Kwanini Comedians wa MIZENGWE wanapotezewa sana?

Kwani Lazima kuiga kila kitu? Sababu Mr Bean kafanya vile imekua sheria kwamba hata wachekeshaji wabongo waige? Halafu Mr Bean ni vitendo wakati Hart ni maneno huoni kwamba unaji contradict mwenyewe vipi watu wasioelewa lugha anayotumia Hart(English). Unajidai wa mbele wakati unaishi Ombokoro
huyu jamaa sijui wa wapi yani kanikera kweli kwa comment yake lazma atakua Nshomile huyu lazima tu. Anataka kutuaminisha kuwa kitu kuwa kizuri ni mpaka yeye akipende. Kuku sana huyu jamaa
 
Majibu yake ni marahisi kama siyo mepesi sana Mkuu....

Hawa ' Jamaa '....

  1. Hawajui ' kujipendekeza ' wala ' kujikomba ' kwa Mtu na hawaendekezi sana ' njaa '.
  2. Wanapambana sana na kujituma mno wenyewe.
  3. Hawataki kujihusisha na kuwa ' mabegi ' ya Drugs barons wa Tanzania kama wanavyofanyiwa wengine.
  4. Wanaridhika na kumshukuru Mwenyezi Mungu sana kwa chochote kile anachowapa kwa ' Jasho ' lao na kamwe hawapendi ' magumashi ' kama wenzao wengi.
  5. Tungo zao nyingi tena 100% ni za ukweli mtupu na usisahau kuwa 100% ya Watanzania hatupendi kuambiwa ukweli.
Mzee umelenga mulemule!
 
kila jumapili sikosi kuangalia, nikikosa hata roho huwa inaniuma
 
Mkuu umeandika vyema mno. Hili ni kundi pekee ambalo nikirudi bongo huwa nalifuatilia sana. Wapo natural sana.
 
Kwani tanzania kuna Comedian?
hahaaaaa wajifunze kwa wenzao basi
sio kuchekesha maneno bali vitendo. kama maneno kwa asiejua lugha hiyo je?
hawaoni wanavochekeaha wenzao kina Mr Bean kina Chaplain au Kelvn Hart...
ndomaana me siangaliagi utumbo huo wa Mizengwe nk.
mizengwe ukweli wapo vizuri hawalazimishi watu kucheka ila utacheka mwenyewe tu alafu wamebezi kwenye reality achana na zecomedy kijiwe cha misifa na majungu wao kusema watu
 
Kwani tanzania kuna Comedian?
hahaaaaa wajifunze kwa wenzao basi
sio kuchekesha maneno bali vitendo. kama maneno kwa asiejua lugha hiyo je?
hawaoni wanavochekeaha wenzao kina Mr Bean kina Chaplain au Kelvn Hart...
ndomaana me siangaliagi utumbo huo wa Mizengwe nk.

We jamaa unijifanya mjuaji kumbe mshamba tu, majina yenyewe umekosea sidhani hata kama unawafatilia hao watu uliowataja
 
Thamani yako unayo wewe mwenyewe, labda kuanzia maisha yao halisi hawajayapata thamani wanayo staili au labda hiyo ndio thamani yao
 
Kwani tanzania kuna Comedian?
hahaaaaa wajifunze kwa wenzao basi
sio kuchekesha maneno bali vitendo. kama maneno kwa asiejua lugha hiyo je?
hawaoni wanavochekeaha wenzao kina Mr Bean kina Chaplain au Kelvn Hart...
ndomaana me siangaliagi utumbo huo wa Mizengwe nk.
Sasa sijui unataka tuambia huyo Kevin Hart huwa anafanya vitendo bila maneno kwenye stand up comedy. Nahisi hujui unachokizungumzia.
 
Hawatafuti kiki... Na ndivyo inavyotakiwa maana mwisho wa kiki ni kuangukia pua na kupotea...
Waendelee hivyo hivyo wafuatiliaji tupo
 
Majibu yake ni marahisi kama siyo mepesi sana Mkuu....

Hawa ' Jamaa '....

  1. Hawajui ' kujipendekeza ' wala ' kujikomba ' kwa Mtu na hawaendekezi sana ' njaa '.
  2. Wanapambana sana na kujituma mno wenyewe.
  3. Hawataki kujihusisha na kuwa ' mabegi ' ya Drugs barons wa Tanzania kama wanavyofanyiwa wengine.
  4. Wanaridhika na kumshukuru Mwenyezi Mungu sana kwa chochote kile anachowapa kwa ' Jasho ' lao na kamwe hawapendi ' magumashi ' kama wenzao wengi.
  5. Tungo zao nyingi tena 100% ni za ukweli mtupu na usisahau kuwa 100% ya Watanzania hatupendi kuambiwa ukweli.
No.3
 
Jamaa wanajitahidi sana...haswa Sumaku ni moja Waigizaji wanaonivutia ndio maana huwa nafuatilia huu mchezo, ila nadhani Sumaku hatumiki fully kwa uwezo alio nao.

Huwa namsikia hata kwenye michezo mingi ya redio kwenye redio tofauti tofauti...kwa sasa kuna mchezo wa redio RFA namsikia unaitwa 'kumekucha' I think.

ILA UKWELI LAZIMA USEMWE JAPO NI MCHUNGU

Hawa jamaa wananikera sana...wapo hewani kwa muda mrefu, zaidi ya miaka kumi sasa kama sikosei lakini sioni maendeleo yoyote haswa kwenye sanaa wanayoifanya...production bado ni poor na ya kimasikini sana.

Inakera kuona kipindi kikongwe na waigizaji wakongwe wa kiwango kile kutengeneza mchezo unaohitaji kuonyesha tukio la siku tofauti na Waigizaji wanashindwa hata kubadili nguo..ile sio stage play, ingawa hata stage play wanafanya zaidi ya hapo.

Production kwa sehemu kubwa inafanywa nje (outdoor) kwa lengo kubwa la kukwepa gharama, haya si ya kufanywa na kundi kama lile tena wanaofanya kazi na TV kubwa kama ITV. Tatizo ni nini? vifaa? sasa kama wao inawashinda hao underground wataweza vipi iwapo watasema tunataka kuwa kama Mizengwe?

Kuna mdau hapo juu naona ameshauri waongezewe muda...nadhani ameshindwa kunotice kwamba jamaa hawana 'content' inayotosheleza, ubunifu unagotea hapo na kwamba wanategemea sana uwezo wa Muigizaji binafsi kusukuma muda, ndio maana utaona huwa wanavuta muda sana kabla kuanza kipindi ili walau wafikie muda..kile kipindi ni cha nusu saa kutoka tatu kamili au na dakika mpaka tatu na nusu, lakini hawajazi huo muda wewe unasema waongezewe.

Sasa sijui tatizo lao haswa ni nini, huwa mpaka najiuliza kama Mzee mengi kweli huwa anajali ni nini kinafanyika kwenye kampuni yake. Labda wanakosa washauri wazuri au wao wenyewe hawana cha kushauriana na kampuni yao (ITV)

Sifa kuu ya binadamu/kazi/biashara yoyote ni kukua kutoka ulivyokuwa awali, hata binaadamu asiye 'grow' hana lolote la kufunza wengine.....Wanaofuatilia Isidingo hapa hebu waniambie jinsi inavyoenda ikibadilika, sio lazima waigizaji wabadilishwe lakini walau production, mandhari n.k.
 
Back
Top Bottom