Hatua 6 za kujenga uwezo wa kujipenda na kujiamini katika maisha yako

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
9,528
14,412
Hatua hizo 6 ni kama ifuatavyo

1.FAHAMU UNAAMINI KITU GANI KUHUSU WEWE MWENYEWE
Watu wengi huishi bila kujua wanaamini kitu gani bali hujikuta wanafanya vitu kwa mazoea bila kujua nini chanzo cha wao kufanya hivyo.
Kuna imani umejenga juu yako kuhusu mtu mwenye kujiamini yupoje na upo na kila sababu ya kuona huna vigezo vya kujiamini kama wengine

Kwa tafiti zinaonyesha kwamba 95% ya watu duniani wanasumbuliwa na tatizo la kukosa kujiamini ,wewe mwenyewe ni shahidi kwamba haujiamini vya kutosha pamoja na kwamba watu wengine wanadhani unajiamini.

Fikra hizo potovu ni kama vile
1.Watu wakinijua uhalisia wangu hawawezi kunipenda
2.Nikiwa pamoja na watu wanaofanya kazi kama yangu huwa naona wao wanastahili wadhifa walionao kuliko mimi
3.Nahofia sana watu wengine watagundua kwamba kuwa uwezo wangu ni mdogo sana tofauti na wao wanavyofikiria

4.Siamini kama mafanikio yangu yanaweza kudumu muda mrefu
5.Sioni kama mafanikio yangu yana maana yoyote kwangu

6.Najiona sistahili mafanikio ambayo nipo nayo
7.Hata kama watu wengine wananipa pongezi juu ya uwezo wangu na mafanikio yangu sioni fahari kwa mafanikio yangu kama wao wanavyofikiria

8.Huwa ninashusha thamani kazi zangu na mafanikio yangu mara kwa mara tofauti na watu wengine wanavyofikiria
9.Kama watu wengine wakinipa pongezi kwa mafanikio yangu huwa napata hofu kuwa sitoweza kutimiza matarajio yao kwa siku za baadaye kama wao wanavyofikiria
10.Ninajenga hofu kubwa kwamba watu muhimu katika maisha yangu watagundua kwamba sina uwezo mkubwa kama wao wanavyofikiria

Hizo fikra potovu huitwa IMPOSTER SYNDROME ni tatizo ambalo huwasumbua 77% ya watu wenye mafanikio makubwa sana duniani.Kwa undani zaidi tuwasiliane.

VYANZO VYA FIKRA POTOVU ZENYE KUZUIA KUJIAMINI NI
Fikra hizo potovu hujengwa kwa muda mrefu sana na huathiri maisha ya mtu kila idara

a.KUJIONA UPO NA DOSARI NYINGI SANA ZA MUONEKANO
Kila mmoja wetu yupo na mapungufu ya muonekano ambayo anaona aibu sana yakitajwa na mapungufu hayo yanaweza kuwa
Kujiona mwenye saizi kubwa sana au ndogo sana ya pua, mdomo, macho, paji la uso, kichogo,kujiona upo na mpangilio usiovutia wa nywele,meno,kucha, kujiona mfupi sana au mrefu sana,kujiona mwenye ngozi tofauti sana na wengine,kujiona mnene kupita kiasi au mwembamba sana,kujiona mwenye ugonjwa wa ngozi wenye kutia aibu mbele ya wengine,kujiona upo na sauti au lafudhi yenye kutia aibu ukianza kuongea.

Eneo hilo linaweza kuathiri uwezo wa kujiamini bila kujali elimu, kipato,cheo, umaarufu,nguvu ya ushawishi n.k

b.MATATIZO YA KIFEDHA
Unaweza kupoteza uwezo wa kujiamini mbele ya wengine kwa sababu unapitia kipindi kigumu sana kifedha.

unaweza kupitia kipindi kigumu sana kifedha kwa sababu zifuatazo
#Kulipwa fedha ndogo sana kwa mwezi kwenye ajira au kibarua,kuwa na madeni makubwa sana,kukosa ajira au kukosa kazi ya uhakika

#Biashara kukosa wateja, kufukuzwa kazi, gharama za maisha kuongezeka sana bila kipato kuongezeka, kustaafu bila maandalizi, kucheleweshewa malipo yako,watu kukopa pesa zako lakini hawarudishi,talaka, kutengana na mwenza wako n.k

Hivyo ukiwa mbele ya watu wengine unahisi watajua hali halisi ya kipato chako hivyo unakuwa unaona aibu muda wote.Unapunguza sauti yako au kuongea kwa ukali sana au kufoka au kubadilisha mada.

