Kwa nini tunasherekea siku ya harusi atusheherekei siku wanapoachana???

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,148
Umewahi kujiuliza hili
umewahi kujua nan anakupenda nani akupendi..............,hivi kwa nini watu wanafurahia sana
waakati wanapooana lakini wakiwa wanaachana unakuta wengi wanafurahia kimoyo moyo kwa ndani
je umewahi kujua upendo halisi ni upi......??
Wakati wa harusi wako wanaochanga mpaaka mamilioni lakini umewahi kujiuliza kwa nini
wakati wa kuachana ni mzigo wenu ninyi wawili pekeyenu ..je unahisi waliokuwa wakichangia mamillion
wamekufa ama awapo hatta kushiriki kusuluhisha shida zako za ndoa....sisemi vibaya kuwa makini na ndugu ama marafiki lakini dhumuni kubwa na halisi weekend hii unapoenda kwenye harusi za enzio leo jumamosi ujue kesho ni ya kwako usikae tu unakata maji bure bila kikomo kisa umelipia sh 30,000 kwenye mchango jua siku mojaa na wewe utakuwa pale mbele ukigonganisha glasss na baada ya hapo saa sita usiku ukiwa na mkeo ndio unajua ndoa ni nini

ni mamombi yangu kwako na kwa familia yako jitahidini matatizo yenu muyasuluhishe wenyewe na sio kutegemea ndugu marafiki ama majirani..ndoa ni watu wawili..ingawa kwingine tumeruhusu wa nne kikomo naamini matatizo yakitokeaa ni ninyi wenyewe

amani ya bwana iwatangulie kwa wale mnaoenda kwenye harusi leo jitahidini muwe na kadi msitegemee ndugu kuwaingiza kwa mkupuo kama wachaga enzi hizo ...najua mtakuja kuongea ninapita tu lizy
mbarikiwe
 
kwanini kwenye sherehe yoyote shangwe na vigelegele vinatawala lakini kwenye msiba vilio na huzuni vinatawala?
 
Binadamu wengi ni wanafiki usione kila anayekupigia makofi anakusapoti,wala si kila anayelia msibani ana huzuni wengine wanachekelea kimyakimya hivo hivo kwenye kuachana
 
Walio wengi ni wanafiki, wengine pale wanatumia tu hela zao walizochanga! harusi ikifana sana utasikia ooh.. haitadumu hiyoo.. sijui vile, sijui hivii.., wengine utasikia, kwanza bi harusi/bw. harusi alikuwa hawara wangu, n.k. acheni hizo nyiee!... waombeeni ili ndoa hizi zidumu, tukumbuke kuna leo na kesho, leo kwangu, kesho kwako!
 
Binadamu huwa wapata hamu ya kulia na kucheka muda tofauti kwa hiyo usishangae
 
Katavi unalaana wewe
mi nataka wawe wanachanga michango kama walivyokuwa wakichangia kwenye ndoa ili wanapoachana wasipate shida wanapokwenda hilo ndilo muhimu zaidi ,nimeona wengi wakiachana wengine wanakuwa wamechanganyikiwa wanawekwa muhimbili hata pesa za kujilipia dawa hawana so nashauri wawe wanawachangia jamani
 
Samahani mkuu ushauri wako nimeupata kuwa wawili wasuluhishe matattizo yao, lakini hii ya kusherehekea siku ya kuachana haileti sense kabisa for many reasons ikiwemo kama kuna uzazi umepatikana hapo, hakuna atakayekuwa tayari kubeba mzigo wa kulea watoto kwa miaka kadhaa ijayo.

Pia usisahau kuna watu, binafsi nilishashuhudia mtu amefanya party ya kuachana na mtu wake, maana ilikuwa abusive marriage na kwake ilikuwa kama kujikomboa.
 
yakiwa mema tunafurahi yakiwa mabaya huzuni,msongo wa mawazo na kupata uhayawani
 
Umewahi kujiuliza hili
umewahi kujua nan anakupenda nani akupendi..............,hivi kwa nini watu wanafurahia sana
waakati wanapooana lakini wakiwa wanaachana unakuta wengi wanafurahia kimoyo moyo kwa ndani
je umewahi kujua upendo halisi ni upi......??
Wakati wa harusi wako wanaochanga mpaaka mamilioni lakini umewahi kujiuliza kwa nini
wakati wa kuachana ni mzigo wenu ninyi wawili pekeyenu
..je unahisi waliokuwa wakichangia mamillion
wamekufa ama awapo hatta kushiriki kusuluhisha shida zako za ndoa....sisemi vibaya kuwa makini na ndugu ama marafiki lakini dhumuni kubwa na halisi weekend hii unapoenda kwenye harusi za enzio leo jumamosi ujue kesho ni ya kwako usikae tu unakata maji bure bila kikomo kisa umelipia sh 30,000 kwenye mchango jua siku mojaa na wewe utakuwa pale mbele ukigonganisha glasss na baada ya hapo saa sita usiku ukiwa na mkeo ndio unajua ndoa ni nini

ni mamombi yangu kwako na kwa familia yako jitahidini matatizo yenu muyasuluhishe wenyewe na sio kutegemea ndugu marafiki ama majirani..ndoa ni watu wawili..ingawa kwingine tumeruhusu wa nne kikomo naamini matatizo yakitokeaa ni ninyi wenyewe

amani ya bwana iwatangulie kwa wale mnaoenda kwenye harusi leo jitahidini muwe na kadi msitegemee ndugu kuwaingiza kwa mkupuo kama wachaga enzi hizo ...najua mtakuja kuongea ninapita tu lizy
mbarikiwe

Hapo kwenye bold hapo, maadamu maamuzi ya kuachana ni ya wawili kama yalivyo ya kuamua kufunga ndoa, ingekuwa busara pia hao wanaoamua kuachana kurudisha mamilioni ya fedha walizochangiwa pamoja na asilimia fulani ya usumbufu wa vikao, loh!
 
Baadhi wameshaanza kusherehekea kuachana, but IMO it is very weird to celebrate the end of your marriage....There is nothing to celebrate.

Last edited by a moderator:
Kuchangiana kwenye arusi mara nyingi ni unafiki wetu..Watu wengi huwa hatupendi kuchanga ila tunaona aibu vile tunajuana au undugu.Na ndio maana wengine wanaenda kulipiza kwa kunywa sana au kula sana ili hela yake irudi.
 
Back
Top Bottom