Kwa wale wasiogopa majini angalieni hizi picha za majini

mkuu kuna tofatauti gani kati ya majini na viumbe toka sayar za mbali maarufu kama aliens.nimewahi ku google na kukutana na habari kuwa taifa kubwa marekani huwatumia sana hawa aliens ktk maabara zake za siri kubuni technology mbalimbali za kijeshi.je kuna tofauti yoyote ya hao viumbe?
 
1wafalme 5:13-17 linasema 13Mfalme sulemani akafanya shokoa ya Israeli wote nayo shokoa hiyo ilkuwa ya watu thelathini elfu. 14Akawatuma Lebanoni kwa mwezi elfu kumi kwa zamu. mwezi mmoja walikuwako huko lebanoni, na miezi miwili wakawako kwao. na Adoramu alikuwa juu ya shokoa. 15Sulemani alikuwa na wachukua mizigo sabini elfu, na wakatoa miti themanini elfu milimani; 16 mbali na maakida wake Sulemani waliokuwa juu ya kazi, elfu tatu na miatatu wasimamizi wa watu waliotenda kazi. 17Mfalme akaamuru nao wakaleta mawe makubwa, mawe ya thamani ili wauweke msingi wa nyumba kwa mawe yaliyochongwa 18 na waashi wa Sulemani na waashi wa Hiramu na Wagebali wakayachonga, wakaweka tayari miti na mawe ya kuijenga nyumba.
sasa nioneshe ni wapi majini wamefanya kazi kwa Sulemani, NENO la Mungu linasema amelaaniwa mtu yule anayeongeza au kupunguza NENO la Mungu, hivyo usiwaaminishe watu uhalali wa hayo mapepo kwa wakristo labda kwa hao wengine lakini kwetu hayo tunayachoma kwa damu ya YESU KRISTO MUNGU WETU na NENO LA USHUHUDA na wala kati yao hakuna jini mwema wala mbaya yote kwa ujumla ni watenda kazi wa muovu ibilisi shetani hivyo adhabu yao ni moto wa milele.
 
Siogopi huwaga...lakin leo nimeogopa haya makitu yamezidi kwa ubayaa..halafu sasahivi usiku nisije nikaota usiku Mungu niepushe Amen.
 
ha ha ha nimekukubali umechukua muda gani kusoma au kijifunza mambo haya? Je nilishawai kusikia majini yanasaidia mtu akiwa na kesi mahakamani je ni kweli?
 
usipotoshe NENO la Mungu [JEHOVA]
1wafalme 5:13-17 linasema 13Mfalme sulemani akafanya shokoa ya Israeli wote nayo shokoa hiyo ilkuwa ya watu thelathini elfu. 14Akawatuma Lebanoni kwa mwezi elfu kumi kwa zamu. mwezi mmoja walikuwako huko lebanoni, na miezi miwili wakawako kwao. na Adoramu alikuwa juu ya shokoa. 15Sulemani alikuwa na wachukua mizigo sabini elfu, na wakatoa miti themanini elfu milimani; 16 mbali na maakida wake Sulemani waliokuwa juu ya kazi, elfu tatu na miatatu wasimamizi wa watu waliotenda kazi. 17Mfalme akaamuru nao wakaleta mawe makubwa, mawe ya thamani ili wauweke msingi wa nyumba kwa mawe yaliyochongwa 18 na waashi wa Sulemani na waashi wa Hiramu na Wagebali wakayachonga, wakaweka tayari miti na mawe ya kuijenga nyumba.
sasa nioneshe ni wapi majini wamefanya kazi kwa Sulemani, NENO la Mungu linasema amelaaniwa mtu yule anayeongeza au kupunguza NENO la Mungu, hivyo usiwaaminishe watu uhalali wa hayo mapepo kwa wakristo labda kwa hao wengine lakini kwetu hayo tunayachoma kwa damu ya YESU KRISTO MUNGU WETU na NENO LA USHUHUDA na wala kati yao hakuna jini mwema wala mbaya yote kwa ujumla ni watenda kazi wa muovu ibilisi shetani hivyo adhabu yao ni moto wa milele.
hello.@hasason mimi sikujibu na hicho kitabu chako cha biblia chenye mikono ya watu mimi nitakujibu kitabu cha Waislam Quran soma hapa Sura 27:15-44

15. Na hakika tuliwapa Daudi na Sulaiman ilimu, na wakasema: Alhamdu Lillahi, Kuhimidiwa kote ni kwa Mwenyezi Mungu aliye tufadhilisha kuliko wengi katika waja wake Waumini.

16. Na Sulaiman alimrithi Daudi, na akasema: Enyi watu! Tumefunzwa usemi wa ndege, na tumepewa kila kitu. Hakika hii ni fadhila iliyo dhaahiri.

