Elections 2010 Kwa nini hofu ya upadre wa Dr. Slaa haina msingi

Kama mtu alidokoa nyama miaka mitano iliyopita then last year hakudokoa kwangu mimi kwenye file lake naandika ana tabia ya udokozi.Sasa Slaa wenu ni kigeugeu.That's it.

Kumbe kadokoa nyama miaka mitano iliyopita bado unakumbuka hilo. Mbona sasa unasahau haraka wanaodokoa hata sasa? Au kwa vile ni wengi na akili yako ni ndogo hivyo sio rahisi kuwashika wote hawa wa sasa, ukabaki na huyo wa zamani ambapo akili yako bado ilikuwa inashika. Sasa kama una akili ndogo kiasi hicho kwanini ujiingize kwenye mijadala mikubwa? Sio lazima ujadili wewe kama huna uwezo nao.
 
Hakuna jambo la msingi kama kushindwa kwake kutunza ahadi.Toka ya upadri hadi ndoa.Hayo ni mambo muhimu.Ninyi kama mnaona ni pumba mimi naona ni muhimu.Nafurahi kuona msimamo wenu ni mmoja so nawajibu collectivelly.Kama mtu alidokoa nyama miaka mitano iliyopita then last year hakudokoa kwangu mimi kwenye file lake naandika ana tabia ya udokozi.Sasa Slaa wenu ni kigeugeu.That's it.
CCM imeshindwq kutunza ahadi ya kuwaletea maendeleo waTZ kwa maiaka 50 sasa, thats is more important kuliko maisha ya mtu mmoja. They are the ones who should go.
 
Nilishasema msimu huu watamiminika kama nzige. Na baada ya uchaguzi kutokomea mmoja mmoja.
TandaleOne
  • profile.png
    View Profile
  • forum.png
    View Forum Posts
  • message.png
    Private Message
  • article.png
    View Articles
  • add.png
    Add as Contact
user-online.png
Member
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
Join DateSat Sep 2010Posts42 Thanks : 8
Thanked 6 Times in 6 Posts
Rep Power0

Na wengine mtawafungia bila sababu za msingi.Wapinzani huku mnaikaba demokrasia????!!Shame.
 
Tunapofuata mambo madogo madogo ya unyumba wa mtu binafsi kwa gharama ya mambo makubwa ya taifa ndipo tunapokosa mwelekeo na kubaki tukirudi nyuma wakati majirani zetu wakizidi kusonga mbele. Dr. Slaa alikuwa padri kwa miaka kama 14 hivi tangu mwaka 1977 hadi mwaka 1991, halafu akawa mbunge kwa 15 tangu mwaka 1995 hadi mwaka 2010. Ni jambo gani tusilojua kuhusu jamaa huyu linalotufanya tutumie nguvu nyingi kutafuta kama ni padri au siyo padri? Kwa nini basi tusisema kuwa ni mbunge wa Karatu anayemaliza muda wake amaboyo ni nafasi yake ya hivi karibuni zaidi kuliko kuangalia kazi aliyofanya miaka karibu ishirini iliyopita? Kama kazi aliyofanya miaka ishirini iliyopita inazidi umuhimu kazi aliyofanya miaka kumi na tano iliyopita basi kuna wanasiasa wengi Tanzania hawatakuwa na sifa za kuongoza kwa vile baadhi yao walikuwa hawajatimiza umri unaotakiwa au walikuwa bado mashuleni, wengine walikuwa ni wanajeshi, na wengine walikuwa ni wababaishaji wa mitaani tu.

Let us be serious

Kama kazi yake aliyofanya kama mtumishi wa dini yake ndilo tatizo kubwa linalopigiwa kampeini ya kisisas sasa, basi hata wafuasi wote wa dini aliyowahi kutumikia hawana sifa za kuingoza Tanzania, kwa hiyo wakatoliki wote siyo sehemu ya taifa hili.

Where are we heading to?
 
Tunamwamini, anaweza, ataleta neema, ushahidi tunao hatudanganyiki! Songa mbele Dr Slaa, hizo ni mbinu za CCM iliyojaa mafisadi. Wanaotumia kila aina mbinu kutaka kurudi madarakani. Tumechoka, hatutaki! hata kama mtahinda lakini mumeona hali halisi ilivyo, mumesikia kilio cha watanzania kuwa inshu siyo Upadre ni maisha ya Watanzania na nchi yao kuporwa na walowezi.

We need creative minds now, we don't need this shit! tunataka kuona watu wanaishi kwa amani a upendo, siyo kiujanja ujanja tu kama sasa. Watu hawafanyi kazi, wala hawana huruma hadi mwenyekiti wa kitongoji ni walafi kama nini, what do you expect? do you think JK can change the system by just laughing with fraud? Sijashawishika, labda mchague ,mtu mwingine kama Ahmed Salim, nitamsikiliza kama naye hataeleweka, why should I vote for someone who is not serious. Siko tayari na jamaa zangu hatuko tayari kuwapa watu kama hao.:A S-coffee:

Unamuamini wewe na wale wachache waliompiga Makenji kule Kinondoni.
Na kama unaamini hivyo,si wote tunaamini hivyo.
How do I trust a man who can't keep his promises or vows???
The best part of the show's he won't win.(Am sure he knows it though anajua pia wapo watu kama ninyi with your way of thinking).
 
Unamuamini wewe na wale wachache waliompiga Makenji kule Kinondoni.
Na kama unaamini hivyo,si wote tunaamini hivyo.
How do I trust a man who can't keep his promises or vows???
The best part of the show's he won't win.(Am sure he knows it though anajua pia wapo watu kama ninyi with your way of thinking).

You are so fun! huwezi kumuamini Dr. Slaa cause he can't keep his promises or Vows! hahaah very fun, yet you trust Kikwete ambaye ameshindwa ku keep promise yake as well, hebu tuambie ni mtanzania gani zaidi ya MAFISADI wa CCM aliyepata MAISHA BORA kama alivyo ahidi JK! You know what, ninafuraha sana baada ya kugundua kumbe hata watanzania wa hali ya chini sana ( wasukuma guta) sasa wameisha gundua kuwa JK is a joker! Kama uliangalia kipindi cha USWAZI cha Chanel 5 (EATV) jana jioni basi unaweza kuwa na jibu!
 
Dr.Slaa ni Mlei????Ndo inavyosomeka katika website yake.Jamani huu si ukweli!!!!Sakramenti ya upadrisho haifutiki.That's the Roman Catholic Law!!!!!!!!


Kwa muda mrefu sasa vyombo mbalimbali vya habari na watu binafsi wamekuwa wakieneza habari kuwa Dr. Willibrod Slaa ni Padre wa Kanisa Katoliki na kuwa kwa vile aliwahi kuwa Padre (Kuhani) ndani ya Kanisa hilo ina maana kuwa hadi leo hii yeye ni Padre kama walivyo mapadre wengine. Wengi wanaosema mambo haya wanaonesha kutokujua au hata kujaribu kujua mafundisho ya Kanisa Katoliki juu ya Upadre na jinsi gani mtu anaweza kuwa Padre na akauacha na kuwa Mlei kama Walei wengine.

Kanisa Katoliki linazo Sakramenti saba ambazo ni Ubatizo, Kipaimara, Komunio (Ekaristia), Upatanisho (Maungamo), Ndoa, Upadrisho (Ukuhani) na Mpako wa Wagonjwa. Sakramenti hizo saba zipo ambazo zinatolewa mara moja tu kwa mtu na nyingine ambazo zaweza kurudiwa. Tunaposema "kutolewa mara moja" maana yake ni kuwa mtu anapopatiwa uwezo na nguvu za kuanza kupokea neema za sakramenti hizo hilo hufanywa mara moja tu na hairudiwi tena (isipokuwa kama hakuna uhakika kuwa alishapokea mara hiyo ya kwanza). Hizi ni Ubatizo, Kipaimara na Upadrisho. Zingine ni zile ambazo mtu anapokea mara ya kwanza lakini katika maisha yake ya kila siku anarudia kupokea mara kwa mara kwa kadiri inavyohitajika. Hizi ni Ekaristia na Maungamamo japo nazo huanza kupewa mara moja tu na kutoka hapo ni kuendelea kuchota neema zake kwa taribu zinazotakiwa. Na zipo ambazo hufanywa upya kabisa kama vile hazijawahi kufanywa kabisa; hizi ni ndoa na mpako wa wagonjwa.

Siyo kusudio letu kuelezea Theolojia ya sakramenti hizo ila tunataka kuzungumzia hili ambalo linaonekana kuwashindwa watu kuelewa. Ni kweli Dr. Slaa alipewa Sakramenti ya Upadrisho ndani ya Kanisa Katoliki baada ya kumaliza maandalizi yake ya kazi hiyo. Upadre siyo kama kazi nyingine ambazo mtu "anasomea"; si sawa na Udaktari, Uwakili au Uhasibu. Upadre ni Sakramenti ya Ukuhani ambayo mtu anaandaliwa kuiingia na kuitumikia. Ndio maana kimsingi kabisa, hata mtu ambaye hajasomea kabisa mambo ya Theolojia na Filosofia anaweza akapewa Upadrisho. Lakini kwa miaka mia nyingi Makanisa (Mashariki na Magharibi) yamekuwa yakiwaandaa wale wanaotaka kuingia katika "Daraja Takatifu" kwa mafunzo maalum ya mambo ya dini, falsafa, utawala n.k Ukiondoa mafunzo ya Theolojia ya Katoliki mafunzo mengine ya Falsafa, utawala, au elimu nyingine yoyote ni sawa kabisa na mafunzo yanayotolewa katika vyuo vikuu vingine.

Mtu akishapata daraja ya Ushemasi na baadaye Upadre basi anakuwa ni "Kuhani Milele" na hakuna kitu chochote ambacho kinaweza kufanywa kuondoa daraja hilo. Hii huitwa "alama isiyofutika". Ni alama ile ile ambayo inapatikana katika Sakramenti ya Ubatizo na Kipaimara ambapo mtu akishabatizwa ubatizo wake hauwezi kurudiwa tena kwani alama hiyo ya neema haifutiki. Ni kwa sababu hiyo mtu ambaye ameshawahi kupata upadrisho ataendelea kuwa kuwa na alama hiyo milele.

Kuwa na daraja hilo katika nafsi haina maana mtu ni mhudumu wa altare tena yaani kuhani. Hivyo, mtu anaweza kuamua kuacha kabisa kazi ya upadre, akaamua kuasi, au akaamu kujiunga na dini nyingine au kutoamini kabisa uwepo wa Mungu, lakini ile alama haifutwi na milele anabakia nayo. Kwa maana hiyo, Padre wa Kikatoliki anaweza kuacha, kufukuzwa, kuachishwa kazi za kila siku za kutoa huduma ya Upadre lakini bado anabakia kuwa ni padre moyoni. Hivyo, mtu huyo aliyeacha hastahili kuitwa "Padre X" kwa maana ya mapadre ambao bado wako kwenye huduma. Ni sawa na Daktari aliyeacha kazi ya Udaktari au kufukuzwa Udaktari au Uwakili lakini bado mafunzo na uwezo wa kutoa huduma hiyo akawa bado anao japo haruhusiwi tena kufanya hivyo. Wapo watu ambao kutokana na mazoea wataendelea kumuita "Daktari" japo hafanyi tena huduma hiyo.

Jambo hili ni muhimu kulielewa. Mtu ambaye ameacha yeye mwenyewe upadre bila kurejeshewa hali yake ya ulei (yaani uumini wa kawaida) kwa mujibu wa taratibu za Kanisa basi mtu huyo bado ni Padre na haruhusiwi kupewa Sakramenti ya Ndoa. Hata hivyo, Kanisa Katoliki lina utaratibu wa kumfanya mtu aliyewahi kuwa padre kurejeshwa kwenye hali ya ulei (yaani kuondolewa kabisa kazi na haki ya kufanya kazi za upadre na kuwa muumini wa kawaida kabisa). Mtu ambaye ameondolewa upadre kwa utaratibu wa Kanisa na kibali cha Vatikani anaondolewa haki na majukumu yote ya mapadre wengine isipokuwa mambo mawili tu yaani useja (celibacy) na kusikiliza maungamo ya mtu aliyekaribu na kifo.

Hilo la useja linahitaji kibali kingine kuondolewa ili aruhusiwe kuoa. Hata hivyo kwa vile padre ni padre milele basi mtu aliyewahi kuwa Padre anaweza kusikiliza maungamo na kutoa msamaha kwa mtu ambaye yuko katika hatari ya kifo tu.
Mfano mzuri wa kuelewa hili ni aliyekuwa Askofu Ferdando Lugo wa San Pedro huko Paraguay. Askofu Lugo alitaka kuingia katika siasa kitu ambacho kinakatazwa na Kanuni za Kanisa Katoliki. Askofu Lugo aliomba Kanisa Katoliki limruhusu arejee katika hali ya Ulei ili aweze kushiriki katika siasa lakini Kanisa lilimkatalia lakini Lugo aliendelea kugombea na aliposhinda uchaguzi Mkuu wa Paraguay Kanisa Katoliki lilikubali kumuondolea Upadre wake na kumrejesha katika Ulei. Hivyo, Rais wa sasa wa Paraguay ni Askofu wa zamani wa Kanisa Katoliki ambaye alirejeshwa katika Ulei.

Hii ina maana ya kwamba, Dr. Slaa siyo tu ni mlei lakini anayo haki kama wakatoliki wengine walei kushiriki katika nafasi ya uongozi kwani hajavunja sheria yoyote ya Kanisa, wala hajaenda nje ya haki zake za kikatiba. Dr. Slaa sasa hivi ni muumini Mlei kama wengine na atakapoamua kupata sakramenti nyingine yoyote ya Kanisa ataweza kufanya hivyo kwa uamuzi wake yeye mwenyewe kwani alifuata taratibu za kanisa za kurejeshwa katika maisha ya mlei.

Hivyo, Dr. Slaa siyo mtumishi wa Kanisa Katoliki na siyo padre kwa maana ya kuwa anahaki na majukumu yote ya mapadre wengine. Yeye ni muumini Mlei ambaye kutokana na nafasi yake ya kuwa aliwahi kuwa padre anabakia na haki za waumini wengine walei ndani ya kanisa hilo na vile vile uwezo wa kusikiliza maungamano ya mtu aliye katika hatari ya kifo TU.

Source:Dr. Slaa ni Mlei - Dr. Wilbrod Slaa 2010

Pumba!
 
Tunapofuata mambo madogo madogo ya unyumba wa mtu binafsi kwa gharama ya mambo makubwa ya taifa ndipo tunapokosa mwelekeo na kubaki tukirudi nyuma wakati majirani zetu wakizidi kusonga mbele. Dr. Slaa alikuwa padri kwa miaka kama 14 hivi tangu mwaka 1977 hadi mwaka 1991, halafu akawa mbunge kwa 15 tangu mwaka 1995 hadi mwaka 2010. Ni jambo gani tusilojua kuhusu jamaa huyu linalotufanya tutumie nguvu nyingi kutafuta kama ni padri au siyo padri? Kwa nini basi tusisema kuwa ni mbunge wa Karatu anayemaliza muda wake amaboyo ni nafasi yake ya hivi karibuni zaidi kuliko kuangalia kazi aliyofanya miaka karibu ishirini iliyopita? Kama kazi aliyofanya miaka ishirini iliyopita inazidi umuhimu kazi aliyofanya miaka kumi na tano iliyopita basi kuna wanasiasa wengi Tanzania hawatakuwa na sifa za kuongoza kwa vile baadhi yao walikuwa hawajatimiza umri unaotakiwa au walikuwa bado mashuleni, wengine walikuwa ni wanajeshi, na wengine walikuwa ni wababaishaji wa mitaani tu.

Let us be serious

Kama kazi yake aliyofanya kama mtumishi wa dini yake ndilo tatizo kubwa linalopigiwa kampeini ya kisisas sasa, basi hata wafuasi wote wa dini aliyowahi kutumikia hawana sifa za kuingoza Tanzania, kwa hiyo wakatoliki wote siyo sehemu ya taifa hili.

Where are we heading to?

nadhani kama hawa watu wangeumia nguvu nyingi namna hii kuelewa ubaya wa mafisadi ningewasifu na ubaya wa kusaini mikataba hotelini nje nchi mbona maendeleo yangekuja kwa speed ya ajabu

jamani watanzania wenzangu tujifunze kuacha kupoteza muda na kuweka mada ambazo zipo nje ya mtizamo mpana wenye tija
 
Mhhh!!! Kampeni mwaka huu zaenda kusiko kabisa!! Sababu yake? Just say it....CCM maji marefu this time....mtajibeba tu hata mlete mambo chungu nzima yasiyohusu, wananchi wameamua kuitosa CCM. Hivi huyo JK wenu akipigwa darubini kali mtaona nini? Si uchafu.... na uchafu.... na uchafu.... na uchafu.....!!!! Turudi kwenye mada za msingi, kama nyie kweli ni wanaume!
 
Mhhh!!! Kampeni mwaka huu zaenda kusiko kabisa!! Sababu yake? Just say it....CCM maji marefu this time....mtajibeba tu hata mlete mambo chungu nzima yasiyohusu, wananchi wameamua kuitosa CCM. Hivi huyo JK wenu akipigwa darubini kali mtaona nini? Si uchafu.... na uchafu.... na uchafu.... na uchafu.....!!!! Turudi kwenye mada za msingi, kama nyie kweli ni wanaume!

Kwangu dole tu nakupa, Mkuu Zak. Kwani vita ya madongo na uchafu CCM hawataiweza kamwe kwa machafu yao yaliyokithiri.. na ndo maana wakiguswa tu -- eti ooh "matusi".
 
Unamuamini wewe na wale wachache waliompiga Makenji kule Kinondoni.
Na kama unaamini hivyo,si wote tunaamini hivyo.
How do I trust a man who can't keep his promises or vows???
The best part of the show's he won't win.(Am sure he knows it though anajua pia wapo watu kama ninyi with your way of thinking).


Kwanza karibu jamvini halafu asijui baada ya uchaguzi utaondoka au utabaki!

Hapo kwenye red inaelekea mmna amini kila anachosema JK maana huyo ndio anayejua ku -keep promises like mabasi yaendayo kasi tangu uchaguzi wa 2005 hadi leo hayajaonekana sasa kaja na flyover sijui ataziweka wapi ikiwa ule mradi wa mabasi umemshinda??? SHAME ON YOU AND OTHER CCM. Unaacha kujadili mambo ya msingi unajadili UDINI.

Kumbuka WATANZANIA WANATAKA KIONGOZI ANAYEJALI MASLAHI YAO NA ANAEOGOPA KUHUJUMU NCHI IKIWEMO UFISADI, KUJILIMBIKIZIA MALI. HATA MWL NYERERE (RIP) ALISEMA KIONGOZI BORA LAZIMA AWE MCHA MUNGU ILA HATUTAMCHAGUA KWASABABU YA KABILA,RANGI WALA DINI! Upo hapo ndugu yangu
 
kwa muda mrefu sasa vyombo kadhaa mbalimbali vya habari na watu binafsi vimekuwa vikieneza habari kuwa dk. Wilibroad slaa ni padre wa kanisa katoliki na kuwa kwa vile aliwahi kuwa padre (kuhani) ndani ya kanisa hilo ina maana kuwa hadi leo hii yeye ni padre kama walivyo mapadre wengine.

Kutokana na madai hayo ya kuwa dk. Slaa bado ni padre hivyo hastahili kuwa rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania. Wengi wanaosema mambo haya wanaonyesha kutokujua mafundisho ya kanisa katoliki juu ya upadre na jinsi gani mtu anaweza kuwa padre na akauacha na kuwa mlei kama walei wengine.

Kanisa katoliki linazo sakramenti saba ambazo ni ubatizo, kipaimara, komunio (ekaristia), upatanisho (maungamo), ndoa, upadrisho (ukuhani) na mpako wa wagonjwa.
Sakramenti hizo saba zipo ambazo zinatolewa mara moja tu kwa mtu na nyingine ambazo zaweza kurudiwa. Tunaposema "kutolewa mara moja" maana yake ni kuwa mtu anapopatiwa uwezo na nguvu za kuanza kupokea neema za sakramenti hizo hilo hufanywa mara moja tu na hairudiwi tena (isipokuwa kama hakuna uhakika kuwa alishapokea mara hiyo ya kwanza). Hizi ni ubatizo, kipaimara na upadrisho.

