Elly official
JF-Expert Member
- Sep 16, 2018
- 727
- 976
Heshima kubwa sana kwenye wana JF, najua nitashambuliwa na baadhi yenu humu. Ila ukweli utabaki kuwa kweli, na uongo utajitenge na ukweli.
Nimetafakari sana juu ya hali ya kisiasa inavyoenda kwa sasa nchini mwetu. Nikiri kuwa almost tawala zote za nchi hii nimeziishi japo ya nyerere na mwinyi kidogo nlikuwa sijajitambua hasa ya nyerere. Ila nlikuwa naona maisha yalivyokua.
Nyerere alipambana kutokomeza maadui 3 ambao ni njaa, maradhi na ujinga na bahati mbaya sana hadi anaondoka hakumtoa adui hata mmoja.
Kipindi cha mwinyi yeye sikumbuki alikuja na kauli mbinu ipi, ila nakumbuka tu watu walikula bata sana pesa ilikuwa njenje, mkapa pia sikumbuki, japo ninachokumbuka ni kilimo kwanza na alibana sana pesa ila akaiacha kwa wachahce watumbue wanavyoweza.
Kwa Kikwete nlikuwa najitambua na ndo nlianza kupiga kura hivo nlikuwa na akili timamu. Ari mpya nguvu mpya na kasi ya ajabu mzee huyu aliachia watu watumbue walivyoweza.
Nikaja kipindi cha jiwe
Babangu huyu aliileta Tanzania niliyokuwa naiota toka miaka ya 2005 nikiwa chuoni, nikiri uongozi wake ndo niliutamani toka miaka hiyo mambobyote aliyoyafanya niliyataman yafanyike tokea miaka ya 2005.
Magufuli alikuja kumfukuza adui mmoja naye ni ujinga na maradhi na njaa kwa sababu alitamani sana tuwe na fikira ya kujitegemea. Umaskini wote huu ni kwa vile tumeshindwa kujitegemea tunawaza tu kuwa kuna watu huko wanaweza kuacha nchi zao kuja kutuletea maendeleo hapa kwetu.
La hasha. Magufuli alihakikisha huduma za afya zinaimarika, alihimiza kila mtanzania mwenye aridhi ya kulima ajilimie chakula chake, aliondoa kodi kandamizi kwenye mazao na uliruhusiwa kusafirisha bure hadi tani moja ya mazao popote pale.
Alikuwa ni kiongozi ukimwangalia alikuwa na nia ya dhati kabisa kulikomboa taifa hili kifikra, na kiuchumi.
Bahari mbaya ngombe wa maskini hazai na akizaa. Watu wabaya wakatupa majonzi na leo huyu shujaa wetu, kipenzi chetu, baba wa taifa hili hatunaye tenaMungu ampe mapumbziko mema huko aliko.