Kwa nini mama tu? Wapi baba?

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,883
2,763
Nimebandika hivi baada ya kuona kupitia runinga, tunzo za kili. Wasanii waliopata tunzo walitoa shukrani zao bila kumsahau mama. Hakuna hata mmoja aliyewashukuru wazazi (baba akiwepo). Au ndio mfumo jike? Hii inaanza kutia hofu. Wapi nafasi ya baba katika mafanikio ya kijana?
 
Hao wanakuwa wamelelewa na mama pekee,mama ndiyo alikuwa mama na baba yake
hapo huna jinsi zaidi ya kumshukuru MAMA tu.
wababa waliwatelekeza either wakiwa tumboni au wakiwa wadogo
 
kama umekua humjui baba, ukalelewa na mama tu, ukapata background ya kuzaliwa kwako. Ukaona kabisa options ya mama kuchoropoa mimba ilikuwepo, lakini hakutoa mimba akakuzaa na akakulea mpaka hapo ulipofikia, unaweza kuwaza hata kumtaja baba?
 
Kutamka Baba ngumu bana kuliko Mama mie sina kumbukumbu ya kutamka Baba mda mrefu sana na amenilea mwanzo mwisho
 
Waliolelewa chini ya utawala wa baba huwa mara nyingi hawaingii kwenye sanaa za namna hiyo.baba hulazimisha mtoto asome tu tena kwa mangumi na mateke.
 
Kuna dhana kuwa japo mama ana nafasi kubwa kwa mwanae kuwa alivyo, bado huyu kijana hawezi kumhofia mama kama baba. Na ndio maana tunaona vituko vya wasanii wetu kama lulu
 
Ni kwa 7bu baba zao huwa hawakubaliani na vitendo vyao vya kijinga vinavyoambatana na usanii wao.
Km ulevi,uzinzi nk.
 
Nimebandika hivi baada ya kuona kupitia runinga, tunzo za kili. Wasanii waliopata tunzo walitoa shukrani zao bila kumsahau mama. Hakuna hata mmoja aliyewashukuru wazazi (baba akiwepo). Au ndio mfumo jike? Hii inaanza kutia hofu. Wapi nafasi ya baba katika mafanikio ya kijana?

Mwanamke na jamii mkuu!
Ma baba wengi ma TP
 
kina baba dhao walichapa lapa kabla watoto hawajaanza kutumia pua zao kuvuta pumzi....HI Mimba si yangu. Tafuta babake... au mi usinitaje.. au mi sitaki kuitwa baba saivi....

sasa watajwe wa nini. cheki hata kwenye harusi nyingi sikuizi mama tu ndo anatunzwa maana baba hakuwepo katika ulezi.....
aliotesha kitu akakimbia.. kusoma kula kuvaa MAMA.
 
Nimebandika hivi baada ya kuona kupitia runinga, tunzo za kili. Wasanii waliopata tunzo walitoa shukrani zao bila kumsahau mama. Hakuna hata mmoja aliyewashukuru wazazi (baba akiwepo). Au ndio mfumo jike? Hii inaanza kutia hofu. Wapi nafasi ya baba katika mafanikio ya kijana?

Na mimi nilijiuliza sana kuhusu hili. Baadae nikahisi kwamba ilitokana na ile tabia yetu wanaume ya enzi za ujana kuingia mitini kukwepa majukumu na hawa watoto wetu hasira zao zote zikaishia kwenye sanaa ambayo haihitaji gharama kubwa kama vile kuhitaji kusomeshwa chuo kikuu na mtu na matokeo yake ndio haya ya kila msanii asimamaye kumkumbuka sana mama yake! Si mnamkumbuka yule wa zamani kidogo aliyeimba:

'Si ulinizaa wewe ukanikataa,
sasa iweje unaona mi nafaa'
 
baba desi, hili ni tatizo/janga ambalo halijawekwa wazi kwa jamii. Tuko wengi katika tasnia na sekta tofauti ambao ni tunda la mama. Familia ni chache sana. Wengi pia ni single parents ndani ya familia
 
Back
Top Bottom