Kwa Mlinganisho huu wa Meli, Bandari ya Dar kuna giza nene

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
Mlinganisho wa meli zilizotia nanga, na zinazotarajia kutia nanga bandari za Durban, Mombasa na Dar es Salaam.

Nashauri Serikali ikae chini itafakari na inapobidi itumie Ushauri wa CHADEMA iliyoutoa Bungeni. Huwezi acha kutumia mawazo ya Wapinzani kwa manufaa ya Nchi kisa tu ni wapinzani wako kisiasa.

Ni aibu sana kwa Bandari iliyokuwa inaingiza meli zaidi ya 40 kwa Siku iingize meli 8 tu.
uploadfromtaptalk1473059574284.jpeg
uploadfromtaptalk1473059581528.jpeg
uploadfromtaptalk1473059587458.jpeg


Tujikumbushe Hotuba ya Kambi ya Upinzani. Wakati akisoma hotuba hii, Msomaji wa Hotuba wa Kambi ya Upinzani, alidai
8. MWENENDO WA MAPATO YA NDANI NA MKANGANYIKO WA TAARIFA ZA SERIKALI YA HAPA KAZI TU
Mheshimiwa Spika, Katika mwaka huu wa fedha, na hususan miezi ya karibuni mwenendo wa mapato umekuwa sio wa kuridhisha sana! Kodi ya ushuru wa forodha haikufikia lengo na kwa kadiri siku zinavyozidi kwenda hali inazidi kuwa mbaya! Idadi ya meli zilizohudumiwa Januari - Aprili 2015 (TPA- Kontena) zilikuwa 41 ukilinganisha na meli 16 tu zilizohudumiwa Januari- Aprili 2016. Pungufu ya meli 25, badiliko la -61%. Halikadhalika kwa Meli ya Mzigo Mchanganyiko ‘General Cargo’ meli zilizohudumiwa Jan- April 2015 zilikuwa 53 ukilinganisha na meli zilizohudumiwa Jan – April 2016 ambazo ni 33 tu. Pungufu ya meli 20 sawa na badiliko la -37%

Mheshimiwa Spika, Maelezo ya waziri wa fedha na Mipango kwenye kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2015/16 kwa kipindi cha Julai 2015 hadi Machi 2016 na mwelekeo hadi juni 201612 anaeleza sababu za upungufu kuwa ni ;
i) kupungua kwa uingizaji wa mizigo kutoka nje kutokana na hofu ya wafanya biashara katika kipindi cha uchaguzi
ii) Udanganyifu uliokuwa unafanywa na wafanyabiashara kwa kukwepa kodi ya ushuru wa forodha kwa bidhaa zinazopitia bandarini
iii) kushuka kwa bei ya bidhaa katika soko la dunia
iv) Na kwa upande wa kodi ya ongezeko la thamani upungufu umetokana na marejesho ya VAT (VAT inputs) kuwa kubwa kutokana na uwekezaji katika viwanda vya sementi pamoja na kupungua kwa mahitaji.
v) Halikadhalika tatizo la kutoa/kuomba risiti za kielekroniki katika huduma mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, Wakati wizara ya fedha ikitoa visingizio tajwa hapo juu, Mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania katika maelezo yake ya Takwimu za uingizaji mizigo katika Bandari ya Dar es salaam kwa kipindi cha 2013-2015 na kipindi cha Jan- April 2016 inaeleza sababu zilizopelekea kupungua kwa shehena ya mizigo kuwa ni:

i) Kudorora kwa uchumi wa china (Hii imeleta madhara katika bandari nyingi duniani)

ii) Hofu ya wateja kutokana na kuanzishwa kwa sheria ya VAT katika huduma zinazotolewa na mawakala kwenye mizigo ya nchi jirani (VAT on Transit GOODS) ambayo ni kinyume na sheria za kimataifa

iii) Tatizo la Single customs Territory. Mizigo inayopatikana kwa mfumo wa single customs territory unatozwa kodi kwa asilimia 100%, baadhi ya wafanyabiashara wanaona kupitisha mizigo Tanzania ni gharama kubwa.

iv) Kushuka kwa bei ya shaba duniani kumesababisha migodi mingi nchini Zambia na DRC kufungwa na hata ile inayofanya kazi uzalishaji umepungua.

v) Tozo la barabara (Road tolls) USD 16 kwa KM 100 hapa Tanzania ulikilinganisha na USD 8 kwa kila KM 100 zinazotozwa kwa nchi nyingine kwa magari yenye ekseli zaidi ya mbili.

vi) Muda mfupi (Short grace period) kwa mzigo wa mafuta wa nchi jirani. Tanzania ni siku 30 mzigo unatakiwa uwe umesafirishwa kabla ya kuwa localised tofauti na nchi nyingine ambazo zinawapa siku 60 hadi 70.

