Kwa nini bando la internet ya Zantel linachelewa kuisha kulinganisha na mitandao mingine?

Ally780

Member
Aug 8, 2021
23
22
Habari wadau,

Mm Nina simu kubwa mbili ambazo natumia laini tatu za mitandao tafauti Zazntel,Vodacom na halotel.

Laini hizo zote nazitumia kwa matuizi ya internet ambapo Mara nyingi huaga naweka salio la 1000 kwa kila laini lakini nilichogundua bando la zantel Mara zote huaga linachelewa kuisha kulingana na mitandao mingine.

Kwa mfano halotel unapata GB 1 kwa buku na zantel unapata 750MB tu kwa buku hiyo hiyo. Lakini ukiangalia movie ya Aina moja YouTube unakuta halotel GB1 zinawah kuisha.

kuliko 750mb zantel.

Nimefanya hivyo Mara kadhaa lakini matokeo hayatafautiani na hata Voda pia Ni Kama halotel tu.

Naomba ufafanuz juu ya Hilo Kama wapo wanaujua.
 
Kwasababu network yake ipo chini kuliko washindani wenzake... Network ikiwa vizuri kwa teja wa mtandao lazima aone kama anaibiwa
 
Kwasababu network yake ipo chini kuliko washindani wenzake... Network ikiwa vizuri kwa teja wa mtandao lazima aone kama anaibiwa
Kwani kama movie ina GB 500 halafu network ikawa chini lakini nikawa nimeangalia movie yote,hizo GB 500 zinakuwa hazijaisha?
 
Ok,kwa hiyo tukubaliane kuwa internet kuwa slow siyo kigezo siyo?
Ni kigezo kwa mfano, kama internet yako ina speed nzuri ukiplay video ya dakika 10 online alafu wewe ukaangalia dakika 2 ukacancel, kitakachotokea utahesabiwa umeplay video yote hivyo kujikuta umetumia mfano MB 50 kwa kutazama nusu kipande cha MB 10
Screenshot_20210828-090403.png

Ukicheki screenshot niliyoweka utaona sehemu nilipopigia mstari wa kijani ni sehemu ya video uliyotazama huku mstari mwekundu ukionesha ni sehemu ya video uliyolipia tayari japo hujaitazama bado....
Hivyo mtu unapokuwa unatumia kifaa chenye kasi nzuri ya Internet ndivyo hivyo kifurushi chako kinaisha mapema kutokana na background ya baadhi ya apps zilizo kwenye kifaa chako

Mfano kuna watu hawajui kuseti simu zao zisiwe zinadownload vitu bila ridhaa zao hivyo wanaweza kuweka kifurushi cha buku, wakiwasha data tu wanaona simu zao zinakuwa nzito sababu zinajipakulia vitu mitandaoni hovyohovyo na baada ya muda mfupi wanatumiwa meseji kuwa kifurushi kimeisha huku wakiwa hawajui kimeisha vipi kumbe unakuta hawajaviwekea mipaka vifaa vyao
 
Ni kigezo kwa mfano, kama internet yako ina speed nzuri ukiplay video ya dakika 10 online alafu wewe ukaangalia dakika 2 ukacancel, kitakachotokea utahesabiwa umeplay video yote hivyo kujikuta umetumia mfano MB 50 kwa kutazama nusu kipande cha MB 10View attachment 1912044

Ukicheki screenshot niliyoweka utaona sehemu nilipopigia mstari wa kijani ni sehemu ya video uliyotazama huku mstari mwekundu ukionesha ni sehemu ya video uliyolipia tayari japo hujaitazama bado....
Hivyo mtu unapokuwa unatumia kifaa chenye kasi nzuri ya Internet ndivyo hivyo kifurushi chako kinaisha mapema kutokana na background ya baadhi ya apps zilizo kwenye kifaa chako

Mfano kuna watu hawajui kuseti simu zao zisiwe zinadownload vitu bila ridhaa zao hivyo wanaweza kuweka kifurushi cha buku, wakiwasha data tu wanaona simu zao zinakuwa nzito sababu zinajipakulia vitu mitandaoni hovyohovyo na baada ya muda mfupi wanatumiwa meseji kuwa kifurushi kimeisha huku wakiwa hawajui kimeisha vipi kumbe unakuta hawajaviwekea mipaka vifaa vyao
Shukrani sana,nimeelewa sasa.
 
Back
Top Bottom