Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 50,956
- 22,149
[h=3]Kwa moyo wote!
[/h]
Sababu za kuwa na migogoro kati ya mume na mke mara nyingi ni kwa sababu wanaume hawawaelewi kabisa wanawake (dont understand) na wanawake wanawaelewa vibaya wanaume (misunderstand).
Kibaya zaidi wanaume mara zote huendelea kufanya kinyume na vile wanawake wanategemea wawafanyiwe na waume zao.
Na wanaume nao wanawashangaa wanawake namna wanavyobadilika kila mara kwani unaweza kumkuta mke dakika moja yupo na furaha na kicheko na baadae kidogo anajikunyata na kuhuzunika na wanaume huwaona wanawake ni viumbe wa ajabu sana chini ya jua.
Linapokuja suala la kutafuta mpenzi (mume mtarajiwa) wanawake wanatabia ya kumkubali na kumshika mwanaume mzima mzima. Na hutumia akili kuhakikisha anamnasa hata kwa kujipitisha sehemu au njia ambazo anaamini anaweza kukutana naye.
Kama anajua mwanaume yule hupatikana maeneo fulani na anampenda basi hujipeleka hilo eneo ili wakutane ili iwe coincidence fulani.
Atasubiri hako kanafasi ili wakutane ghafla.
Mwanamke hutumia njia ya hisia anapoingia kwenye suala la mapenzi na kuwa karibu na kifua chake (moyo) si mwonekano kama wanavyofanya wanaume.
Kawaida mwanaume huchelewa sana kufungua moyo kwa mwanaume na akishaufungua huufungua kwa asilimia 100 na akimpenda huyo mwanaume (fall in love) basi huwekeza kila kitu maishani mwake kwa ajili ya