Kwa wanaopinga Mkataba wa DP World vijiweni ila kwenye media wanasifia na kumsifia kwa kufuru Rais

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
57,130
110,528
Tunakoelekea sasa Mheshimiwa Rais Samia tutakutajia Watendaji wako (hasa Mawaziri, Wabunge, Wakuu wa Mikoa na Wilaya) wenye Unafiki mkubwa ambao GENTAMYCINE huwa napata Taarifa zao kupitia kukutana nao baadhi, Wanafamilia Wao, Ndugu zao, Madereva, Wasaidizi Ofisini na Walinzi wao na hata Mahawara zao ambao Off Mic wanakupinga na wanakuponda sana juu ya Sakata zima la Uwekezaji wa DP World na hata Uongozi wako, ila wakiwekewa tu Mic na Watu wa Media wanaliunga mkono na Kukusifia utadhani Wewe ni Malaika wakati kumbe ni Mwanadamu kama Sisi Wengine.

Mnaendekeza tu Njaa na si Uhalisia.
 
Generalization...

Vijiwe gani ?!!!

Ikiwa wa kahawa nami nasema si kweli....

Baada ya kupata fedha yangu ya kuuzwa jumba katikati ya mji nimeamua kutofanya kazi za nguvu nikiwa kijana na kuamua kushinda vijiwe vya kahawa vya mji huu.....kwa siku ninakunywa kahawa vijiwe 15 vya maeneo tofauti hapa Dar es salaam....ninachokisikia ni wengi kuunga mkono mkataba huu wa DP WORLD.....

Usiku huwa nakuwa Bar za mjini...siyasikii hayo USEMAYO....

Punguza uongo kidogo.....

Vipi jamaa yako uliyesoma naye SAUT...mkurya B......o hajambo ?!!!
Mawaziri, Wabunge, Wakuu wa Mikoa na Wilaya hawa huwa unakutana nao kwenye hivyo vijiwe 15 vya kahawa na kashata na vi glocery/vi pub kama unavyoita bar za mjini.
 
Hii inatokana na mfumo tulionao wa kupata hao watu uliowataja ie mchawi wetu katika mapambano ya unafiki, kujipendekeza na rushwa ni mfumo wa uteuzi, kuna nafasi mtu anateuliwa unashangaa kumbe ni upendeleo(rushwa) kwaiyo mtu Kama huyu lazima ajipendekeze au awe mnafiki lakini tungekua na mfumo mwingine labda meritocracy system yaani sio unateuliwa au unachaguliwa kienyeji ila tunaangalia faida tutakazopata kutokana na uwezo, taaluma au uzoefu kwaiyo hata kuwajibisha utawajibika kutokana na hayo hata kumshauri Raisi utashauri kwa weledi bila woga ila see sio Kama ilivyo sasa
 
Kwa
Kwanini watu wa vijijini mnapenda kutumia maneno ya kizamani hivyo?

" Mahawara" ndio nini?

Mara ya mwisho kusikia mtu akitumia neno " mahawara" ilikuwa mwaka 1994.
Kwa hiyo mkuu atumie tem gani, mchepuko au nyumba ndogo?

Maana yote hayo yanawakilisha neno moja.
 
Kwanini watu wa vijijini mnapenda kutumia maneno ya kizamani hivyo?

" Mahawara" ndio nini?

Mara ya mwisho kusikia mtu akitumia neno " mahawara" ilikuwa mwaka 1994.
Hiv wew 'Gasho' wa jelajela haunaga Kaz nyngne Zaid ya kumfuatilia Genta! unajishusha thaman sana ..tumekuchoka Pang'ang'a wew!! kila muda shobo kwake...utapgwa mkia Gasho weeh!
 
Attachment
 

Attachments

  • 1692735077857.jpg
    1692735077857.jpg
    31.5 KB · Views: 1
Back
Top Bottom