Kwa nini wanawake huongopeana hivi?

NGULI

JF-Expert Member
Mar 31, 2008
4,803
637
Hasa mida ya asubuhi ukiingia ofisini utasikia.....hiiiiii mambooo umependeza wigi lako umenunua wapi? Ilihali ukimwangalia hilo wigi ni kama helmet ya pikipiki ambayo no oversize. Na mwenyewe bila kujua anaanza kutoa location ya eneo alilonunua. Au nguo kavaa imembana na mtu mwenyewe ni mnene na umri haukubaliani na hizo nguo lakini anaambiwa leo umetoka bomba ile mbaya anaitikia asante hizi nimezishusa juzi tu!!! Mm natamani niwaambie ukweli umevaa kibody tight huku kitambi kinaanguka na michirizi ya michelini kwenye mbavu inaoneka, vaa kiafrica upendeze mavitenge makubwa yangekupendeza zaidi.....nk.
 
Inawezekana wanapendeza, lakini we unakuwa huoni vizuri labda Nguli. Ila hilo la mawigi hata mimi kwa kuwa siyapendi hasa hayo yakuvaa kama helmet, mtu akipendeza naweza hata nisione kama kapendeza.
 
Inawezekana wanapendeza, lakini we unakuwa huoni vizuri labda Nguli. Ila hilo la mawigi hata mimi kwa kuwa siyapendi hasa hayo yakuvaa kama helmet, mtu akipendeza naweza hata nisione kama kapendeza.
Mkubwa mtu akipendeza utamuona tu, haitaji kipaji maalumu.
 
Kweli sikatai mtu kusifiwa ila anasifiwa kwa ukweli au basi tu imekuwa sehemu ya utamaduni wa mwanamke?? Kusifia hata pasipohitaji sifa?
Jamani acha wasifiwe tu!Wale wasiopendezaga hata siku moja unataka wafe hawajasifiwa?
 
Hahahahaha lohhh
Umenichekesha kwa kweli..
Nabaki humu humu migodini
Staki kufanya kazi na wanawake wa
hivyo lohhhhh
 
Aisee Nguli, ile safari yetu bado iko palepale?

BTW Avatar yako imekupendeza sana. Bado unapiga tizi pale MayFair?
 
Aisee Nguli, ile safari yetu bado iko palepale?BTW Avatar yako imekupendeza sana. Bado unapiga tizi pale MayFair?
Ndio safari iko pale pale, sijabdilika mkuu. Mazoezi ni sehemu ya maisha yangu nikiachaga naugua kabisa na nikienda hospital hawaoni ugonjwa. Ila napiga aerobics zaidi nisije onekana kama mlinzi. Halafu masharti hayo ya kupungua yameshinikizwa zaidi na AFRODENZI
 
Back
Top Bottom