Kwakuwa kizazi chetu kimeshindwa... Tuwekeze katika kizazi kijacho!

Kuna ukweli kwamba Waafrika au African Diospora hawafanyi vizuri katika kustawisha uchumi katika mataifa waliopo Na wakifanya vizuri ni mara chache ukilinganisha na watu wengine.Lakini background ya mtu mweusi yawezekana imechangia kutofanya vizuri kutokana na matatizo ya muda mrefu yaliokumba vizazi hadi vizazi zaidi ya karne 5.Hii imedumaza fikra na kumjengea hofu,hivyo kupungukiwa na umakini ,wepesi wa kuamua na kutenda kwa kujiamini.
Tukija upande wetu wa Tanzania.Si tofauti sana na nchi za kiafrika katika ustawishaji wa jamii na uchumi.
Maamuzi ya mtu mmoja mmoja hayana tofauti sana na maamuzi ya serikali,kwani serikali inaponunua ndege ya raisi,au waziri kusafiri business class,au kutumia mabilioni ya maela kwenye campaign ya ubunge Igunga na ikaacha wanafuzi wanakaa chini,zahanati hazina hata bandage,ina tofauti gani tunapofanya harusi ya kifahari kwa kuchangishana wenyewe kwa sherehe ya siku mmoja,lakini hatuchangii watoto kwenda kusoma elimu bora kwenye shule bora ?
Hatuna haja ya kuongeza maazimio mengi bila kutekeleza yalio ndani ya maazimio,inaonekana makongamano mengi yanayofanyika nchini hayaboreshi makusudio ya kongamano bali yamegeuka matumizi mabovu ya hazina.
Kujitambua kwawezekana lakini kutenda ndio kitendawili.
 
Nimeipenda makala yako sana mana inatufanya tutafakari kwa kina kule tunakotaka kwenda, Kama kichwa chahabari kinavyojieleza yakuwa tumeshindwa tunahitaji kuwekeza katika kizazi kijacho hilo nilamsingi sana. Wenzetu waitaliano katika mji wa Reggio Emilia mara baada ya vita ya pili ya dunia walikaa chini nakutafakari kizazi chao klivyoa adhilika na vita, watu kukosa utu, udhalimu na ukiukwaji mkubwa wa haki zabinadamu, waliamua kuanza kufukiria namna yakutengeneza kizazi kijacho ambacho hakitavumilia ukiukwaji wa haki zabinadamu namambo yote yanayoenenda kinyume nataratibu, leo hii Reggio Emilia ni moja kati ya maeneo muhimu duniani ambapo watu wote duniani wanakwenda kujifunza jinsi yakutengeneza kizazi chawatu makini kupitia pre-school zao.

Leo hii tuje katika jamii yetu yakitanzania tunayosafari ndefu sana yakujifunza juu yakuwekeza katika kizazi kijacho. Swala hili ni gumu kwasababu kimsingi viongozi wetu wanafikiria mambo ambayo yanatekelezeka kwa haraka ili wapate umaarufu nawaendelee kubaki madarakani. Hakuna anaefikiria kuwekeza katika elimu ya pre-school kama msingi wakizazi ambao utakataa aina zote zaufisadi, viongozi wasiotaka kuwajibika baada yakufanya vibaya ktk majukumu yao.
Njia ambayo inaweza kutusaidia nikuwaambia ukweli viongozi wetu dhidi yataifa lakesho na namna yakuenenda pasipo kuadhiri taifa. Kama ulivyomalizia mti mmoja hautengenez msiti , ila msitu ulianza na mti mmoja natumai wajukuu zetu watafika mahali watasema hapana, kikubwa tuwafundishe iliyo kweli ili kweli iwaweke huru,
 
Tatizo hapa ni kwamba watoto wetu tunawaandaaje?

Human being is product of himself " baba uozo, mama uozo!!" mtoto ataponaje?
 
mi nafikiri kila mzazi a take responsibility kuanzia kwenye family level. We do not need Viongozi ambao nao ni product of malezi mabaya atuletee mabadiliko. Kwa mfano, baba anasimamishwa na trafic police kwa kosa la barabarani, anaamuo kutoa hongo mbele ya watoto wake. hapo watoto tunawafundisha nini? Tupunguze malalamishi na tuanze na sisi wenyewe. tusitegemee hawa viongozi wetu wa sasa are capable of making any changes in this country.