17. Na alikusanyiwa Sulaiman majeshi yake ya majini, na watu, na ndege; nayo yakapangwa kwa nidhamu.

18. Mpaka walipo fika kwenye bonde la wadudu chungu, alisema mdudu chungu mmoja: Enyi wadudu chungu! Ingieni majumbani mwenu, asikupondeni Sulaiman na majeshi yake bila ya wao kutambua

19. Basi (Sulaiman) akatabasamu akacheka kwa neno hili, na akasema: Ee Mola wangu Mlezi! Nizindue niishukuru neema yako uliyo nineemesha mimi na wazazi wangu, na nipate kutenda mema uyapendayo, na uniingize kwa rehema yako katika waja wako wema.

20. Na akawakagua ndege, na akasema: Imekuwaje, mbona simwoni Hud-hud, au amekuwa miongoni mwa walio ghibu?

21. Kwa yakini nitamuadhibu kwa adhabu kali, au nitamchinja, au aniletee hoja ya kutosha.

22. Basi (Hud-hud) akakaa si mbali na akasema: Nimegundua usilo gundua wewe, na ninakujia hivi kutoka nchi ya Sabai, na nakuletea khabari za yakini.

23. Hakika mimi nimemkuta mwanamke anawatawala, naye amepewa kila kitu, na anacho kiti cha enzi kikubwa

24. Nimemkuta yeye na watu wake wanalisujudia jua badala ya Mwenyezi Mungu; na Shet'ani amewapambia vitendo vyao na akawazuilia Njia. Kwa hivyo hawakuongoka,

25. Na hawamsujudii Mwenyezi Mungu ambaye huyatoa yaliyo fichikana katika mbingu na ardhi, na anayajua mnayo yaficha na mnayo yatangaza.

26. Mwenyezi Mungu - hapana mungu ila Yeye, Mola Mlezi wa A'rshi tukufu..

27. Akasema (Sulaiman): Tutatazama umesema kweli au wewe ni miongoni mwa waongo.

28. Nenda na barua yangu hii na uwafikishie, kisha waache na utazame watarejesha nini.

29. (Malkia) akasema: Enyi wahishimiwa! Hakika nimeletewa barua tukufu.

30. Imetoka kwa Sulaiman nayo ni: Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

31. Msinifanyie jeuri, na fikeni kwangu nanyi mmekwisha kuwa wenye kusalimu amri.

32. Akasema: Enyi wahishimiwa! Nipeni shauri katika jambo langu hili, kwani mimi sikati shauri yoyote mpaka mhudhurie.

33. Wakasema: Sisi ni wenye nguvu na wakali kwa vita; na amri iko kwako, basi tazama ni nini unaamrisha.

34. Akasema: Hakika wafalme wanapo uingia mji wanauharibu, na wanawafanya wale watukufu wake kuwa wanyonge. Na hivyo ndivyo watendavyo.

35. Lakini mimi nitawapelekea zawadi, nami nitangoja watakayo rudi nayo wajumbe.

36. Basi alipo fika (mjumbe) kwa Sulaiman, alisema (Sulaiman): Hivyo ndio nyinyi mnanisaidia kwa mali? Aliyo nipa Mwenyezi Mungu ni bora zaidi kuliko aliyo kupeni nyinyi. Lakini nyinyi mnafurahia hii zawadi yenu.

37. Rejea kwao! Kwa yakini sisi tutawajia kwa majeshi wasio yaweza kuyakabili. Na hakika tutawatoa humo na hali wao wamekuwa madhalili na wanyonge.

38. Akasema: Enyi wahishimiwa! Ni nani kati yenu atakaye niletea kiti chake cha enzi kabla hawajanijia nao wamekwisha salimu amri.

39. Akasema: Afriti, katika majini: Mimi nitakuletea kabla hujainuka pahala pako hapo. Na mimi kwa hakika nina nguvu na muaminifu.

40. Akasema mwenye ilimu ya Kitabu: Mimi nitakuletea kabla ya kupepesa jicho lako. Basi alipo kiona kimewekwa mbele yake, akasema: Haya ni katika fadhila zake Mola wangu Mlezi, ili anijaribu nitashukuru au nitakufuru. Na mwenye kushukuru, kwa hakika, anashukuru kwa manufaa ya nafsi yake; na anaye kufuru, kwa hakika Mola wangu Mlezi ni Mkwasi na Karimu.

41. Akasema: Mgeuzieni kiti chake cha enzi hiki, tuone ataongoka, au atakuwa miongoni mwa wasio ongoka.

42. Basi (Malkia) alipo fika akaambiwa: Je! Kiti chako cha enzi ni kama hiki? Akasema: Kama kwamba ndicho hichi. (Sulaiman na watu wake wakasema): Na sisi tumepewa ilimu kabla yake (Malkia), na tukawa Waislamu

43. Na yale aliyo kuwa akiyaabudu badala ya Mwenyezi Mungu yalimzuilia. Hakika yeye (Malkia) alikuwa katika kaumu ya makafiri

44. Akaambiwa: Liingie behewa la hili jumba. Alipo liona alidhani ni maji, na akapandisha nguo mpaka kwenye miundi yake. (Sulaiman) akasema: Hakika hilo ni behewa lilio sakafiwa kwa viyoo! Akasema (Malkia): Mola wangu Mlezi! Mimi nimejidhulumu nafsi yangu, na sasa nanyenyekea pamoja na Sulaiman kwa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote.

