Kwa Sheria ya usalama barabarani hili limekaaje?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,695
6,398
Unaendesha gari kutoka point A kwenda point B.

Point B ipo hatua chache kutoka iliko point C ambako kuna kizuizi cha Polisi.

Ulipokaribia point B, ambapo utapaswa kukata kulia kwa kuwa ndiko unakoelekea hivyo hulazimiki kufika point C, na kabla hujaindicate kuwa unataka kukata kona kwenda point B, askari akakuonesha ishara ya kusimama kwa ajili ya ukaguzi.

Kwa mujibu wa Sheria, unapaswa kufanyeje?

1. Uende hadi point C ukaguliwe kwanza kisha ugeuze kwa ajili ya kwenda point B?

2. Utaonesha ishara ya kuelekea point B bila kujali kuwa askari alishakuashiria kusimama?
 
Mimi sijasoma sheria za barabarani hata kidogo mkuu! Ila kwa maelezo yako na askari wetu wa nchi hii kazi unayo!
Mimi ningesimama hapo hapo pointi B na kuwasha indicator ya kuingia pointi B, wala nisingeenda pointi C mpaka aniite
 
Lakini ujue kabla ya kuwasha indicator yeye alishakuonesha ishara ya kukusimamisha. Ukikata kona hatadai kuwa umefanya hivyo kumkwepa?
 
Ndiyo maana nimesema nitasimama hapo hapo huku nimewasha indicator ya kuingia pointi B!
Ngoja waje mkuu mimi sina chochote ninachokijua kuhusu sheria za barabarani
 
Acha uongo mkuu😃

Hujui chochote wakati unajua mpaka umuhimu wa indicator unapotaka kukata kona😀

Inawezekana hujui Sheria zote, lakini inawezekana ukawa umeniacha mbali sana kwenye uelewa wa Sheria za usalama barabarani.
 
Unaendesha gari kutoka point A kwenda point B.

Point B ipo hatua chache kutoka iliko point C ambako kuna kizuizi cha Polisi.

Ulipokaribia point B, ambapo utapaswa kukata kulia kwa kuwa ndiko unakoelekea hivyo hulazimiki kufika point C, na kabla hujaindicate kuwa unataka kukata kona kwenda point B, askari akakuonesha ishara ya kusimama kwa ajili ya ukaguzi.

Kwa mujibu wa Sheria, unapaswa kufanyeje?

1. Uende hadi point C ukaguliwe kwanza kisha ugeuze kwa ajili ya kwenda point B?

2. Utaonesha ishara ya kuelekea point B bila kujali kuwa askari alishakuashiria kusimama?
Kwakuwa ulikuwa unaenda Point B itabidi uende point B kwa hatua chache halafu tia Gari Pembeni kumsubiri atakuja..
Asipokuja Shuka kwenye Gari mfuate ujue kwaninu amekusimamisha
 
Acha uongo mkuu😃

Hujui chochote wakati unajua mpaka umuhimu wa indicator unapotaka kukata kona😀

Inawezekana hujui Sheria zote, lakini inawezekana ukawa umeniacha mbali sana kwenye uelewa wa Sheria za usalama barabarani.
Kujua umuhimu wa kuwasha indicator imetokana na mimi kuona vyombo vya moto vikiwasha indicator vinapo katiza upande fulani!

Mimi kama mtembea kwa miguu hiyo imenisaidia!

Kwakuwa imenisaidia hata mimi nitakuwa na wajibu wa kuwasha indicator nitakapo kuwa naendesha chombo cha moto ili kuwasadia watumiaji wengine wa barabara kujua uelekeo wangu!
 
Kama una haraka mfuate tuu point C, Maana ukikaa hapo point B atakuchelewesha
 
Ukiona tu ' Magwanda Ya Trafiki Barabarani' Ujue kuwa Sheria ni Hayo 'Magwanda' ...!

Sheria Zinabadilika Ghafla unatakiwa Kufuata Magwanda Yanaelekeza nini..!

Sasa Wewe Jifanye Mjuaji...ndo Utajua hujui....!
Magwanda ndo Serikali... Ndo kila Kitu.
 
Yeah mkuu ILA elewa kuwa traffic officer's anauwezo ku over run sheria ya usalama barabarani, ila kwa reasonable reason,inatakiwa ufuate maelekezo yake, epuka kuonyesha kuwa ni aggressive driver au hauna respect kwao
 
Back
Top Bottom