Kwa nini hawamtaki gaddafi?

Masika

JF-Expert Member
Sep 18, 2009
723
30
Helo wana jf,
hivi kwa nini walibya hawamtaki huyu raisi wakati amefanya makubwa?
Mfano;
1:anatoa elimu bure,tofauti na nchi nyingi za afrika
2:anatoa huduma ya afya bure,hii ni kitendawili kwa nchi nyingi afrika
3:ana wajengea nyumba wanaotaka kuoana,wenye miaka 21...
4:anatoa mshahara kwa wasio na kazi
5:anaendesha nchi kama nyumba yake,wanataka nini cha ziada? Au ni kusema hawajajua waafrika wenzao wanavyoteseka?
Ama hawajui viongozi wengi wa afrika ni mafisadi na watu wasio jali raia wa nchi wanazoziongoza? Ama hizi taarifa za vyombo vya habari ni za uongo,nawakilisha tujadili
 
Wanachotaka ni demokrasia, kama misingi imara kashaweka kwa nini asipishe wengine waendeleze?
 
....

Hiyo namba tano kwenye red ndiyo tatizo kubwa. Nyumba yako ni nyumba yako na nchi (republic) ni nchi, na huu ndiyo ujinga unaojitokeza hapa home. Watoto wa rais kutaka waonekane kama marais wadogo. Ajenda ya Ghaddafi ni kuwaridhisha republic of Libya watoto wake, yaani kageuza natural resources za taifa kuwa mali yake wakati ni haki ya kila m-Libya na hivyo kusema anasomesha watu bure ni makosa, it is their God given rights kwani ni mafuta waliyopewa na Mungu walibya wote.
 
Pamoja na yote mazuri, bado haimpi uhalali wa yeye kukaa madarakani maisha yake yote. Akifa leo ina maana hayo mema yatakwisha!
Watu wanataka uhuru. Hawahitaji uongozi wa kurithishana kutoka kwa baba kwenda kwa mtoto.
Anasemaje kuhusu Palestina?
 
Shida ni kwamba amekaa muda mrefu na inasemekana anapendelea watu wa kabila lake otherwise kuna maendeleo sana Libya!
 
Hiyo namba tano kwenye red ndiyo tatizo kubwa. Nyumba yako ni nyumba yako na nchi (republic) ni nchi, na huu ndiyo ujinga unaojitokeza hapa home. Watoto wa rais kutaka waonekane kama marais wadogo. Ajenda ya Ghaddafi ni kuwaridhisha republic of Libya watoto wake, yaani kageuza natural resources za taifa kuwa mali yake wakati ni haki ya kila m-Libya na hivyo kusema anasomesha watu bure ni makosa, it is their God given rights kwani ni mafuta waliyopewa na Mungu walibya wote.

Umesema vyema lakini walipaswa kutumia njia nyingine tofauti na hiyo.
Inaelekea wanawaiga waarabu wenzao, mfano misri, lakini hali ya kisiasa miongoni mwa nchi za kiarabu ni tofauti. Mfano kwa nini hawakutumia viongozi wakuu wa umoja wa afrika ili wapeleke matakwa yao bila umwagaji wa damu au vyombo vingine ikishindikana ndo watumie njia mbadala?
 
Tatizo time.
 
Hata mimi nimejiuliza sana swali hilo maana walibya wanapata kila kitu bure. Gaddafi yuko radhi kupunguza bei ya bidhaa kutoka nje hata kama serikali imezinunua kwa bei ya juu, maana kwa kutumia mafuta waliyonayo wana uwezo wa kufanya hivyo. Jana nilifurahishwa na kipanya kwenye gazeti la Mwananchi kwenye katuni yake kulikuwa na maneno nanukuu: "IKIWA HATA LIBYA NA BAHRAIN WAMEANDAMA, MIMI NIFANYAEJE?" mwisho wa kunukuu. Yaani nchi alizozitaja wana utajiri na maisha mazuri na wanapata kila kitu, wanaandama, je sisi wadanganyika..............TAFAKARI, CHUKUA HATUA!!!
 
unajua watu wengi tunasahau kitu kimoja..unaweza kuwa unapata kila kitu lakini huna uhuru, tanzania tu maskini lakini angalau tuna ka-uhuru fulani kakuikosoa serikali, kupiga kura na access ya unfiltered information sasa wenzetu wa middle east na north africa mambo hayo hawana. Na wao wanataka kuila keki ya taifa uku wakipata uhuru kama wa wenzao wa nchi zilizoendelea.
 
