Kwa waliopitia level ya FTC naombeni msaada wenu kielimu

MUIKOMA

Member
Nov 1, 2011
35
8
Wana bodi hamjambo?
Kwa wataalam waliopitia level hii ya FTC ninomba kujua kama mdogo wangu anaweza kupata chuo cha kuendelea na elimu juu kwani ana B moja ya mathematic, C tatu, D moja na F moja ya FTC in highway engineering kutoka D.I.T mwaka 2002. Alishindwa kusuppliment kutokana na kupitiliza muda wa miaka 3 ambayo ilikuwa maximum duration ya kusup. Naombeni ushauri wenu, nifanyaje ili aendelee na elimu zaidi. Mods nisameheni kwani najua wengi wanapita jukwaa la siasa. Mbarikiwe sana
 
Ukishakuwa na F hata moja tu, tayari unakuwa huna FTC. Hapo kusonga mbele inakuwa kagota kwakuwa hata cheti chenyewe anakuwa hajapewa.
 
Kweli hii elimu hawakuwa wanatutendea haki lakini aombe private universities anaweza pata maana kunajamaa zangu walipata. Ila kwa kifupi huyo sio fundi mchundo na pole sana maana alikuwa anakigezo kimoja cha mathematics kupata B tatizo ni hiyo F
 
cheti amepataje? ila kwa DIT naona sijui inakuwaje wanapta vyeti maana kunajamaa yangu nilimuona anacheti lakini ana F ya somo moja. kwa vyuo kama MTC (MIST) na Arusha tech. kama hujaclear hupati cheti
 
Mkuu cheti hana, ni result slip toka baraza
la mitihani
 
Kama kaamua kurudi kwenye kusaka elimu, basi afanye private candidate Form VI.Najua mpaka kwenda DIT ni kwamba alifanya vizuri paper ya F IV.Mimi ndivyo nilivyofanya na nikajoin UDSM.Asikate tamaa,bado future ipo.
 
kweli kabisa FTC ukiwa na F moja tu unaacha mchundo.ila mwambie ajiandae aende ST.JOSEPH watu kama hao wanawapokea,unasoma semester moja wanaita BRIDGE COURSE akifaulu anajoin chuo kama kawa.asikate tamaa,anaweza kwenda hata leo wakampokea ingawa kachelewa kidogo
 
Kama kaamua kurudi kwenye kusaka elimu, basi afanye private candidate Form VI.Najua mpaka kwenda DIT ni kwamba alifanya vizuri paper ya F IV.Mimi ndivyo nilivyofanya na nikajoin UDSM.Asikate tamaa,bado future ipo.

Ushauri kuntu huu. Aufanyie kazi. Hamna shortcut nyingine.
 
Wana bodi hamjambo?
Kwa wataalam waliopitia level hii ya FTC ninomba kujua kama mdogo wangu anaweza kupata chuo cha kuendelea na elimu juu kwani ana B moja ya mathematic, C tatu, D moja na F moja ya FTC in highway engineering kutoka D.I.T mwaka 2002. Alishindwa kusuppliment kutokana na kupitiliza muda wa miaka 3 ambayo ilikuwa maximum duration ya kusup. Naombeni ushauri wenu, nifanyaje ili aendelee na elimu zaidi. Mods nisameheni kwani najua wengi wanapita jukwaa la siasa. Mbarikiwe sana
Jaribu UDSM kozi kama Bussiness Administration wanakuchukua!!
 
Back
Top Bottom