NGULI
JF-Expert Member
- Mar 31, 2008
- 4,803
- 637
Hasa mida ya asubuhi ukiingia ofisini utasikia.....hiiiiii mambooo umependeza wigi lako umenunua wapi? Ilihali ukimwangalia hilo wigi ni kama helmet ya pikipiki ambayo no oversize. Na mwenyewe bila kujua anaanza kutoa location ya eneo alilonunua. Au nguo kavaa imembana na mtu mwenyewe ni mnene na umri haukubaliani na hizo nguo lakini anaambiwa leo umetoka bomba ile mbaya anaitikia asante hizi nimezishusa juzi tu!!! Mm natamani niwaambie ukweli umevaa kibody tight huku kitambi kinaanguka na michirizi ya michelini kwenye mbavu inaoneka, vaa kiafrica upendeze mavitenge makubwa yangekupendeza zaidi.....nk.