Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,620
- 46,261
Ukiangalia makubaliano, tenda na mikataba mbalimbali ya kibiashara ambayo nchi za Africa huwa zinaingia na nchi au hizo kampuni za nje kutoka Ulaya, Marekani, China, Uarabuni n.k ni ya kunufaisha zaidi hizo nchi na kampuni ila Waafrika wenyewe kwa wenyewe kukubaliana katika mambo ya kibiashara ambayo yatanufaisha Waafrika wenzao ni vigumu sana. Yani Waafrika ni kama tunaona bora zaidi mtu wa bara lingine apate lakini Mwafrika mwenzetu jirani akose!
Kwa mfano nimeona Ruto amemteua Mdachi kuwa Chancellor wa Chuo kikuu cha Nairobi lakini sio rahisi kabisa kwa Mwafrika mwingine tofauti na Mkenya kuteuliwa kushika nafasi chuo katika hiko. Rwanda walikuwa wanapokea wakimbizi kutoka Uingereza wakati Africa imejaa wakimbizi, TANESCO walienda kuchukua kampuni ya IT huko India wakati Kenya na Rwanda kuna kampuni za IT zinafanya vizuri sana, Kuna wakati Kenya ilizuia maziwa ya Uganda lakini ukienda maduka ya Kenya kuna maziwa ya Ulaya na Uarabuni!
Mifano ni mingi sana, Waafrika inabidi tujitafakari katika kufanya biashara pamoja kwa ushirikiano kati yetu sisi zaidi kuzidi mataifa ya mabara mengine. Tunahitaji kuelewa fursa ya biashara kati ya mataifa yetu ina faida kubwa zaidi kuliko na mataifa ya mbali.