Haya tena nimekuletea kisa cha Nabii Suleyman na Yule Malkia wa Yemen Bilgis huyu Malkia wa Yemen

alikuwa analiabudia Jua kuwa ndio Mungu badala ya Mwenyeezi Mungu mmoja tu hana mshirika wake.

Hata kwenye kitabu chako cha Biblia kisa hiki kimetajwa angalia kwenye hiyo Biblia yako kisha uje

unipinge hapa. Huyu Nabii suleyman alikuwa na Wana jeshi Binadamu na Majini na ndege pia walikuwa wana mtumikia Huyu Nabiiwa Mungu Nabii suleyman amani ya Mungu iwe naye mpak siku ya hukumu amka Mkuu acha kupinga pinga kama hujuwi uliza utajibiwa. Wewe unachojuwa kuwa kuna Damu ya Bwana Yesu Mungu Mtu Yesu Mwana wa Mungu YESU hakuna kitu kingine mnachofundishwa nyinyi makanisani zaidi ya hayo amka wewe acha ujinga wako. Ulizeni kwa Ma-Padri Maswali ndio hakuna Maswali wala Majibu Makanisani? Misikitini kuna Maswali na Majibu Mkuu.

usipotoshe NENO la Mungu [JEHOVA]
1wafalme 5:13-17 linasema 13Mfalme sulemani akafanya shokoa ya Israeli wote nayo shokoa hiyo ilkuwa ya watu thelathini elfu. 14Akawatuma Lebanoni kwa mwezi elfu kumi kwa zamu. mwezi mmoja walikuwako huko lebanoni, na miezi miwili wakawako kwao. na Adoramu alikuwa juu ya shokoa. 15Sulemani alikuwa na wachukua mizigo sabini elfu, na wakatoa miti themanini elfu milimani; 16 mbali na maakida wake Sulemani waliokuwa juu ya kazi, elfu tatu na miatatu wasimamizi wa watu waliotenda kazi. 17Mfalme akaamuru nao wakaleta mawe makubwa, mawe ya thamani ili wauweke msingi wa nyumba kwa mawe yaliyochongwa 18 na waashi wa Sulemani na waashi wa Hiramu na Wagebali wakayachonga, wakaweka tayari miti na mawe ya kuijenga nyumba.
sasa nioneshe ni wapi majini wamefanya kazi kwa Sulemani, NENO la Mungu linasema amelaaniwa mtu yule anayeongeza au kupunguza NENO la Mungu, hivyo usiwaaminishe watu uhalali wa hayo mapepo kwa wakristo labda kwa hao wengine lakini kwetu hayo tunayachoma kwa damu ya YESU KRISTO MUNGU WETU na NENO LA USHUHUDA na wala kati yao hakuna jini mwema wala mbaya yote kwa ujumla ni watenda kazi wa muovu ibilisi shetani hivyo adhabu yao ni moto wa milele.

Sasa hii nkisoma nkimaliza ntalala kwel mkuu!!!
 
aiseee mdhee wangu nifanyie huyo wa noti aisee ili anitafutie hela ila mashariti sitaki ati ,yeye aniletee pesa kisha aende zake akaendelee kula kula mavi ya falasi ,tafadhari mwambie aje nahamu nae sana
 
Mkuu usiniguse Ukimtaka huyo Jini wa kuleta Pesa wasiliana na Maalim wangu anaye itwa Maalim Hassan namba yake ya simu hii hapa 0645017777
 
hello.@hasason mimi sikujibu na hicho kitabu chako cha biblia chenye mikono ya watu mimi nitakujibu kitabu cha Waislam Quran soma hapa Sura 27:15-44

Mr me sina tatizo na kitabu chako ila ni kosa kubwa kwa Mungu ninaemwabudu mimi kwa mujibu wa Biblia au NENO ku-corrupt NENO ambavyo siyo halali kama ulivyofanya kwa kitabu cha 1wafalme 5:13-17 ambapo nukuu uliyoiandika haipo sio tu kwenye kitabu cha WAFALME bali kwenye Biblia yote hapana ushirika wa namna yeyote kati Mungu na majini wala roho zote chafu kutoka kuzimu.
beside kiwe namikono ya watu au miguu haijalishi NENO ni nyundo ivunjayo mawe vipande vipande [ikiwa ni pamoja na hayo mapepo]na pia NENO lasema; NENO la MSALABA kwa wao wanaopotea ni upuuzi bali sisi tunaokombolewa ni Nguvu ya Mungu.
 
Upumbavu, ujinga na mawazo duni kama haya ndio kisa cha umaskini na kutokuendelea kwetu.

Kuua albino, kuamini watu kupaa na ungo, kuganga maofisini kwa kutaka vyeo au kupata kazi, kuamini limbwata zipo, na ushenzi mwingine wote unaotujia sie wabantu wenye akili fupi...

Sio siri wabongo hasa tunapenda njia fupi kwa kila jambo, barabarani, mashuleni, maofisini, n.k. sie kufanya kazi kwa bidii na kuwa wabunifu ni hakuna...ni balaa kwa kweli..!:embarassed2:
 
Back
Top Bottom