Kwa waliosoma Kigonsera Ruvuma

Napenda kukumbushana na wana jf kwa wale walopita kigonsera nini unacho kimisi walimu gani unao wakumbukaa Nikianza na mm nilikua pale 1991/1994 Twiga house. Nammiss sana Papalika Mlasu Mbonde

Nilisoma pale 1963-1966. Namkumbuka sana Father Gotard, mwalimu Mahai, mwanafunzi mwenzangu kalubandike. Tulikuwa tunaiba sana mihogo ya bruda Lukundus.
 
Ilikua ukisikia anauaaaa..ni mwendo wa speed mabwenini.nakumbuka mshkaji wangu mmoja alikua nyerere,Balugu akaja dorm,jamaa alikua bwenini akakimbilia chooni.Ticha akamfuata kulekule,wakaenda dorm jamaa akavaa nguo wakaongozana mpaka ofisini,walipofika mlango wa ofisi akamwambia jamaa amsubiri ampe karatasi ya kuandika maelezo,ile kuingia ofisini tu jamaa nduki,alipotoka ofisini ilibidi aanza kucheka tu.ilikua ni burudani sana Camp la Kygo....
 
R.I.P Mlasu! Vipi Balugu na Naneka umewasahau!
dah, mimi nilikuwa wa simba dom. mlasu nilikuwa sijui kama kafa. rip. balugu nakumbuka mwaka 2001 alipigwa na form six mmoja hivi aliyekuwa mcheza karate, alipigiwa pale juu walipokuwa wanauza vimbolo a.k.a vidole, vile vidude vya kutafunia (wanaita hivyo). shelimo alikuka kuhamia hapo pugu, siku hizi sijui ameenda wapi. sitasahau kitimoto ya halale kule chini na ndizi za kimatengo. ila kuna siku wamatengo walichoma msitu kimila shule yetu ilipona...hahahaha
 
Nakumbuka ile 1998 tunaanza advance PCB pale.,shule imefungua nilivuta kama wiki mbili hivi nikajua ntakuta watu wamesha-report to my surprise nilikuwa peke yangu! I stayed almost one week advance peke yangu! Kumbu kumbu adimu
 
mkuu kijana wa digitali, nilipita pale advance 2011/2013

Nimemiss mwalimu wangu wa chemistry mr. Mtweve
 
Mkuu mimi nilikuwa jirani yenu pale Likonde Seminary 1998-2000,nakumbuka mechi za mpira wa miguu kigonsera na likonde seminary ilikuwa si mchezo.

ilikuwa dili kwenda kaigo kuosha macho mademu wa taasisi, sema wao walikuwa wanadata na matarumbeta ya lise
 
Nilisoma pale 1963-1966. Namkumbuka sana Father Gotard, mwalimu Mahai, mwanafunzi mwenzangu kalubandike. Tulikuwa tunaiba sana mihogo ya bruda Lukundus.

Hapo kwenye red ndio kumenifanya nikuulize hili swali: MKUU BAADA YA HAPO UKAENDA WAPI NA UNA WADHIFA GANI SERIKALINI? unaweza ukanipa jibu hata kwa pm
 
Back
Top Bottom