KWA MTINDO HUU MASHIRIKA HAYAWEZI KUWA NA TIJA - TTCL yaitaka serikali ilipe deni

Ustaadh

JF-Expert Member
Oct 25, 2009
413
19
KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL), imeitaka serikali iilipe deni lake la Sh 7.2 bilioni linalotokana na gharama za matumizi ya huduma simu katika ofisi zake.

Mkurugenzi wa kampuni hiyo, alisema jana kuwa kutolipwa kwa deni hilo na ya wateja wengine, kunaifanya TTCL, kushindwa kujiendesha kibiashara.Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo aliyekuwa akizungumza mbele ya Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa, kampuni inahitaji Sh322 bilioni ili iweze kujiendesha kwa faida.
Said alisema kwa sasa, TTCL imekuwa ikifanya shughuli zake chini ya viwango kwa sababu ya madeni sugu ambayo wateja wake, ikiwemo serikali, hawajalipa.
"TTCL ina uwezo wa kufanya kazi na kuzizidi kampuni zingine za simu haopa nchini, lakini inakabiliwa na tatizo ukosefu mkubwa wa fedha," alisema Mkurugenzi huyo.

Alisema kama TTCL itapata Sh322 bilioni, itakuwa katika nafasi nzuri ya kutekeleza mipango yake kikamilifu na kwa kutumia teknolojia za kisasa katika mawasiliano.

Kwa upande wake, Profesa Mbarawa alisema mazungumzo yake na viongozi wa TTCL, yalilenga katika kufahamiana na kujua matatizo yanayoikabili kampuni hiyo kongwe ya simu nchini.
"TTCL ina matatizo mengi lakini mpango kazi wa serikali ni kurekebisha mapungufu yaliyopo katika taasisi zake mbalimbali.Hapa tatizo kubwa ni la mtaji na malimbizo ya madeni," alisema.

My take: MASHIRIKA YAENDESHWE KIBIASHARA NA SERIKALI PAMOJA NA WATEJA WANAODAIWA WALIPE MADENI. HII TABIA YA MASHIRIKA KUENDESHWA KIKOMUNISTI IACHWE MARA MOJA. KILA SIKU TUNASIKIA WIMBO WA UBINAFSISHAJI LAKINI HAKUNA TIJA YOYOTE.
 
Serikali kwa serikali wanaoneana haya kudaiana unaweza kuta ata TANESCO hayo hayo
 
Hizo ni dalili za kufa kwa shirika hili muhimu. Kiasi hicho cha fedha kinaweza kupatikana lakini ndo hivyo serikali yetu haina utashi wa kufanya hivyo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom