ukweli unaweza pata uchizi kwa biashara hii,nilishataka kunywa sumu baada ya kuamka asubuhi na kukuta kuku 322 kati ya 500 wamekufa na takriban 40 wameparalise,na ndiyo kwanza wamefikisha wiki nne na nusu,yaani nilichanganyikiwa nikatamani afadhali hela yangu ningepigia lagha nikaongeza damu na kuweka heshima bar
Pole kuku hawa hawataki mchezo, hapa itakuwa ni chanjo ulichelewa au hukuwapa vizuri, pili ku paralise au miguu kwisha nguvu ni kukosa calcium, wiki ya 3 unatakiwa uwape mifupa ili kuwaongezea uimara kwenye miguu kwasababu wiki ya nne wanaanza kuwa na uzito mkubwa kulingana na mwili. Pia chakula unachowapa jaribu kuona wenzio wanaokitumia kuku wao wakoje, kwani chakula kisichokuwa na dagaa ya kutosha ndio huwa kinamadhara zaidi.
Vifo vingi ni kutokana na Newcastle infection, Gumboro na multiple infection kwa kukosa hewa safi kama kuku ni wengi kulingana na ukubwa wa banda., pia typhoid fevers kutokan na maji yasiyo safii au uchafu kwenye vyombo vya maji
Lakini ukifata kanuni zao, yaani huwezi kutana na hivi vifo hata kidogo