C.KUFANYA KAZI CHINI YA VIWANGO
Kama unafanya kazi chini ya viwango utajikuta huipendi kazi yako,unakosa utulivu kazini,unafanya makosa yenye kujirudia rudia ofisini,unakosa usingizi au kulala sana mpaka unachoka, kujitenga kazini,kukataa msaada au ushirikiano na wengine,kuwa mkali kupita kiasi ukikosolewa.

Kufanya kazi chini ya viwango hushusha uwezo wa kujiamini,hata kwenye vikao vya kiofisi unakosa sauti ya kueleza kuhusu utendaji wako,muda wote hofu ya kufukuzwa kazi inazidi kuongezeka,mtu yeyote akicheka hoja yako kwenye vikao unahisi anakudharau .

D.MATATIZO YA KIAFYA
Unaweza kupoteza uwezo wa kujiamini kwa sababu ya matatizo ya kiafya kama vile kupoteza uwezo wa kuona au kusikia kwa ufasaha, màumivu ya kichwa na mgongo,ugonjwa wa moyo,miguu kuvimba ,fangus,kutokwa na harufu fulani yenye kusababisha watu wengine kulalamika uwepo wako,ugonjwa wa ngozi wenye kutia aibu mbele ya wengine n.k

E.KUWA KATIKA MAHUSIANO YENYE MIGOGORO
Unaweza kupoteza uwezo wa kujiamini mbele ya wengine kama kila mtu anamsifia sana mwenza wake lakini wa kwako anakusumbua sana ,hivyo unaweza kukaa kimya muda wote,kuongea kwa sauti ya ukali kupita kiasi, kuondoka katikati ya mazungumzo, kujitenga,kukwepa mada za mapenzi.

Vilevile kuwepo katika mazingira yenye taharuki kazini labda kila siku kazini kwako unafokewa, kutukanwa kudhalilishwa hadharani, kufanywa kichekesho, kuzushiwa uongo, kukosolewa kupita kiasi hali hiyo husababisha unapoteza uwezo wa kujiamini mbele ya wengine.

2.MATUKIO YA KIHISTORIA
Unaweza kupoteza uwezo wa kujiamini ukiwa mbele ya wengine kwa sababu zifuatazo
Labda UMEZALIWA katika familia yenye sifa zifuatazo
a.Umasikini kupita kiasi
Umasikini kupita kiasi husababisha mtu kukosa chakula kizuri,kuvaa nguo chafu,kutembea bila viatu,kukosa mahitaji muhimu ya shuleni,kukosa zawadi ukifanya vizuri,kukosa mtu wa kujali mafanikio yako shuleni kwenye mahafali n.k

Hali hiyo husababisha unapoteza uwezo wa kujiamini ukiwa na mwenza au marafiki ambao wanajisifia sana kuhusu kudekezwa na wazazi wao,mara kwa mara utakaa kimya,unakwepa mada za kuhusu maisha ya utotoni, kuonekana upo busy sana hutaki mazoea na mtu yeyote.

b.WAZAZI WENYE UGOMVI
Kama wazazi wako utotoni mwako walikuwa na ugomvi wa mara kwa mara huwezi kupata ujasiri wa kumtambulisha mtu yeyote kwa wazazi wako.Vilevile utakuwa unakwepa masuala ya marafiki au mwenza wako kutaka kumjua mzazi au wazazi wako na mara kwa mara utakuwa unakuja na visingizio mbalimbali ili kuzuia kumpeleka kwa wazazi wako kuepuka aibu ya maneno makali ambayo mzazi au wazazi wanaweza kuongea mbele ya wageni au marafiki zako

Vilevile unaweza kupoteza uwezo wa kujiamini kama wazazi wako wapo na tabia zenye kutia aibu mtaani,

Unaweza kupoteza uwezo wa kujiamini kwa sababu wazazi wako walitengana,kupeana talaka,au hujui mzazi wako labda mama au baba wapi alipo labda hujawai kumuona tangu uzaliwe.

Vilevile tabia kama ulevi kupindukia,wizi,kamari, kutembea na watoto wadogo kimapenzi ikiwa ni tabia ya mzazi unaweza kupoteza uwezo wa kujiamini mbele ya wengine.

C.MANYANYASO
Unaweza kupoteza uwezo wa kujiamini mbele ya wengine kwa sababu utotoni mwako umeishi huku unafokewa, kutukanwa, kudhalilishwa, kufanywa kichekesho, kuzushiwa uongo, kukosolewa kupita kiasi,kuitwa majina ya aibu hali hiyo husababisha unakuwa unajisikia vibaya sana mara kwa mara ukifanya makosa.

3.FAHAMU MAPUNGUFU YAKO
Walisema wahenga kwamba kama hakuna adui ndani yako adui kutoka nje yako hana madhara.Watu waliokuzunguka wanaweza kujenga urafiki na wewe ili kujua udhaifu wako upo wapi ili watumie udhaifu wako kushusha uwezo wa kujiamini.

Zingatia kwamba hakuna binadamu aliyekamilika wala asiefanya makosa hivyo makosa yako ya utotoni,aibu zako za utotoni, historia yako yenye maumivu watu wengine wataitumia kukufanya kichekesho, kukudhalilisha, kukufanya upoteze uwezo wa kujiamini kila siku ukiwa mbele yao.

Weka ulinzi eneo hilo piga marufuku mtu yeyote kutumia historia yako,makosa yako kama njia ya kutaka upoteze uwezo wa kujiamini mbele yake.

Mwambie mtu yeyote anayejaribu kukufanya kichekesho au kukuumiza hisia zako kwa lengo upoteze uwezo wa kujiamini mwambie "Siwezi kuona aibu mbele ya mtu yeyote kwa sababu ya historia yangu,makosa yangu au mapungufu ya muonekano kwa sababu kila mtu yupo na siri zake zenye aibu na mapungufu yake ambayo anafanya siri"

Ukifanya hivyo watu wengine wanaotaka upoteze uwezo wa kujiamini wanakosa hoja na kuondoka.

4.JIFUNZE TABIA ZA WATU
Kama hujui tabia za watu utapoteza uwezo wa kujiamini haraka lakini fuata njia hii.Watu wengi hawajiamini kabisa ila hutengeza mazingira uone wanajiamini hivyo acha kuzingatia maneno ya watu angalia VITENDO vyao.

VITENDO huongea zaidi kuliko maneno.Sehemu kubwa ya watu wasiojiamini hawawezi kukupa uhuru wa kufanya maamuzi wewe mwenyewe badala yake wanataka ufuate vile wanasema tu.

Mtu asiejiamini anataka uamini maneno yake kwa nguvu bila kuhoji chochote.Hivyo kuwa mwepesi wa kuhoji sio kufuata mkumbo

5.JIFUNZE KUKABILIANA NA NYAKATI NGUMU
Nyakati ngumu zitakuja katika maisha yako bila kujali utakuwa mchamungu au mshirikina, mwema sana au muovu, mchoyo au mkarimu, muaminifu au msaliti, matatizo hayatazami malengo yako, matatizo hayatazami kama wewe unasaidia sana watu au huna huruma kabisa, matatizo hayatazami kama ni mlemavu au upo na viungo kamili, matatizo hayatazami kama upo na watu wa kukusaidia au huna kabisa.

Kwa sababu matatizo yatakuja jiandae kukabiliana nayo eneo hilo ndio uwezo wa kujiamini unajenga haraka.

6.JIFUNZE KUPATA UTULIVU WA AKILI
Watu waliokuzunguka watakujaribu kama unajiamini kweli au Lah,wapo watakugeuka, watakusaliti, watavunja ahadi, watavunja uaminifu, wataongea uongo, watafanya makosa mengi sana,wapo watasambaza uongo na uzushi,wapo watasambaza umbea n.k lakini wote hawana nguvu yoyote ya kukuzuia kujiamini kama utapata utulivu wa akili ukiwa nao.

Kuna watu watakushambulia kwa maneno makali sana mitandaoni au mtaani au ofisini,wapo watashusha thamani kazi zako,wapo watakujibu kwa mkato,wapo wataonyesha sura zenye hasira ukiwa nao lakini wote hawana uwezo wa kukuzuia kujiamini ukiwa nao kama utapata utulivu wa akili.

Tatizo lolote lile utakumbana nalo ukiwa na utulivu wa akili ufumbuzi wake unapata.
Amehlo
 
Tangu nianze kutumia bange,
Basi hakuna nacho ogopa, najiamini sana tena sana, naweza hata kujaribu kutembea juu ya maji kama nabii fulani katika historia ya vitabu vitakatifu.


🍁........... kush master..........🍁
 
Back
Top Bottom