vii) Kuongezeka kwa Tozo kutokana na “Government Chemical Agencies” kutoza USD 1.00 kwa Tani badala ya USD 100 kwa “ Bill of Lading” kwa bidhaa ambazo wanazikagua kama vile mbolea hivyo kuongezeka kutoka wastani wa USD 500 hadi USD 20,000 au Zaidi kutokana na ukubwa wa mzigo.

viii) Mfumo wa TANCIS wa TRA kutoruhusu kugawanywa kwa “Bill of Landing” ili kuruhusu kutoa mizigo ambayo haina tatizo panapokuwa na tatizo la mzigo mmoja badala ya mzigo wote kuzuiwa na kusababisha gharama za tozo za hifadhi kwa mteja ambazo sio lazima.
Mheshimiwa spika, Ni aibu kubwa, kwa vyombo viwili vya serikali kuzungumza lugha tofauti katika suala moja! Hiki ni kiashiria kwamba ama serikali hii haifanyi kazi kama timu…ama waziri wa fedha amedhamiria kulipotosha Bunge kwa kutoa sababu nyepesi huku zile za msingi akiziweka kibindoni (sijui kwa manufaa ya nani).

Kambi rasmi ya upinzani inaitaka Serikali ya CCM na Magufuli kutambua kwamba Tanzania sio kisiwa na kwamba Bandari ya Dar es salaam inakabiliwa na ushindani kutoka kwenye bandari za Mombasa (Kenya), Beira,Nacala na Maputo (Msumbiji) , Durban (Afrika KUSINI

Hata Hizo zzinazotarajiwa leo ni viporo tu, kihalisia, leo hakuna meli hata moja inatakiwa kuingia.
tpa.png
 
Mlinganisho wa meli zilizotia nanga, na zinazotarajia kutia nanga bandari za Durban, Mombasa na Dar es Salaam leo.

Nashauri Serikali ikae chini itafakari na inapobidi itumie Ushauri wa CHADEMA iliyoutoa Bungeni. Huwezi acha kutumia mawazo ya Wapinzani kwa manufaa ya Nchi kisa tu ni wapinzani wako kisiasa.

Ni aibu sana kwa Bandari iliyokuwa inaingiza meli zaidi ya 40 kwa Siku
View attachment 393890View attachment 393891View attachment 393892
Uchumi wa hizo nchi unajieleza
 
Hii ilivyo haitoi picha kamili. Utajuaje kama tangu zamani uwiano ulikuwa ni huu au la? Ilitakiwa kuwe na ulinganifu lbd mwaka jana kipindi kama hiki na sasa hali ikoje
Umeandika nilichokuwa nawaza tatizo Tanzania tulichezea sana tasnia ya Habari asilimia kubwa ya waandishi wa Habari na watangazaji wa redio Tanzania ni makanjanja, yaani ukisikiliza wanavyopanga hoja zao au wanachoandika ni hatari tupu
 
Hii ilivyo haitoi picha kamili. Utajuaje kama tangu zamani uwiano ulikuwa ni huu au la? Ilitakiwa kuwe na ulinganifu lbd mwaka jana kipindi kama hiki na sasa hali ikoje
Ubishi bwana ni mzuri , kwani Bandari wamesemaje?tumekosea tujirekebishe
 
Aibu na hasara ipo wapi!! Katika Kuingiza meli Zaidi ya 40 za wapigaji wasiolipa kodi na ushuru stahiki serikalini au kuingiza meli chini ya 20 kwa siku zinazolipa kodi na ushuru stahiki???....TRA imeshatangaza kuwa mapato kutokana na kodi bandari ya Dar es salaam kwa mwezi Augost yameongezeka mara dufu, licha ya kupungua kwa mizigo, hadi kufikia Zaidi shilingi trilioni 1.158, ikivuka lengo la kukusanya sh. trilioni 1.152, ambapo mwezi kama huo mwaka jana TRA ilikusanya shilingi bilioni 923 tu.

Ukweli mchungu usiowapendeza baadhi ya watu ni kuwa serikali imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwadhibiti wapigaji na mafisadi kuitumia bandari kama shamba la bibi; na hao ndio wanaosita kutumia bandari hivi sasa!
 
Kwanini umeleta taarifa za uongo ndugu yangu? Watu mnapenda sana kuonesha serikali imeshindwa sijui mnapata faida gani kukaa na kutunga uongo. Wewe hzo expected vessel 8 umezitoa wapi? na ni bandari ipi ilikua inaingiza meli 40 kwa siku? kwanini unakua muongo na wenzio wanakushangilia. Ni kweli vessel zimepungua bandarini lakini sio kwa takwimu zako hzo zakupika.
Mwezi huu expected vessel sio 8 ziko vessel zaidi ya 30 zinatarajiwa kutia nanga na muache ushabiki maandazi wenu. kwenye ukweli wekeni ukweli muache kuchafua serikali ya CCM.

Mwenyekiti CCM JF
 
Back
Top Bottom