Msemaji Simba kuna Majini wazuri na wabaya Simba mnatumia yapi?

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,323
4,667
Visanga vya mpira wa Tanzania havitakaa viishe, nimemsikia msemaji wa Simba akisema kuna majini wazuri na wabaya kwa Imani yangu ni Big No majini ni roho chafu zilizoasi mbinguni na kutupwa Motoni.

Swali la kujiuliza je msemaji wa Simba anatumia majini wazuri, kama kama msemaji anaishi kwa itikadi hizo za kuamini kwenye majini wazuri na vipi je timu nzima ya Simba.

Hakika mpira wetu una safari ndefu sana kwanini tumetokea kuishi na kuamini sana kwenye uchawi? Ingekua majini/ uchawi unacheza mpira hakika kuna nchi wangebeba makombe yote makubwa tunayoyafahamu.

Hii ni shida sana kwa wachezaji wa kiafrika hawataki kuamini katika mazoezi bali kwenye ushirikina nakumbuka Emanuel Adebayor alipata kusema mama yake mzazi anamloga ili asifunge kwa maisha ya wachezaji wa kiafrika hii ni kawaida sana.

Mchezaji anashinda kidimbwi kesho na kesho kutwa vikimshinda anakimbilia kwa waganga wa kienyeji hivi wewe ukienda kwa mganga wa kienyeji hata kama ni kikohozi cha kutumia Mucolyn tu atakwambia umetupiwa jibu.

Nlitegemea msemaji wa Simba aje na kauli za kupinga huu upumbavu ili yeye anajinadi eti wamenunua kesi ya Mayele na kuna majini wazuri na wabaya.

My country people tuna safari ndefu sana ya kutoka hapa tulipo.

Ni hayo tu
 
Mchezo wa mpira hauna tofauti na wachimbaji wadogo wadogo, mara ya kwanza naanza kuchimba nilipata watenda kazi aisee Hawa majamaa bila ya kuwaletea mganga na kuajiri 'mchoma dawa' hawazami Shimoni KAMWE, utachimba mwenyewe
 
Yeye ana mtazamo wake ulioathiriwa na imani yake, wewe una mtazamo wako unaothiriwa na imani yako na Kiranga pia ana mtazamo wake! Kila mtu yupo sahihi katika Imani yake

Kubali kutokubaliana na utofauti wa kiimani,kiitikadi na kimtazamo.
 
Acha Makolo Waweweseke Maana Hawana Cha Kuzungumzia Mwaka Huu Tena.


Kila La Kheri Dar Young Africans Kwa Ushindi Mwingine Tena Wa Ligi Kuu Ya NBC 2023/2024
Bila kuwatupia majini wachezaji wa timu pinzani uto mngekuwa mnashika mkia.
Hata yale magoli matano dhidi ya simba ukitafakari kwa makini utagundua kwamba wachezaji wa simba walirushiwa majini ya kuwafanya washindwe kukimbia uwanjani.
MAJINI FC
 
Yeye ana mtazamo wa ulioathiriwa Imani yake, wewe una mtazamo umaothiriwa Imani yako na Kiranga pia ana mtazamo wake! Kila mtu yupo sahihi katika Imani yake

Kubali kutokubaliana na utofauti wa kiimani,kiitikadi na kimtazamo.
This is not even wrong, as Dr. Pauli used to say.
 
Back
Top Bottom