Mitch McDeere
JF-Expert Member
- Feb 24, 2017
- 299
- 619
USAJILI, UTAJIRI, UMAHIRI
Kuanzia sasa ninafanya usajili,
Kuanzia sasa ninajisajili,
Najiunga kwenye chama cha utajiri.
Kwanza nitaboresha uwezo wangu wa akili,
Kila jambo nitafanya kwa kufikiri,
Na kwenye kazi yangu nitaongeza umahiri.
Kwa nini nimeanza na akili?
Kwa sababu nilimsikia tajiri Bill,
Kuwa utajiri huanza na mindset, yaani namna unavyofikiri.
Pili nitaongeza ujasiri,
Changamoto zote nitazikabili,
Na mikikimikiki ya utafutaji nitaihimili.
Tatu, nitaongeza "kidoogo" ubahili,
Ila ninaapa sitakuwa na ukatili,
Nitatafuta bila utu wangu kujiathiri.
Nne, nitakuwa na bajeti za bili,
Za mapato, maokoto na maduhuli,
Vyote nitaviandika na nitavikariri.
Tano, nitafanya kazi kwa bidii kamili,
Vyanzo vyangu vya mapato nitaviongeza kwa utitiri,
Nitapambana huku na huko hata ikibidi kusafiri.
Mwisho, wanasema utajiri una siri,
Hivyo, nitaendelea kujifunza siri za utajiri,
Bila kuathiri yangu dhamiri.
Karibu Tajiri.
By Mitch McDeere