Kwanini CHADEMA hawaadhimishi siku ya kuzaliwa kwake?

Hebu jiulize siku ya kuazimisha Uhuru hela ilitumika bilioni 68 wakati huo kuna wanafunzi wamenyimwa mikopo pua kuna akina mama wanakufa kwa kukosa dawa Hospitalini.CCM imetumia gharama nyingi sana kuazimisha siku ya kuzaliwa kwa chama wakati huohuo kuna wagonjwa wengi hospitali ya Maweni Kigoma wamekosa dawa,Umeme wa Kigoma hauko kwenye Grid ya Taifa harafu leo ccm inajenga hoja ya kijinga.Ni sawa na kutembeza Mwenge kwa mabilioni ya watanzania harafu mwenge huo unakuwa kielelezo cha kuzindua mradi wa laki 8.Chadema tuna mambo ya umma tunayatanguliza mbele kuliko sherehe zisizokuwa na tija
 
Wana jf kwanini CHADEMA hawaadhimishi siku ya kuzaliwa kwake?
Fedha zinatumika kuwafikia wananchi badala ya kuchezea. wangefanya hivyo, hata hili swali usingeuliza, maana wangekuwaawa na TLP au UPDP
 
Mpaka mtei akubari maana ni mali yake mkubwa chadema ni sawa na saccos hawakumbuki tarehe ya kuzaliwa wanakumbuka maandamano na matusi bungeni!
 
Chadema haiwezi kuadhimisha siku ya kuzaliwa maana haifahamiki ilianzishwa lini na nani. Hata bendera yao yenye rangi nyekundu iliibuka wakati wa uchaguzi lakini ukiangalia wakati inaanzishwa haikuwa na hii bendera. Kituko kingine ni itikadi. Chadema ilianzishwa ikiamini katika ubepari kwani mwasisi wake edwin mtei hakukubaliana kabisa na baba wa taifa katika ujamaa na hata alifukuzwa uwaziri wa fedha kwa kukubaliana zaidi na imf. Lakini siku za karibuni chadema inaimba sana ujamaa majukwaani ingawa maisha ya viongozi wao hayafanani na ujamaa

Vipi, CCM? Itikadi ni ipi (kwenye vitabu) na wana-practice nini? Miaka 36 tangu kuanzishwa kwa CCM, na muda wote huo wamekuwa wanaongoza nchi, je, unaweza kusema dira ya nchi hii ni ipi?

Kuna jambo jengine ambalo linashangaza kidogo, CCM wamefanya sherehe za miaka 36 nation-wide, lakini hata matawi ya nje pia. (fine). Kwa kawaida, sherehe kubwa za maadhimisho (anniversary) huwa ni miaka mitano-mitano e.g 5yrs, 10yrs, 15yrs, 35yrs etc.

Kelele za 36yrs zinaashiria 'tatizo' na hapa naamini wale 'ma-consultants' wa CCM wamekuja na proposal ya ku-reband (wengine watasema re-launch) the party! The question is, CCM as brand inauzika tena? Ni kitu gani kilichofanya hadi chama kitumie nguvu kubwa kuji-brand? Na solution ya CCM ni re-branding kwa mtindo wa sherehe nchi nzima?
 
waadhimishe ili iweje, chama bado kinajengwa kama ni gorofa la floor kumi ndio kwa nza liko kwenye floor ya ya tisa
 
Kusoma hujui hata picha huoni? Ni mara ngapi ulimwona Rais Barrack Obama akihangaika na siku ya kuzaliwa chama chake cha Demokrasia kila mwaka kama mfanyavyo magamba?

CHADEMA hatufanyi vitu kimbulula kama ninyi, wananchi wanatakiwa waletewe maendeleo ya kweli.Siyo kuua reli kisha unaikarabati kidogo kwenye anniversary huku mkiimba...nataka kulewa eeh,nataka kulewa ili nimwage radhi mkiongozwa na Diamond.

Polisi wanapigwa na raia, makazi yao ni duni, vifaa vya kazi havijitoshelezi, vituo vyao vinachomwa kisa sakata la gesi magamba umevaa usiri kwenye mikataba. Lakini Amiri jeshi mkuu mnakaa nae huko,mnakula pilau na mkiserebuka na kulewa mnataka CHADEMA tuwaonee wivu wa kijinga thubutuuu. Hapa ni kazi tu mpaka kieleweke 2015, magamba wenzenu wamefukuzwa na nyuki huko wilayani Meatu mkutanoni.
 
sasa mkuu,,chama kilianzishwa sebuleni tu watu wakigonga mbege unategemea watakuwa na kumbukumbu gani?
 
Acha uka-cameroon, sasa kingesajiliwaje?

Chadema haiwezi kuadhimisha siku ya kuzaliwa maana haifahamiki ilianzishwa lini na nani. Hata bendera yao yenye rangi nyekundu iliibuka wakati wa uchaguzi lakini ukiangalia wakati inaanzishwa haikuwa na hii bendera. Kituko kingine ni itikadi. Chadema ilianzishwa ikiamini katika ubepari kwani mwasisi wake edwin mtei hakukubaliana kabisa na baba wa taifa katika ujamaa na hata alifukuzwa uwaziri wa fedha kwa kukubaliana zaidi na imf. Lakini siku za karibuni chadema inaimba sana ujamaa majukwaani ingawa maisha ya viongozi wao hayafanani na ujamaa
 
wataanzimisha mwaka huu kwasababu wanafikisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwake..
 
Wana jf kwanini CHADEMA hawaadhimishi siku ya kuzaliwa kwake?

Wataonesha mafanikio yepi? labda ya kukopa na kujengea majumba mahawara? au watatuonesha malumbano ya kina Ben eight o'clock na Zitto?

Au watakuja watwambie kuna makontena (hewa) yameshikwa Tunduma? labda watasema "tumesusa"?
 
Chadema nacho chama jamani hadi kifanye sherehe pesa zote za chadema babu amejikopesha ndizo anazotumia na nyumba ndogo josephine huku mama watoto wake akiteseka pole sana wana cdm.
 
Kwanza CHADEMA hakikuzaliwa, hakina babu wala bibi ni chenyewe tu na Watanzania. Pili hata kama ingekuwepo si Muhimu kama kwa hali ya Tanzania ya sasa.
Yapo ya muhimu kuyafanya.
 
Back
Top Bottom