Nyingine ni zile ambazo mtu anapokea mara ya kwanza lakini katika maisha yake ya kila siku anarudia kupokea mara kwa mara kwa kadiri inavyohitajika. Hizi ni ekaristia na maungamamo japo nazo huanza kupewa mara moja tu na kutoka hapo ni kuendelea kuchota neema zake kwa taribu zinazotakiwa. Na zipo ambazo hufanywa upya kabisa kama vile hazijawahi kufanywa kabisa; hizi ni ndoa na mpako wa wagonjwa.

Si kusudio langu kuelezea theolojia ya sakramenti hizo ila nataka kuzungumzia hili ambalo linaonekana kuwashinda watu kuelewa. Jambo hili kwa wengine wanalipa ugumu usiostahili kwani unahitaji kukaa chini kwa sekunde chache tu kuelewesha na wewe mwenyewe ukajikuta unapata ule wasaa wa kusema “aha! Nimekuelewa”. Hata hivyo, natarajia kutokueleweka kwa baadhi ya watu kwa sababu aidha ni wagumu mno kuelewa au wana wepesi wa kusahau.

Ni kweli dk. Slaa alipewa sakramenti ya upadrisho ndani ya kanisa katoliki baada ya kumaliza maandalizi yake ya kazi hiyo. Upadre si kama kazi nyingine ambazo mtu "anasomea"; si sawa na udaktari, uwakili au uhasibu. Upadre ni sakramenti ya ukuhani ambayo mtu anaandaliwa kuiingia na kuitumikia. Ndiyo maana kimsingi kabisa, hata mtu ambaye hajasomea kabisa mambo ya theolojia na falsafa anaweza akapewa upadrisho endapo haja kama hiyo inatokea.

Lakini kwa miaka mia nyingi makanisa (mashariki na magharibi) yamekuwa yakiwaandaa wale wanaotaka kuingia katika "daraja takatifu" kwa mafunzo maalumu ya mambo ya dini, falsafa, utawala n.k ukiondoa mafunzo ya theolojia ya katoliki mafunzo mengine ya falsafa, utawala, au elimu nyingine yoyote ni sawa kabisa na mafunzo yanayotolewa katika vyuo vikuu vingine.

Mtu akishapata daraja ya ushemasi wa mpito (hatua ya kwanza kabla ya upadre) na baadaye upadre basi anakuwa ni "kuhani milele kwa mfano wa melkizedeki" na hakuna kitu chochote ambacho kinaweza kufanywa kuondoa daraja hilo. Hii huitwa "alama isiyofutika". Ni alama ile ile ambayo inapatikana katika sakramenti ya ubatizo na kipaimara ambapo mtu akishabatizwa ubatizo wake hauwezi kurudiwa tena kwani alama hiyo ya neema haifutiki. Kama vile wakristo wote waliobatizwa nao wanayo alama ya kudumu ya ukristo wao. Hata mkatoliki anapoacha dini, kuhamia dhehebu jingine au kuhamia dini nyingine alama hii ya ubatizo haifutiki.

Kutokana na hilo mkatoliki huyo akiamua kurudi kwenye imani katoliki basi habatizwi tena zaidi ya kuungamishwa imani ya mitume. Alama hii ya ubatizo si kwa wakatoliki tu, kanisa katoliki linatambua kama ni halali ubatizo unaofanywa na madhehebu mengine ya kikristu (japo si yote) kama vile waanglikana na walutheri.

Ndiyo maana wakatoliki, kwa mfano, wakimpokea mkristu anayetoka ulutheri au anglikana ambaye amebatizwa huko hatobatizwa tena kwenye ukatoliki atapokelea tu baada ya kukiri imani katoliki.

Hili nalo ni kweli kwa mtu analiyepadrishwa. Alama yake ya upadrisho wake ni ya kudumu na hakuna kitu ambacho yeye au mtu mwingine anaweza kufanya kuifuta milele. Hata yeye mwenyewe hawezi kuifuta kwa kutoamini au kukana uwepo wa mungu. Ni kwa sababu hiyo mtu ambaye ameshawahi kupata upadrisho ataendelea kuwa na alama hiyo milele. Hili ni fundisho ambalo ni msingi wa kuelewa padre ambaye bado anahudumu na padre ambaye ana alama ya kudumu. Mapadre wote wanayo alama hii ya kudumu lakini si wote wanaweza kuhudumu kama mapadre.

Kwa maana hiyo, padre wa kikatoliki anaweza kuacha, kufukuzwa, kuachishwa kazi za kila siku za kutoa huduma ya upadre lakini bado anabakia kuwa ni padre moyoni. Hivyo, mtu huyo aliyeacha hastahili kuitwa "padre x" kwa maana ya mapadre ambao bado wako kwenye huduma. Ni sawa na daktari aliyeacha kazi ya udaktari au kufukuzwa udaktari au uwakili lakini bado mafunzo na uwezo wa kutoa huduma hiyo akawa bado anao japo haruhusiwi tena kufanya hivyo. Wapo watu ambao kutokana na mazoea wataendelea kumuita "daktari" japo hafanyi tena huduma hiyo.

