WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 956
Mapenzi ni dhana pana - hakuna ubishi kwa hilo.Ila naona wakati mwingine baadhi yetu tunachanganya au kushindwa kutofautisha baina ya mapenzi na vitendo au viashiria vya mapenzi.Hii imejitokeza mara nyingi hapa jamvini na hata sasa kuna mada inaendelea kuhusu makabila yanayojua na yasiyojua mapenzi! Hivi kweli binadamu kamili aliyeumbwa na Mwenyezi Mungu anaweza akakosa kujua mapenzi?