nawasilisha
 
Watanzania wengi hatuendelei kwa mengi...mfano wa hii topic watu wanaanza kumdiscuss Miriam instead of finding a solution ya hiyo nyumba. Huyu binti hana kosa na mtu I know her personlly she is one in a million kuwa mbovu au mzima au chochote kinachomuhusu yeye is none of our business. Let's talk on the issue presented here and not a person mentioned otherwise tutakuwa tunatwanga maji kwenye kinu. Tubadilike
 
ndugu mtulutumbi umeandika sana. Uliyoandika yanafahamika. Ukishajua tatizo unachukua hatua gani? Binafsi umechukua hatua gani kuona haya yanarekebishika? Huu si wakati wa kuorodhesha tena matatizo ya waafrika. Yanajulikana na yamejaa. Pamoja na kujua matatizo na kutafuta suluhu zake, kuna haja ya kupima pia vinasaba kuona ni kwa nini mwafrika popote alipo haendelei.

Watu weusi hawako Afrika pekee. Wapo Amerika na kwingineko. Kwa nini kila alipo mtu mweusi pana dhiki? Suala la ubaguzi kutotiliwa maanani ni suala ambalo kwa sasa halipewi uzito. Hakuna taifa la mfano la mtu mweusi ambalo limepiga hatua kiasi cha kumshangaza mtu mweupe. Wote walewale. Hii ni zaidi ya kujituma, ni zaidi ya persistance, ni zaidi ya creative thinking. Something to do with genes.

Mwafrika ni kama mwezi. Anasharabu mwanga wa jua ilhali hana mwanga wake. Jua lisipokuwepo hakuna mwanga kwenye mwezi. Wazungu wanatusukuma kufanya mambo pale wanapokuwa kati yetu. Wasipokuwepo mambo yanadorora na kuharibika. Kuna mifano mingi kuthibitisha haya. Maeneo mengi walipokuwa wazungu na wengine weupe yalistawi. Walipotuachia tukaharibu. Kwa kuwa wanajua we are half beings they treat us like half beings. The only way to prove them wrong is to equal with them and stop being moons
 
Mradi mkubwa utakaowatoa waafrika katika matatizo yao ni mradi utakao wabadili fikra. Mfano wakati nchi nyingine mtu asipolipa kodi anapata mfadhaiko, kwetu sisi mtu anakwepa kodi kwa bidii zote. Hali hii ya kufadhaika usipolipa kodi ni fikra zilizojengeka muda mrefu sana na ndiyo maana nilisema iimani, Kizazi chetu chahitaji ubatizo! Kuna kitabu cha jamaa mmoja kiko wavuti.com 'Sindano Inayovuja' Kina Mbinu nyingi sana nzuri
 
Wapo waafrika wanaojua na wasiojua matatizo yaliotufikisha hapa lakini kwa nafasi zao tofauti waweza kukuta wote tunatenda ovyo ovyo,yaani aionekani tofauti kati ya mjuaji na mjinga.
Sitaki kuamini kuwa ni laana la hasha,Ipo siri imejificha inatakiwa kuifichua tumekuwa kama mbwa akiona chatu ana bweka huku akifuatia chatu,kwanini?
 
Tulipofika Sblanders hatuwezi kuleta mabadiliko sisi, tunahitaji kuwekeza katika kizazi kijacho na kwa kuanzia tulihitahi elimu ya uzalendo kuanzia chekechea ,kutengeneza mifumo bora ya kielimu ili tuzalishe watu wawajibikaji na si walalamikaji tu, tuzalishe walipa kodi si wakwepa kodi, tuzalishe wachukia rushwa si wapenda rushwa...
 
Kinachosikitisha zaidi ni ongezeko wingu kubwa la watu wazima wasiojua kusoma na kuandika,ingawa huku nyuma miaka ya 60/70 Kisomo cha ngumbalu( Elimu ya watu wazima) kilipunguza kwa kiwango kikubwa cha wasiojua kusoma na kuandika hii ilitupatia heshima kimataifa.Maana yake ni kuwa hatuna tabia au desturi ya kuendeleza kitu kizuri,lakini tuna tabia ya kuharibu hata vile vizuri vichache tulivyokuwa tunajivunia.Kama haitoshi zimefunguliwa shule nyingi za kata kwa nguvu ya serikali na wananchi,lakini sote tunajua hali halisi ya elimu ilivyo katika shule hizo. Kuwekeza katika kizazi kijacho it must be a continuation process kutokea sisi.
 