Jambo hili ni muhimu kulielewa. Mtu ambaye ameacha yeye mwenyewe upadre bila kurejeshewa hali yake ya ulei (yaani uumini wa kawaida) kwa mujibu wa taratibu za kanisa basi mtu huyo bado ni padre na haruhusiwi kupewa sakramenti ya ndoa na anafungwa na vifungo vingi zaidi.

Hata hivyo, kanisa katoliki lina utaratibu wa kumfanya mtu aliyewahi kuwa padre kurejeshwa kwenye hali ya ulei (yaani kuondolewa kabisa kazi na haki ya kufanya kazi za upadre na kuwa muumini wa kawaida kabisa). Mtu ambaye ameondolewa upadre kwa utaratibu wa kanisa (laicization –kufanywa mlei) na kibali cha vatikani anaondolewa haki na majukumu yote ya mapadre wengine isipokuwa mambo mawili tu yaani useja (celibacy) na kusikiliza maungamo ya mtu aliyekaribu na kifo.

Hilo la useja linahitaji kibali kingine kuondolewa ili aruhusiwe kuoa. Hata hivyo, kwa vile padre ni padre milele basi mtu aliyewahi kuwa padre anaweza kusikiliza maungamo na kutoa msamaha kwa mtu ambaye yuko katika hatari ya kifo tu.

Kwa mfano, wamesafiri mahali na gari limepinduka na hakuna msaada wa karibu na yupo mtu ambaye ni mkatoliki (au mtu mwingine mwenye imani hiyo ya maungamano) na akaomba kama kuna padre asikilize maungamano yake basi yule aliyekuwa padre anaweza kabisa kusikiliza maungamo hayo na kumpatia ondoleo la dhambi. Japo kama na yeye atanusurika kuna utaratibu wa kutoa taarifa kwa askofu wa eneo hilo juu ya tukio hilo bila kutoa taarifa ya kilichoungamwa.

Sasa basi, si ajabu kabisa kwa padre kufuata utaratibu na kurejeshewa hali yake ya ulei. Pindi hilo linapotokea basi padre huyo hupewa masharti yake mapya ya hali yake hiyo mpya ya jinsi gani aishi kama asiye padre.

Miongoni mwa mambo hayo ni kukatazwa kuvaa nguo yoyote ya kipadre (kama kola ya kirumi shingoni), kukatazwa kukaa katika eneo la kanisa, kunyimwa haki za matunzo atakapostaafu kama mapadre wengine, kukatazwa hata kuwa mhudumu wa komunio ndani ya kanisa ili isije kuwachanganya watu na wengine wanaopewa masharti ya kutofundisha elimu ya theolojia katika vyuo visivyo vya kikatoliki n.k lengo ni kuhakikisha kuwa mtu huyo anabakia ni padre jina tu na si mhudumu.

Jambo kubwa, hata hivyo, ni kuwa watu wanachanganya masharti ya sheria ya kanisa yanayomkataza padre mhudumu kushiriki kugombea nafasi ya kisiasa. Sheria ya kanisa namba 285 kwenye mojawapo ya sehemu zake ndogo inakataza kwa padre mhudumu kushiriki katika nafasi ya kuchaguliwa katika mambo ya siasa. Hivyo, paroko au paroko msaidizi mahali au padre mwingine yoyote ambaye bado yuko katika huduma haruhusiwi kugombea uchaguzi au nafasi ya kisiasa.

Hii kanuni hata hivyo haifuatwi wakati wote. Historia inao mapadre kadhaa ambao kutokana na matakwa yao wenyewe waliamua kushiriki katika nafasi za kisiasa wakati mwingine kinyume na maelekezo ya uongozi wa juu wa kanisa (maaskofu wao au vatican).

Mwaka jana huko ufilipino padre edd panlilio alitamani kuwa rais wa nchi hiyo mojawapo yenye wakatoliki wengi duniani. Kwa vile alikuwa bado ni padre mhudumu sheria za kanisa zilikataza yeye kufanya hivyo. Hata hivyo, alikuwa tayari kuomba kuruhusiwa kuwa mlei ili agombee nafasi hiyo.

Mfano mzuri wa kuelewa hili ni aliyekuwa askofu ferdando lugo wa san pedro huko paraguay. Askofu lugo alitaka kuingia katika siasa kitu ambacho kinakatazwa na kanuni za kanisa katoliki. Askofu lugo aliomba kanisa katoliki limruhusu arejee katika hali ya ulei ili aweze kushiriki katika siasa lakini kanisa lilimkatalia, yeye aliendelea kugombea na aliposhinda uchaguzi mkuu wa paraguay kanisa katoliki lilikubali kumuondolea upadre wake na kumrejesha katika ulei. Hivyo, rais wa sasa wa paraguay ni askofu wa zamani wa kanisa katoliki ambaye alirejeshwa katika ulei.

