ambacho kila mtu aka feel life limekuwa rahisi? Kila awamu ni afadhali ya jana

Tiba ya haya ni nini au ndo tusubiri yesu ashuke hakuna wa kututoa huku.
 
Kwa sababu tuna viongozi walafi, wanafiki, wanajali maslahi yao sio ya taifa.
Huu ndio uhalisia.

Mengine yatakuja ila sababu kuu itabaki hapo, hata katika kipindi kigumu serikali haichukui hatua stahiki, mafuta yakipanda wao hawawezi kujibana, bado matumizi ya serikali ni ya juu mnoo, kiongozi kutembelea landcruiser ya milioni 400 ni kawaida, wakati taifa ina vipaumbele vingi mnooo kuboresha hali ya maisha ya mtanzania.
Barabara mtihani, afya shida..
 
Wanaweza kuja na ngonjera zingine lakini jibu halisi la maisha magumu Tanzania ni urafi wa viongozi wa ccm,ukosefu wa ubunifu na ubinafsi uliopitiliza
 
Wanaweza kuja na ngonjera zingine lakini jibu halisi la maisha magumu Tanzania ni urafi wa viongozi wa ccm,ukosefu wa ubunifu na ubinafsi uliopitiliza
Viongozi wanawezaje kutawala wananchi? Au ndo wananchi wengi ni wajinga wasioweza kuonesha nguvu yao juu ya viongozi wao waliwachagua wenyewe wawe wawakilishi... Mbunge ajaleta alichoahidi mnakubali veep aje ata kusimama tena mbele yenu bila kumpigia ata mijiwe?
 
Back
Top Bottom