Kuna ukweli kwamba Waafrika au African Diospora hawafanyi vizuri katika kustawisha uchumi katika mataifa waliopo Na wakifanya vizuri ni mara chache ukilinganisha na watu wengine.Lakini background ya mtu mweusi yawezekana imechangia kutofanya vizuri kutokana na matatizo ya muda mrefu yaliokumba vizazi hadi vizazi zaidi ya karne 5.Hii imedumaza fikra na kumjengea hofu,hivyo kupungukiwa na umakini ,wepesi wa kuamua na kutenda kwa kujiamini.
Tukija upande wetu wa Tanzania.Si tofauti sana na nchi za kiafrika katika ustawishaji wa jamii na uchumi.
Maamuzi ya mtu mmoja mmoja hayana tofauti sana na maamuzi ya serikali,kwani serikali inaponunua ndege ya raisi,au waziri kusafiri business class,au kutumia mabilioni ya maela kwenye campaign ya ubunge Igunga na ikaacha wanafuzi wanakaa chini,zahanati hazina hata bandage,ina tofauti gani tunapofanya harusi ya kifahari kwa kuchangishana wenyewe kwa sherehe ya siku mmoja,lakini hatuchangii watoto kwenda kusoma elimu bora kwenye shule bora ?
Hatuna haja ya kuongeza maazimio mengi bila kutekeleza yalio ndani ya maazimio,inaonekana makongamano mengi yanayofanyika nchini hayaboreshi makusudio ya kongamano bali yamegeuka matumizi mabovu ya hazina.
Kujitambua kwawezekana lakini kutenda ndio kitendawili.

Point, tena ni point of our time
 
Tulipofika Sblanders hatuwezi kuleta mabadiliko sisi, tunahitaji kuwekeza katika kizazi kijacho na kwa kuanzia tulihitahi elimu ya uzalendo kuanzia chekechea ,kutengeneza mifumo bora ya kielimu ili tuzalishe watu wawajibikaji na si walalamikaji tu, tuzalishe walipa kodi si wakwepa kodi, tuzalishe wachukia rushwa si wapenda rushwa...

Point number two.
Kwenye Biblia, ambacho ndio kitabu kilichowawezesha wazungu kuwa hapo walipo, kwa sababu they were promised blessings too,
pameandikwa kwamba, mzazi mwenye akili ni yule anayetafuta kwa ajili ya mjukuu wake.
 
Umewahi kujiuliza kwa nini nchi za Ulaya zinaendelea kutajirika kila kukicha huku za kwetu zikiendelea Kumasikinika? Umewahi kujiuliza kwa nini wakati Life Expectancy kwao Ikiongezeka kwetu ndiyo inapungua zaidi? Umewahi kujiuliza kwa nini idadi ya watu kwao inapungua wakati kwetu ndo kwanza tunazaliana? Umewahi kujiuliza kwa nini 'vijiji' vyao vinakua kwa kasi wakati vya kwetu ndo Vinachakaa?

Kwa miaka mingi sana nimekuwa na fikra tofauti na wengine kuhusu umasikini na hali duni ya afya katika nchi zetu za bara la tatu. Japo hadi sasa bado ni mwanafunzi wa Human mind lakini maarifa ambayo nimejikusanyia hadi sasa yananitosha kuandika makala hii.
Mkuu mimi nekuosma na nitatofautiana na wewe sehemu kadhaa kwa sababu mimi natazama WAPI TULIPO na tutaweza vipi kusonga mbele kutoka hapa tulipo na sii kuwatazama ambao tayari wameisha fika wakutakako..It's very logic, kabisa kwamba nyenzo zetu ni tofauti kabisa..Kwa mtu aliyetumbukia ktk shimo au amekwamba ktk tope huwezi kumpa koleo ajiomboe kwa sababu ndio nyenzo inayozunngumziwa sana na Nchi tajiri..

Msemo wangu siku zote - WATU na MAZINGIRA waliyopo siku zote ndio huzaa creative thinking ktk maamuzi magumu na kuweka mikakati na maazimio. Leo hii Tanzania tuna furnish mahitaji yetu kimaendeleo zaidi ya kuondokana ktk umaskini maana tumeshaukubali kuwa ni sehemu ya maisha yetu... Look around you!

Tumeleta Umeme na hata huo mradi wa MCHUCHUMA kwa sababu wananchi hawana umeme, umeletewa Richmond kwa usanii kwa sababu ya upungufu wa umeme ktk jiji la Dar kwa kutazama mahitaji na Mtanzania na sio mahitaji ya uzalishaji. Tumejenga misingi yote ya kiuchumi kukidhi wahitaji yetu badala ya kukidhi masoko ya nje kuuza. Tupo sawa kabisa na mkulima kijijini anayelima mazao ya chakula kwa jili ya familia na sii kwa ajili ya biashara na miaka yote amekuwa akitumikia tumbo lake la umaskini maskini na akaridhika. We have gone nowhere!.. Huu ndio mtazama wa Watanzania kwa ujumla na hauwezi kufanisiwa kwa kufikiria ama kutazam matumbo yetu..

