Kwa wale waliosoma barua ndefu kama hii naomba tujikumbushie

bakarikazinja

Senior Member
Nov 9, 2009
177
8
Mtunzi mariama ba:
Madhari:senegal
hiki ni kitabu kina cho zungumzia ukombozi wa mwanamke katika jamii siyo tu katika nchi ya senegali bali dunia nzima kwa ujumla hivyo tunaona wahusika mbalimbali kama vile wakina ramatulayi ,binetuu,maudo,modufali,daba na hata fatmata malenga mshirikina alikuwa akitumia simbi kutabili mambo ya baadaye na bila kumsahau dauda dienga haya wana jamii/wanajamvi hebu tukumbushiane visa mbalimbali vilivyojili katika riwaya hii ya barua ndefu kama hii
 
Haa haa! Ndoa za mitala zimeelezwa vzuri humu...
Jinsi Dauda Dieng alivyompenda Ramatoulaye, ingawa tajiri lakini Rama hakubabaika akamkubali mtu aliyempenda ingawa pia alimtesa sana na maisha kuwa magumu sana na watoto akitahudumia peke yake..
Ni barua nzuri na yenye mafundisho mengi..
Imeeleza vizuri utamaduni wa kiafrika, mchanganyiko na ule wa kiislam na kadhalika..
Nakumbuka kuna sehemu anazungumzia enzi za utoto ' tukila embe mbichi za ugwadu' yaani inachota hisia za ndani barua hii ndefu..
Hakika ni barua ndefu na yenye kila aina ya ubunifu na katu hutaacha kuisoma, nawahamasisha wote msiosoma kitabu (barua hii) mkitafute.
 
oh,MARIAM BA anasema,wakat una kanuni zake,znapoachwa hutenda,ingawa binadamu hulazimisha wakat,
DaUda Dieng hakuwa akimtendea haki mkewe hata KIDOGO!
 
Hata hivyo msisahau ile sehemu ambayo alimfukuza tamsiri pindi alipo kwenda kutaka kumuo lakini kwa ujasiri wake rama alikataa na kusema "mimi sikama chombo cha kupokezana mkono kwa mkono "hivyo alimtaka tamsiri asiyarejehe tena yale mazungumzo yake.
 
Mmm swahiliani je umelionaje swala la imani za ushirikina katika hii riwaya hivi nikweli wanawake wengi wa kiafrika ndivyo walivyo jamani
 
mmenikumbusha mbali sana 2001, itabidi nikisome tena michang ya hivi ni mizuri tukumbushane kwa haya na tuzidi kusoma kazi za fasihi.
 
Peck naomba ukitafute uje hapa jamvini tukijadili ni kitabu kizuri sana ambacho kina faa kwenye ujenzi wa jamii mpya
 
kwenye page ya kumi na tisa kuna sehemu inasema "kile ambacho mwanamke wa kizungu anamzidi mwanamke wa kiafrika ktk maumbile ya kimwili ni tofauti ya rangi,na nywele zale ni nyingi
 
mwanzoni kinachosha sana, na hakieleweki,
Baadae kinaeleweka vzr sana na ni kitamu sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom