Kwanini bank hela nyingi zikiwekwa ghafla kwenye akaunti unafuatiliwa sana!!?

BRO SANTANA

JF-Expert Member
Jun 15, 2015
1,845
2,245
Habarini ndugu zangu.
Mimi huwa nasikia kwamba endapo akaunti yako ya bank haijawahi kuwekwa hata mil 5 toka ifunguliwe na ina muda mrefu lakini ghafla ikaingizwa mil 100 au zaidi wanaanza kukufuatilia sana tena wakishirikiana na serikali.
Wakati wakubwa hata hawaulizwi maana zinaingia za escrow,richmond,epa lakini kimya.
Naomba kujuzwa juu ya hilo.
 
mkuu kuna nature na behaviour za transaction. na sio kila ukifanya hivo serikali inataarifiwa. Benki yenyewe inavyombo vyake achilia ile sfi. Uwe na aman kama umeuza mazao yako bei ya dhahabu we katie mzigo benki. Hela chafu ndio uwe makini.
 
ni kwa sababu banks zinatakiwa kisheria kureport pale panapokua na wasiwasi mteja anajaribu kuficha chanzo cha fedha zilizopatikana kwa njia chafu au pale banki inapokua na wasiwasi kua fedha zinalenga kuchangia au kufadhili ugaidi.Na mojawapo ya viashiria ni hiyo ya akaunti kupita kiasi ambacho hakiendani na miamala ya kawaida ya mteja.
 
Mie niliingiza 20m wakati wa kuchukua bank wakawa wanataka vielelezo nimepata wapi fedha wakati account yangu ni ya mshahara na haizidi laki 5.

Raia pangu pakavu ndio tunaonyanyashwa wenzetu wameenda na viroba,masandarusi,masafleti,mabox na magunia wamebeba pesa bot kimya pamoja na ukiukwaji Mkubwa wa mihamala.
 
Habarini ndugu zangu.
Mimi huwa nasikia kwamba endapo akaunti yako ya bank haijawahi kuwekwa hata mil 5 toka ifunguliwe na ina muda mrefu lakini ghafla ikaingizwa mil 100 au zaidi wanaanza kukufuatilia sana tena wakishirikiana na serikali.
Wakati wakubwa hata hawaulizwi maana zinaingia za escrow,richmond,epa lakini kimya.
Naomba kujuzwa juu ya hilo.

Siku hizi benki zote duniani ziko kwenye mtandao mmoja wa kufahamishana transactions kubwa kubwa zisizoelezeka kwa ajili ya:

  1. Kuzuia usafishaji wa fedha chafu/haramu (kama za kuuza unga) - money laundering.
  2. Kudhibiti fedha zinazotumika kwa kufanyia terrorism.

Kama wewe una ka-akaunti kasikozidi hata milioni moja halafu ghafla unaweka milioni 100, saa hiyo hiyo vyombo vya usalama vitafahamishwa na benki na pengine utakapokuwa unaondoka hapo benki kuna watu (usalama wa taifa) watakufuatilia kiupelelezi ili wajue wewe ni nani, unakaa wapi, unafanya kazi gani , marafiki zako ni nani, na mawasiliano yako na ya watu wote wengine kwa simu na internet yatakuwa yanafuatiliwa in real-time.

Hiki sio kitu kibaya kwa kweli. Kwa sababu kama hela zako ni safi (umeuza shamba, umepiga consultancy moja kubwa ukapata hela kwa mkupuo, nk.) basi usiwe na wasiwasi utakuwa salama. Haya yanafanywa kwa usalama wetu wote.

Nashauri kama unaona vyombo vya usalama na sheria vinakufuatilia na kukuhoji, ni vema uweke mwanasheria standby ili hawa watu wasije wakakutega na kukudhulumu fedha zako (ingawaje sidhani kuwa ni lazima).
 
Hata ukitaka kutoa kiwango fulani kikubwa cha fedha, ni lazima pia wazitaarifu mamlaka juu ya hilo na hata muda unaopewa kuzitoa sio kama ule unaoweza kutumia kutoa mil 5.
Na hiyo inaaply hata kwa kampuni kubwa kabisa kama Mohamed Enterprises au Azam. Ni jambo la kawaida.
 
Mtu binafsi mwenye akaunti isio ya kibiashara basi wana kiwango cha juu wanachoweka cha kutoa. Nitakupa mfano wa marekani: Kama umeweka hela kwa hundi ya uhakika (kama cashier's check) basi unaweza kutoa mara moja $5000 (Tsh. Milioni 9) tu. Fedha za ziada unaweza kuzitoa baada ya wiki moja. Baada ya wiki unaweza kutoa kiasi kikubwa lakini kikizidi $10,000 (Tsh. Milioni 18) basi ujue watakufuatilia wajue unafanya shughuli gani. Samahani sijui hivi viwango kwa bongo siku hizi.

Hapa namaanisha cash transactions katika benki. Kama unatumia hundi kufanya malipo au manunuzi basi hakuna kiwango, na kama kipo kitakuwa ni kikubwa sana mimi sijakutana nacho.

Kama wewe ni mfanya biashara, hasa bongo basi hawafuatilii. Mara nyingi wafanya biashara wakubwa wala hawaendi benki. Anaagiza tu kwa meneja kuwa nileteeni milion 50 ofisini. Au wanaweza kutuma makarani wao na ulinzi kwenda kuchukua fedha nyingi tu (kwa mfano kwa ajili ya kulipa mishahara). Hii ni kwa sababu shughuli zao zinafahamika kwa hiyo hakuna wasiwasi kama hizo hela zitatumiwaje.
 
Habarini ndugu zangu.
Mimi huwa nasikia kwamba endapo akaunti yako ya bank haijawahi kuwekwa hata mil 5 toka ifunguliwe na ina muda mrefu lakini ghafla ikaingizwa mil 100 au zaidi wanaanza kukufuatilia sana tena wakishirikiana na serikali.
Wakati wakubwa hata hawaulizwi maana zinaingia za escrow,richmond,epa lakini kimya.
Naomba kujuzwa juu ya hilo.

Ndio maana tunataka CCM itoke madarakani
 
Habarini ndugu zangu.
Mimi huwa nasikia kwamba endapo akaunti yako ya bank haijawahi kuwekwa hata mil 5 toka ifunguliwe na ina muda mrefu lakini ghafla ikaingizwa mil 100 au zaidi wanaanza kukufuatilia sana tena wakishirikiana na serikali.
Wakati wakubwa hata hawaulizwi maana zinaingia za escrow,richmond,epa lakini kimya.
Naomba kujuzwa juu ya hilo.

Yah ni kwel ndo maana bot walianzisha kyc ila bank zingine hawafuati.hii kwa ajili ya kuzuia money laundering,ugaid nk.
 
Back
Top Bottom