Hakuna linalotendeka nchini kuwa ni la bahati mbaya hakuna.. Reli ya kati imekufa kwa sababu hatutarajii kuongeza export na sii ajabu we export almost nothing kupitia reli so why bother. watu wanataka kuona ATC ikifa kwa sababu we don't think of export bali usafiri wa kwenda Mwanza, Kigoma na Mbeya! Tutaweza vipi kupata maendeleo ikiwa fikra zetu wenyewe ni kuboresha maisha ya wananchi - maneno ya rais wetu JK - MAISHA BORA KWA KILA MWANANCHI hayatanguliwi na kuboresha sera za uzalishaji kwa kutazam soko la nje kwa bidhaa zetu. Kila kiongozi anatazama uchumi wetu kisiasa zaidi ktk kuridhisha Watanzania badala ya kujenga sera bora za uzalishaji, kulinda na kujenga faida ambazo ndizo zitakazoboresha maisha ya wananchi wake. The more investment for export the more we create jobs.. while unalinda viwanda vya ndani kukidhi mahitaji ya ndani, ndio maana siku hizo small industries zinapata unamaarufu kwa sababu hawa wanatazama nyanja zote za mahitaji ya ndani na sio maswala makubwa ya exports..

China leo hii duniani ni mteja mkubwa wa oil and coal ktk imports zake. China's hunger for resources is unsustainable yaani toka chakula steel hadi mchanga nikubwa sana. Haya sisi ndio kwanza tumekwenda wakabidhi Coal wao kwa kutaka watuletee umeme ambao hatujui watawauzia bei gani Tanesco. Kesho Tanesco wakisema umeme umepanda tunaanza kulalamika while we had a chance ya kuuza Coal China sisi wenyewe na tukatengeneza faida yetu wenyewe tukazalisha umeme na kadhalika.. lakini ndio kwanza tumeenda wakabidhi wao shamba na duka la kujiuzia mali yetu kwa ahadi ya Umeme kukidhi tu mahitaji yetu.Yaani tunakula toka dukani ile biashara ya Washihiri - Kumradhini mtanisamehe!

Hivyo, sio kweli kwamba we lack creative thinking bali hatujui tulipokwama, tulikwama vipi na tutaweza vipi kujikwamua na ndio maana wazungu na IMF wametutupia koleo la kuzidi kujichimbia tukiwa ndani shimoni. We have run out of ideas kwa sababu tumeridhika na kuwepo shimoni tukisaidia kutupiwa misaada ya chakula na maji while THEY figure out for us solutions ya kutuondoa ktk Umaskini..Hatuna sababu kabisa kwa nini reli ya kati na juu imekufa, kwanini bandari za Tanga na Mtwara zimekufa, kwa nini ATC imekufa, Shirikka la meli limekufa..yaani vitu vyote muhimu kwa boost export vinakufa na ndio kwanza tunasherekea kufa kwake..

Binafsi naamini kabisa tunaweza fanya mabadiliko makubwa ya kiuchumi ikiwa tutaweka misingi bora ya kuzalisha uchumi wetu kwa kutazama soko nje. wengine mnaita Tiger economy lakini ukweli siku zote unabakia kwamba unapouza zaidi ya mahitaji yako ndipo unapoboresha faida na maisha yako kwa ujumla. Huwezi kutafuta mtaji ili ujenge nyumba bali nyumba ni matokeo na matunda ya kazi uloifanya. Hao Japan na nchi zote zilizoendelea kwa kila wanachokifanya leo ni kutazama watauza wapi mali zao..

Hii ndio asili ya Ubepari - freee market economy ni kuwezeshwa sisi kuzalisha mali na tukaziuza nje kulingana na soko lililopo nje na sii kutazama mahitaji yetu sisi kuwa kigezo cha maendeleo..Hizi ni fikra za Kikomunist, fikra za woga na kujilinda dhidi ya kukoloniwa wakati umekwama na kuwa mhitaji zaidi ulipokwama badala ya kufikiria mbinu za kujikwamua..