Hii ina maana ya kwamba, dk. Slaa si tu ni mlei lakini anayo haki kama wakatoliki wengine walei kushiriki katika nafasi ya uongozi kwani hajavunja sheria yoyote ya kanisa, wala hajaenda nje ya haki zake za kikatiba. Dk. Slaa sasa hivi ni muumini mlei kama wengine na atakapoamua kupata sakramenti nyingine yoyote ya kanisa ataweza kufanya hivyo kwa uamuzi wake yeye mwenyewe kwani alifuata taratibu za kanisa za kurejeshwa katika maisha ya mlei.

Hivyo, dk. Slaa si mtumishi wa kanisa katoliki na si padre kwa maana ya kuwa anahaki na majukumu yote ya mapadre wengine. Yeye ni muumini mlei ambaye kutokana na nafasi yake ya kuwa aliwahi kuwa padre anabakia na haki za waumini wengine walei ndani ya kanisa hilo na vile vile uwezo wa kusikiliza maungamano ya mtu aliye katika hatari ya kifo tu.

Hii ina maana ya kwamba dk. Slaa anayo haki kama mtanzania mwingine bila kujali dini yake au nafasi yake katika dini hiyo kugombea nafasi ya urais.

Hili ni muhimu kuelewa kuwa katiba yetu haimkatazi hata padre mhudumu kugombea nafasi ya urais au ubunge kama akitaka, makatazo hayo yako kwenye kanisa na si kwenye katiba yetu. Hivyo, hata kama leo akatokea padre, shehe, mchungaji n.k akataka kugombea nafasi yoyote ya ubunge basi anazo haki hizo.

Tayari tunajua wapo wasomi wengi tu wa dini zetu kubwa mbili ambao wamekwishakuingia bungeni. Dk. Slaa ameshakuwa mbunge kwa vipindi vitatu. Wapo na wabunge wengine na hata katika nafasi nyingine za kisiasa za watu ambao wamewahi kushika elimu ya juu ya dini za kikristu na kiislamu na hatukuwahi kuona watu wanalalamika kuwa kwanini watu waliowahi kuwa wachungaji (au walio bado wachungaji), mashehe au walimu wa dini kuingia na kuchaguliwa kwenye siasa.

Kama tunakubali kuwa watu hao wote wameweza kutimizwa matakwa ya katiba yetu na tukawakubali kwa nini inapofika kwenye suala la urais tuanze kutoa sababu zisizo na kichwa wala miguu? Hivi leo kama kikwete angekuwa ni msomi wa dini ya kiislamu au mtu aliyewahi kuwa shehe huko nyuma kweli tungeweza kwa haki kusema kuwa hilo peke yake linamfanya asistahili kuwa rais wetu kama tunamkubali?

Lakini jambo la mwisho ambalo linaonekana kuwasumbua watu wengine na halihitaji maneno mengi kwa sababu hapo juu tayari nimeliashiria ni hofu ya baadhi ya watu kuwa ati dk. Slaa kwa vile aliwahi kuwa padre basi akiingia madarakani atakuwa chini ya maelekezo ya baraza la maaskofu au vatican yenyewe.

Kwa vile nimekwishakusema hapo juu kuwa mtu akisharudishwa kwenye hali ya ulei hawi tena chini ya utawala, nidhamu au maelekezo ya askofu wake kama mapadre wengine kumbe dk. Slaa hayuko chini ya askofu wa mbulu, baraza la maaskofu au vatican kiutawala. Yuko kama mkatoliki mwingine yoyote ambaye anaweza kwenda popote, kufanya biashara yoyote, kuishi popote na yeyote bila kulazimishwa kuulizwa au kutoa maelezo kwa mtu yeyote.

Hii ina maana ya kwamba hakuna mtu wa baraza la maaskofu ambaye anaweza kumuita dk. Slaa ati ampatie maelezo au mtu ambaye anaweza kuingilia shughuli zake za kisiasa. Viongozi wa kanisa wameachiwa eneo la kiroho tu kama ilivyo kwa wachungaji, mashehe, na viongozi wengine wa dini kwa imani ya waumini wao.

Tukikubali kuwa ati kwa vile mtu amewahi kuwa mkatoliki basi atapokea maelekezo toka kwa uongozi wa kanisa kwenye mambo ya kisiasa ni lazima tukubali kuwa mtu wa dini nyingine au dhehebu jingine naye ataweza kuburuzwa na viongozi wake wa dini.
Hadi hivi sasa tunaweza kuona wazi kuwa mambo kadhaa ambayo dk. Slaa ameyafanya au kuyasema hadharani nina uhakika baadhi ya viongozi wa dini wasingependa ayaseme jinsi hiyo au wangeweza hata kumkalisha chini.

Dk. Slaa ameweza kujionyesha kuwa ni mtu wa kuthubutu, yuko huru na haangalii nyani usoni. Kama alivyozungumza siku chache zilizopita staili yake hiyo ya utawala inafahamika hata kwa mapadre na viongozi wengine wa kanisa ambao aligongana nao wakati akiwa katibu wa baraza la maaskofu katoliki.

Tanzania haimhitaji padre kuwa rais, tanzania haihitaji mchumi kuwa rais, tanzania haihitaji daktari kuwa rais, tanzania haihitaji mwalimu kuwa rais, na vile vile haihitaji shehe kuwa rais. Hizo zote si sifa za kuwa rais.

