Kwa nini Zanzibar in watu wachache lakini wabunge wengi?

Kama wabunge wangekua wanaleta maendeleo basi zanzibar ingekua juu sana!
Mfano zanzibar watu elfu kumi wanawakilishwa na wabunge wawili wa kuchaguliwa hapo bado viti maalumu na kuteuliwa! Wote hao wanapata mshiko sawa kama wa mh Mdee ambaye anawakilisha watu zaidi ya laki tatu!
 
Wakuu nashukru sana kujadili hoja hii. Hapa kuna tatizo la msingi inabidi tupate majibu. Je Zanzibar kuwa na wabunge wengi tofauti na uwiano wa watu na ama ukubwa kijiografia kunalenga kuleta usawa wa uwakilishi kinchi? Kama ndivyo usawa huo ni Kati ya Zbar na nchi gani? Je swala hili haliibui umuhimu wa kuwa na serikali tatu? Niliwahi kushiriki katika shughuli moja ya tadhimini ya serikali Zbar tulichoelezwa nikwamba kodi yote inayokusanywa Zbar inatumika Zbar, fedha za wafadhiri zinazokuja katika serikali ya muungano zinagawanywa kwa uwiano hivyo Zbar inapata mgao wake. Kwa lugha nyingine Zbar haigarimii chochote katika serikali ya muungano. Licha ya hilo bado kuna wafanyakazi wanaotoa huduma Zbar ambayo wanaolipwa na serikali ya muungano (mfano TRA, Police, Jeshi NK.)

Hivi kweli hii si dhahiri kuwa Wanzanzibari ni wanufaika wakubwa wa kodi zetu? Kwanini haya mambo yasiangaliwe upya hasa hili la wabunge wanaowakilisha "kata"?
 
Na licha ya kuwa na vimajimbo vidogodogo(kijiogrsfia) vinavyotawalika kirahisi, bado Wazanzibari wengi ni masikini hohehahe wanaoshindia mlo mmoja ulio substandard?

miundo mbinu ya Zanzibar ni mibovu kuliko maelezo: si majengo, si barabara, si anga.

why?
Ukiweza kuzijua sababu kwa upande wa T.bara ni rahisi kujua kwani matatizo yao yanafanana.au mwenzetu unakaa masaki tu? Tatizo liliuepo hap watu hawaujui muungano lakini wana pretend kuujua
 
Back
Top Bottom