Huwezi kuzugumzia medical Aid na Insurance kwa watu maskini ambao pato lao kwa siku ni dollar 1. Na huwezi kuzungumzia kukuza Elimu kwa kutoza karo jamii ambayo asilimia 80 hawana uwezo. WE LACK CREATIVE THINKING kwa sababu, we copy and paste mambo mengi sana kutoka Ulaya na ndio maana tumefikia kuchukua lugha ya Kiingereza kama njia ya kufundishia Elimu... hatuna sababu yoyote ya msingi zaidi ya ku copy and paste.. Hivyo, vijana wetu hawaoni umuhimu wa elimu ikiwa swala ni kujifunza lugha ambayo wataijua huko mitaani na Madisco ndiko lugha inapojengwa kwa nini aende darasani?..

Sasa muulize Mtanzania wa kawaida maana ya CEO au hata tafsiri yake - Vijana wengi sana hawajui Kiswahili chake, lakini waulize maana na PEDEGEE watakambia ni President Director General... wow haya ndio cheo gani hicho? - aaah sii unamuona Papa Msovu - huyo ndio Pedegee bana. Kwa hiyo tunajifunza yasiyotakiwa kujifunza. Ya japan yaacheni Japan, tujitazame sisi tumekwama wapi na tunatakiwa kujikwamua vipi ktk mazingira haya.
 
Hapana, hii ni kukwepa ukweli. Hakuna nchi yoyote itakayoweza kuzuia maendeleo ya nchi zetu za Afrika. Hiyo new economic order ni matokeo ya madadiliko katika sayansi na teknolojia. Umaskini wa Tanzania unatokana na sisi wenyewe, na ni makosa kutegemea kuwa nchi zingine zitatutoa kwenye umaskini. Anayeuza rasilimali ni sisi wenyewe. Kwa mfano miaka ya mwanzo ya 1980 kulikuwa hakuna nguo za mitumba, ilikuwa kama unataka nguo au ununue mpya dukani au ushoneshe, jambo ambalo lilikuwa na gharama zake. Lakini pamba tunayoizalisha ndiyo tulikuwa tunaitumia, mitumba ilipoingia, nguo zikawa za bei ya chini, pamba ikakosa soko la ndani, ikabaki inategemea tuuze nje, halafu zikikasha valiwa na wazungu zikachakaa kidogo ndio tuzinunue kwabei ndogo. Hapo nani anamakosa? Nchi tajiri? Kwa upande mwingine watati huo ilikuwa kawaida kuina watoto vijijini wamevaa nguo zilizochanika, makalio yakiwa wazi.
Kuna mambo mengi ambayo tunaweza kuyafanya ili kujenga uchimu wetu, kabla ya mwaka 1995 Tanzania ilikuwa na laini za simu 120,000 labda nusu zikiwa za taasisi na serikali, leo hii kuna laini 16,000,000. Hiyo imepanua biashara ya huduma. Kama wananchi watakuwa ni wadau wa kwanza wa kutumia malighafi zinazozalishwa ndani ya nchi na uchumi ni lazima ukue. Vitu kama bidhaa za ngozi, pamba, dawa za binadamu /mifugo, umeme wa kutokana na makaa ya mawe, biodiesel nk ndivyo vitakavyo jenga uchumi wa ndani (domestic economy). Kiwanda cha Machine Tools kingeweza kugeuza cha kutengeneza spea za magari kwa ruhusa kutoka kwa huyo "toyota" uliyemtaja na wengine, pia kingeweza kutengeneza cherehani, baiskeli, piki piki, magenereta, pampu za maji nk
Makaa ya mawe ya mchumuma, ngaka, lumecha na ruhuhu (tani 1,200,000,000) zingeweza kuzalisha umeme, kutengeneza kemikali za kuzalisha bidhaa zingine (chemical feed stocks) kama mbolea, dawa za binadamu, mpira, plastiki nk. Yote haya yangeweza kufanyika katika miaka 50 iliyopita, mengi ujuzi wa kuyatekeleza tulikuwa nao, na kama Tanzania ilipokea zaidi ya 50% ya misaada yote iliyopewa nchi 25 maskini duniani kati ya mwaka 1970 na 1980 basi hata mtaji ulukuwepo. Hatuna wa kumlaumu ni sisi wenyewe. Mfano wa Saddam na Mugabe ni potofu, Saddam alivamia Kuwait bila sababu, Mugabe alikuwa na nafasi ya kutaifisha mashamba tangu mwaka 1980, kwa awamu. Yeye alitumia ardhi kama silaa na wakamgeuka nayo. Kwa taafira tu, ardhi iliyotaifishwa nyingi waligaiwa vigogo wa ZANU-PF.
 
NDC (National Development Cor-operation) inapumua bado au imekufa,kwani huko nyuma ndio ikishughulikia miradi mikubwa ya Makaa ya mawe na chuma.
 
Back
Top Bottom