Ndugu zangu Watanzania, hii ni Nchi yetu sote. Kwa aina ya Wabunge hawa tulio nao sasa, kamwe hatutakuja kupata maendeleo ya kweli.
Ebu fikiri, Mbunge anapewa dakika 10 za kuchangia hoja Bungeni.
Kati ya dakika hizo, Mbunge anatumia zaidi ya dakika 7 kumsifu Rais. Dakika zinazobaki anaongelea miradi iliyotekelezwa.
Je, hapo kuna kitu kipya? Hakuna kabisa.
Mbunge anayejitambua na anayewawakilisha Wananchi wake kikamilifu anatarajiwa atumie huo muda wa dakika 10 kama ifuatavyo kwa mfano:-
(1) Dakika labda 5, azitumie kuelezea kwa kina shida zinazowakabili Wananchi anaowawakilisha.
(2) Dakika zinazobaki atumie kutoa mapendekezo au njia za kutatua matatizo hayo.
Kwa hiyo, kwa zaidi ya 80% ya Wabunge wetu wanamwakilisha Rais zaidi kuliko Wananchi waliowachagua.
Watanzania tuna wajibu wa kufanya mapinduzi/mabadiliko makubwa kabisa ili tuwe na Wabunge wanaowawakilisha Wananchi waliowachagua.
Nawasilisha.