Tanzania inahitaji mtanzania mwenye kutimiza masharti ya katiba kuwa rais na awe ni mtu mwenye uwezo wa kutuongoza tunakotaka kwenda na ambaye atakuwa tayari kutupa uongozi bora tunaouhitaji kuelekea katika safari ya ujenzi mpya wa taifa.

Kama hilo litamhusisha mtu aliyewahi kuwa mchumi, mkuu wa wilaya, waziri wa mambo ya nje au mtaalamu wa nyota na iwe! Lakini kama itamtaka mtu aliyewahi kuwa padre basi na iwe, kwani tukianza ubaguzi kwa sababu ya maisha ya kidini ambayo mtu amewahi kuyaishi, itakuwaje kwa wale ambao leo wanagombea na wamewahi kuwa waganga wa kienyeji au bado ni waganga wa kienyeji?

Source: Raia mwema

padri anaweza kuwa rais wa nchi hata kama bado ni padri katika nchi zenye wachristo wengi na ni lazima nchi hio iwe ya kidemocrasia kweli sio tanzania.
Dr. Slaa anaweza kuwa ni kiongozi mzuri ndani ya kanisa , na bungeni ameonesha uhodari wa kupasua mabomu ama scandal bungeni ..

Pengine hii ilikua ni njia ya kutafuta umaarufu ili kuja kugombea urais. Sio sifa inayotosha kuwashawishi watu wamuamini hasa ikizingatiwa chadema ni chama kichanga sana.

Suali jee kama padri anaweza kuwa rais wa nchi hii ?? Jawabu abaweza katiba haimkatazi...lakini jee raia wa nchi hii wanamwamini kumpa kura zao ?
Jawabu sio rahisi....kwa nini ??? Kwa sababu nchii hii tayari kuna mgawanyiko mkubwa wa kidini ..kila mtu anavutia upande wake ki-maslahi...japo hakuna mfarakano...wa magomvi lakini hakuna kuaminiana huu ndio ukweli....hivyo sio rahisi upande wa waislam kumpa kura mtu ambae amewahi kuwa padre.....hasa wa kikatoliki.....mtakumbuka waislamu namna gani wanavolalama kwamba wakati wa nyerere mapadri walipendelewa tena hasa wa kikatoliki....maandishi yao yapo na ushahidi wao upo...hivyo sio rahisi kumwamini dr slaa hata kidogo...kura zao ni muhimu sana kumweka mtu yoyoyte ikulu...

Ni hivyo hivyo kama sheikh mussa kundecha ange gombea urais ....wakristo wangekua na mashaka nae...na magazeti na hapa jf....angepewa majina kama ..mujahidina....

So slaa anaweza kuwa rais katiba inamruhusu....lakini kama urais unaupata kwa kura...na kura za nchii hiii zimegawika baina ya wana dini wa 2 basi upande mmoja sio rahisi kumwamini....hakuna ushahidi ama hajawahi kuonesha kuwapo pamoja na waislam..kwenye sehemu zao ama hata kuwatakia salam tu za eid au ramadhan amejitenfa nao tangu amekua padri mpaka katika pirika zake za ki siasa....haoneshi kama ni kiongozi wa wote...



 
Mwizi wewe unayetaka mtu apate popularity isiyo na msingi wakati naye ni tatizo tu.Mbona alilamba marupurupu ya ubunge??Si alilalama yalikuwa makubwa??Angeyakata basi.

Kuna mapadri wangapi wameoa na wanaendelea na maisha yao kama kawaida, kuna mapadri wangapi wangapi bado wako kwenye service na wamezaa watoto mitaani licha ya kiapo unachokifagilia. Suala la kutumika katika kazi ya Bwana ni suala binafsi wala hakuna kifungu kwenye bible kinachokataza watu kuoa kwa ajili ya kumtumikia Mungu.

Siwezi kum judge mtu kupitia maisha yake binafsi. Huyo Mkwere anao watoto wangapi wa mtaani?and that doesn't bother me at all as long as He is doing job correctly! Wapo akina Zuma wa Afrika ya kusini, Bill clinton na Ronald Regan waliowahi kuhusishwa na masuala ya wanawake wakiwa madarakani, je hilo liliathiri ufani na utendaji wao kazi? La Hasha!

CCM wamekosa cha kumkosoa kuhusia na utendaji na record zake, wameanza ku-attack personal life! His record is clean and He has been consistent and with what He preaches despite of several attempts to bribe and silence Him.
Kinachoniumiza zadi ni watu kama nyie mnaodhani siku moja CCM iliyoshindwa kuleta maendeleo licha ya miaka 50 ya uhuru itakuja badilika! Never hilo sahau! Hakuja cha majaaliwa future is in your hand! Umeridhika na tunavyoibiwa sio? Nina kuhurumia! Si ajabu umeenda shule na uko wapi utashi wako wa kuuliza na kuhoji mambo yasiyoenda sawa! Cheo ni dhamana na nitakuwa tayari kumhoji yeyote atayeingia madarakani maana ni haki yangu ya msingi!
Endelea kusubiria majaaliwa!
 
Back
Top Bottom