Umesema vyema lakini walipaswa kutumia njia nyingine tofauti na hiyo.
Inaelekea wanawaiga waarabu wenzao, mfano misri, lakini hali ya kisiasa miongoni mwa nchi za kiarabu ni tofauti. Mfano kwa nini hawakutumia viongozi wakuu wa umoja wa afrika ili wapeleke matakwa yao bila umwagaji wa damu au vyombo vingine ikishindikana ndo watumie njia mbadala?

HIVI KWELI MIAKA 41 HAIMTOSHI MTU KUACHIA NGAZI NA KUWAPA WATU WENGINE WAONGOZE NCHI??
HIVI KWELI GADAFI NDIO RAIA PEKEE WA LIBYA ALIETEULIWA NA MUNGU KUIONGOZA HII NCHI MPAKA KUFA KWAKE?
HIVI KWELI WATOTO W RAIA WENGINE WA LIBYA HAWANA UWEZO WAKUONGOZA ILA WATOTOT WA GADAFI TUUU??
HIVI KWELI ASILIMIA 40 YA MALI YA LIBYA NI MALI YA FAMILIA YA GADAFI NA SIO YA WALIBYA???
HIVI NI KWELI KWAMBA GADAFI NDIE MWENYE MAMLAKA YA NANI WAMUUZIE MAFUTA NA NANI ASIUZIWE DUNIANI??
HIVI KWELI MAFUTA YA LIBYA YANAPELEKWA ULAYA NA NCHI NYINGINE ZA MAGHARIBI HALAFU WAO NDIO WANAOUZA KWA AFRIKA KWA SABABU AFRIKA INA NUKA NA HAINA FEDHA??

gadafi hafai aondoke,NAUNGA MKONO MAANDAMANO YA LIBYA NA NINAOMBA YAJE NA TANZANIA YAKITOKA LIBYA.
 
Mkuu inabidi utambue kwamba uhalali wa serikali yoyote duniani ni kukubalika kwake na wananchi. Ndiyo maana kuna msemo "Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu." Kama wananchi hawa kutaki ni hawa kutaki haijalishi wana sababu gani au wewe ume wafanyia nini. Kwa hiyo kwa Libya wananchi wameamua wenyewe kutaka mabadiliko whether it is for better or for worse sisi tusio Walibya haituhusu.

Ila pia tambua kwamba kukaa madarakani muda mrefu kuna effects kadhaa

Fatigue- Watu kukuchoka. Kitu chochote kikiwepo kwa muda mrefu kina chosha. That is a fact of life. Kwa hiyo bila kosa lolote kitendo cha kukaa muda mrefu tu kina wachosha watu. Ndiyo maana mtu kama Mwl Nyerere aliye pendwa na wengi pamoja na kwamba ange weza kuwa raisi wa maisha ali tambua kwamba akiendelea kuwepo madarakani zaidi watu wange mchoka na inge tia dosari legacy yake.

Elitism- Kuwepo madarakani muda mrefu kuna jenga hali ya kuwa "elitist". Kwa maana una jenga mfumo wa watu wachache kuweza kushika madaraka. Sikiliza taarifa za habari uta sikia kwamba Ghadafi kadumu muda wote huu kwa kuweka karibu wafanya biashara wakubwa, viongozi wakuu wa usalama na wakuu wa makabila. Hii ina maanisha kwamba kuna kundi la watu wachache walikua wana faidika. Uki create hali hii mwananchi wa kawaida anaanza kuona kwamba hata aji tume vipi hawezi kufika mbali kwa sababu nchi ina "wenyewe."

New generation- In nature vijana ni ambitious. Hata watu wa rika kubwa nao ni ambitious lakini haswa vijana zaidi. Je una dhani hamna vijana ambao wange tamani na wao kuja kuwa raisi wa Libya? Wao wanaona wana zibiwa na kunyimwa haki. Kumbuka si yeye tu anaye penda huo uraisi. Wale ambao wanashindwa kuupata kwa sababu yake lazima watake opportunity ya kumuondoa.

My take: Ni maajabu sana kwamba kaweza kudumu muda wote huu. Madikteta wengi huja ribu kuzuga kwa kuweka visheria vya kiini macho ili wananchi wajihisi wana maamuzi. Ila Libya haina katiba wala Bunge. It is the most extreme case of rule by a strong man. Sasa nchi bila katiba na Bunge una tegemea nini? Kila raisi anacho ota ndotoni akiamka ana weza kukifanya.
 
mkuu mbona mwalimu aliweka misingi bora akawapisha wenzake, matokeo ni madowans, epa badala ya demikrasia

Mkuu una ongea kana kwamba hamna kifo. na ndiyo mawazo ya watu wanao jiona ni wao tu wanaoweza kushika madaraka. Mtu ana jiona bila yeye nchi hamna huku ana sahau siku ata kufa tu na itabidi uongozi uende mikononi mwa mwingine. Cycle of life is part of nature. Change is part of life. Matokeo ya Dowans na EPA si kwa sababu Nyerere aliachia madaraka bali ni kwa sababu sisi tumeachia nchi iende kwa wahuni. Hata Nyerere ange baki madarakani si leo hii ange kua marehemu tu? Je una dhani ni wakina nani wange rithi hayo madaraka? Si hawa hawa tulio nao sasa?
 
Wanachotaka ni demokrasia, kama misingi imara kashaweka kwa nini asipishe wengine waendeleze?

Hakuna cha misingi imara Libya. Misingi imara ni kuwa na institutions. Kwa maana nafasi muhimu za nchi kama uraisi nk zina kuwa ni taasisi na si mtu. Kama una fuatilia mambo Libya hamna katiba wala chombo cha uwakilishi sasa ni misingi ipi hiyo una dhani ata kuwa kaweka?
 
Umesema vyema lakini walipaswa kutumia njia nyingine tofauti na hiyo.
Inaelekea wanawaiga waarabu wenzao, mfano misri, lakini hali ya kisiasa miongoni mwa nchi za kiarabu ni tofauti. Mfano kwa nini hawakutumia viongozi wakuu wa umoja wa afrika ili wapeleke matakwa yao bila umwagaji wa damu au vyombo vingine ikishindikana ndo watumie njia mbadala?

Njia ipi tena na wakati mtu hataki kutoka madarakani? Watu wanaandamana kumpiga leo Al Jazeera katishia kuwa lipua. Sasa mtu kama huyo ni mtu ambae ana weza kuondoka kwa njia yoyote nyingine? Be realistic. Mtu hata kwa nguvu hataki kutoka kwa kuongea nae ndiyo ataondoka? Serikali yoyote ni ya wananchi kama wananchi hawa mtaki basi nothing else matters including your personal opinion regarding the matter.
 
unajua watu wengi tunasahau kitu kimoja..unaweza kuwa unapata kila kitu lakini huna uhuru, tanzania tu maskini lakini angalau tuna ka-uhuru fulani kakuikosoa serikali, kupiga kura na access ya unfiltered information sasa wenzetu wa middle east na north africa mambo hayo hawana. Na wao wanataka kuila keki ya taifa uku wakipata uhuru kama wa wenzao wa nchi zilizoendelea.

Tanzania uhuru wetu ni theoretical not realistic. Una weza ukadhani una uhuru lakini hauna. Ngoja nikupe scenarios mbili na uniambia kwenye scenario ipi unaona uhuru.

Nchi A hakuna ruhusa kupinga wala kuisema vibaya serikali. Vyombo vya habari vipo censored nk.

Nchi B watu mna ruhusiwa kuongea ila maoni yenu hayana madhara yoyote na mnaishia tu kuongea ila hamna naesikiliza.

In theory nchi B ina uhuru kwa vile ina ruhusiwa kuongea ila in reality uhuru upo?
 
Umesema vyema lakini walipaswa kutumia njia nyingine tofauti na hiyo.
Inaelekea wanawaiga waarabu wenzao, mfano misri, lakini hali ya kisiasa miongoni mwa nchi za kiarabu ni tofauti. Mfano kwa nini hawakutumia viongozi wakuu wa umoja wa afrika ili wapeleke matakwa yao bila umwagaji wa damu au vyombo vingine ikishindikana ndo watumie njia mbadala?

mkuu hivi nani katika AU anaweza kumshawishi Gaddafi vinginevyo? na Hebu jiulize, Ghaddafi amekuwa kwenye power for 42 years, is this fair ikiwa yeye alipindua kwa kuona kuwa utawala si wa familia moja tu, kwa nini yeye ang'ang'anie na kuanza mipango ya kumrithisha mwanaye?

Pia ujue kuwa Ghaddafi si mtu anayependa democrasia ya uchaguzi. Aliwahi kumshawishi either Mugabe au Mseveni kuwa asing'atuke wala kukubali kuondolewa kwenye uraisi kwani aliyomweka madarakani si masanduku ya kura.
 
Back
Top Bottom