Kwa mlio na matarajio makubwa kwa TLS ya Tundu Lissu, waulizeni wana Ikungi

Mjadala wangu unawalenga wale wanaomshangilia leo Tundu Lissu kwa kuamini kuwa TLS itashindana na Serikali
Sasa swali ni kwa nini serikali hio ilikua inahaha jamaa asigombee wala kuchaguliwa kama hawezi ifanya kitu serikali...
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Awali ya yote, napenda kuwapongeza wanachama wa TLS kwa kufanikisha mkutano mkuu na uchaguzi wa viongozi wao. Demokrasia imetawala na aliyeshinda kashinda kwa sababu amepata kura za kuwazidi wenzake. Haina maana kuwa yeye ni bora zaidi ya wenzake. Kikubwa zaidi ni kuwaomba viongozi wapya watekeleze yale waliyoahidi ili kutimiza lengo.

Nawahurumia sana wale wenye matarajio makubwa kwa TLS ya Tundu Lissu. Niwahakikishie kuwa baada ya mwezi mmoja, mtakuwa mmesahau nafasi ya hiyo taasisi katika jamii. Anayechaguliwa leo kwa mbwembwe kesho mtamguna na kumlalamikia kwa upendeleo wa dhati kwa chama chake. akiendekeza mahaba ya chadema na kusahau kuwa chombo hicho kipo kwa maslahi ya watu wa itikadi tofauti za kisiasa basi ajiandae kurushiwa virago mapema.

Jimboni kwake wanalalamika kila uchwao kutokana na nyodo na dharau zake kwa wananchi. Hakuna la maana analofanya zaidi ya kulalamika na kulia lia bungeni. Tumtakie kila la kheri katika uongozi wake ila akumbuke kuwa mtoto hakui kwa mama.
Na tulio na matalajio makubwa kwa makonda tufanyeje?
 
mm ni mkaz wa dun'unyi yanayosemwa apo ni kweli akuna ubishi
Waukhaya hawa watu wa Dar hawajui yanayojiri huku wao wanafurahia kuona jamaa anakomaza upinzan ambalo c jambo baya ila angalia kwetu tunavomsikia tu redioni hatujafaidika hata kuongezwa mhudumu pale mwisi dispensary
 
Hahahahahaaaaa! Kwa sasa wanajuuutaaaa kumchagua mtu asiyejua maana ya maendeleo
Na CCM iliyoongoza tangu 1977 (tangu 1961 ikiwa Former TANU + ASP) mpaka leo maadui badala ya kupungua/kuisha ndi wanaongezeka inajua maana ya maendeleo?
 
Ikungi ipi unayoizungumzia wewe? Acha uchawi,Jimbo limekaa kwa maccm miaka yote hakuna cha maana leo unasema hajafanya lolote, kwa taarifa yako, huku mpaka achoke mwenyewe,Mbunge wetu anatutetea sana,isingekuwa huyu Lisu tungenyang'anywa ardhi yetu kibabe kule sehemu ya kuchimba madini ya dhahabu Londoni na kampuni ya kitapeli ya ccm, sasa hivi hatuonewi hovyo na mgambo,watoto wanakaa chini? Acha uzuzu kwenu mbona kila mitihani wanashika mkia vipi wao wanakaa kwenye maji? Lisu kafanya mengi jimboni nyie nzi wa kijani endeleeni kupiga kelele na 2020 tunamchagua tena kwa hasira
Kweli we wasingida wengine wanajifanya waikungi ili waongee mbovu jina lako tu we wa singida
 
Lisbon acha ujinga CCM mlikuwa mnakula kula kuku za Wanayaturu jimboni mwa TL kabla hajawa Mbunge kwa kuwakata watu ovyo na kuwapiga faini.

Leo hii kuna utulivu jimbo la Singida Mashariki halafu unaleta uongo.
CCM ndio watalia maana mlizoea kuweka Rais wa TLS mwenye kutii kila kitu hata jambo lenye kuleta madhara kwa WANANCHI.
 
Ukisikia majungu ya kiwango cha rami ndoo haya
Ajabu ni pale Lizaboni ameshindwa kulitaja Jina la mshindi wa nafasi ya Urais wa TLS katika aya ya KWANZA ya bandiko lake. Hii ni sawa na Gazeti la Mzalendo (Machi 19, 2017), liliposhindwa KABISA kutangaza habari za uchaguzi wa TLS!
 
Demokrasia imetawala na aliyeshinda kashinda kwa sababu amepata kura za kuwazidi wenzake. Haina maana kuwa yeye ni bora zaidi ya wenzake. Kikubwa zaidi ni kuwaomba viongozi wapya watekeleze yale waliyoahidi ili kutimiza lengo.

Alieshinda kwa kura nyingi ndio mshindi???
Sasa mbona nyie huwa mnasema alietangazwa na tume ya uchaguzi ndio mshindi???
Kwa nini siku ile hamkumtangaza aliepata kura nyingi mkakubaliana na alietangazwa na NEC
 
Waukhaya hawa watu wa Dar hawajui yanayojiri huku wao wanafurahia kuona jamaa anakomaza upinzan ambalo c jambo baya ila angalia kwetu tunavomsikia tu redioni hatujafaidika hata kuongezwa mhudumu pale mwisi dispensary

yaan awajui tuu mwaka huu billa kuwa na mizizi acngepata ubunge
 
Asiyeunga mkono juhudi za kuwatetea watanzania wenzetu walioko huko magerezani bila sababu na chama kinapata pesa nyingi kutoka kwa donor basi ana tatizo la akili.
 
Back
Top Bottom