Kwa siku Muhimbili inaona Wagonjwa 2000 wa nje na 1300 Wanaolazwa kati yao wote 36% ni wa Waonjwa wa msamaha

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Mohamed Janabi amesema “MNH ndio hospitali kubwa Tanzania ambapo wataalamu bingwa wa kada nyingi wanapatikana hapa ambapo kwa siku tunaona wagonjwa wa nje kati ya 1,500 hadi 2,000 na waliolazwa takribani 1,300.

“Asilimia 36 ya wagonjwa hawa ni wa msamaha, kwa hivyo msaada utasaidia hospitali kuelekeza pesa ambazo zingetumika kwenye manunuzi ya luninga kwenda kwenye mahitaji ya wagonjwa,” amesema Prof. Janabi.
9ddfd276-61b8-4a4b-9861-c9095b4aaca8.jpg

Ameyasema hayo wakati akipokea msaada kutoka Kampuni ya Bima ya Assemble Insurance (T) Ltd ambayo imetoa msaada wa luninga 10 kwa MNH ikiwa ni sehemu ya mpango wa kampuni hiyo kurejesha kwa jamii.

Amesisitiza kuwa msaada huo ni wa manufaa kwa MNH kwa kuwa pesa ambazo zingetumika kununulia luninga hizo zitaelekezwa kwenye mahitaji mengine ya wagonjwa ikiwemo ununuzi wa dawa.

Amebainisha kuwa uwepo na luninga katika mazingira ya Hospitali unasaidia kuhabarisha ndugu wanaouguza wagonjwa lakini pia ni sehemu ya tiba kwa baadhi ya wagonjwa.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Assemble, Bi. Tabia Massoud amesema kuwa kampuni yake inavutiwa kwa namna MHN inavyopiga hatua kwa kuboresha huduma.

“Muhimbili ni mshirika wetu mkubwa kwa kuwa wateja wetu wengi wanahudumiwa hapa, msaada huu utawanufaisha pia na wateja wetu ambao wananufaika na huduma za matibabu hapa,” amesema Bi. Massoud.
 
Back
Top Bottom