Kwa Miaka 2, Rais Samia amepaisha Bajeti ya Barabara Vijijini Chini ya TARURA Mara 5 kutoka Bilioni 272 mwaka 2020/21 Hadi Trilioni 1.2 Mwaka 2023/24

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,115
49,835
Nawakumbusha tuu Machadema na Haters wengine kwamba Rais Samia ni geneous wa Masuala ya Uongozi.

Huyu ndio Rais anayefikiria kimkakati Kwa kutambua kwamba 70% ya Watanzania wote wanaishi Vijijini na kazi Yako kubwa takribani 65% wanategemea Kilimo tena peasantry farming huko 85% ya Ajira zote Tanzania zinatokana na shughuli za Kilimo.

Wakati anachukua madaraka mwaka 2021 alikuta Bajeti ya TARURA ya mwaka mzima ni Bilioni 272 tuu na hali ya Barabara za Vijijini zilikuwa mbaya na hazipitiki.Lakini miaka 2 na ushee Ameipaisha Bejeti kutoka Bil.272 Hadi Trilioni 1.2 mwaka huu..

Kwa wale wanaosafiri Vijijini watakuwa ni mashahidi wa jinsi Vijiji sana vinafikika Kila Kona na ndio maana hakuna mwanakijiji Kwa Sasa utamlalia bei maana Wanunuzi wanafuata mazao huko huko Vijijini..

Kwa mwendo huu niwakumbuehe Chadomo na Sukuma gang kwamba kura zoote za Vijijini ni za Samia na ndio maana hutokaa usikie kelele za shida ya Barabara kama ilivyokuwepo hapo miaka ya nyuma..

Hii ni sekta Moja tuu ya Barabara ila Hali Iko hivyo sekta zoote za Uchumi.

My Take
Hakuna Rais aliyewahi ku deliver mambo makubwa Kwa mda mfupi kama Rais Samia.Buyu Rais aendelee kugombea Hadi achoke mwenyewe maana ataleta Mageuzi makubwa sana.

====
TARURA KUTUMIA TILIONI 1.2 KUBORESHA BARABARA VIJIJINI NA MIJINI

Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) unatarajia kutumia Shilingi Tilioni 1.2 kwa mwaka wa fedha 2023/24 katika kuboresha barabara za vijijini na mijini zenye urefu wa Km 144,429.77 ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya usafiri na usafirishaji kwa urahisi.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Angellah Kairuki wakati wa hafla ya kukabidhi magari kwa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) iliyofanyika katika Ofisi za TARURA Makao Makuu katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.

Mhe. Kairuki amesisitiza kuwa Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kuboresha miundombinu ya barabara za vijijini na mijini kupitia TARURA ili kuhakikisha wananchi wanasafiri kwa urahisi.

’’Serikali ya awamu ya sita imedhamiria kuwezesha wananchi kuwa kitovu cha maendeleo na kuimarisha ubia baina ya wananchi na Serikali, katika ngazi ya msingi kwa kuimarisha miundombinu ya barabara kupitia TARURA na kwa kufanya hivyo, Bajeti ya TARURA imeongezeka hadi kufikia tilioni 1.2 kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ambapo pia leo tunakabidhi magari yatakayosaidia katika usimamizi wa miradi ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati’’, amesema Mhe. Kairuki .

Aidha, Mhe. Kairuki ametoa pongezi kwa Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor H. Seff pamoja na watumishi wote wa TARURA kwa usimamizi bora wa miradi katika maeneo mbalimbali nchini.

Akitoa taarifa fupi ya utekelezaji wa kazi za ujenzi na matengenezo ya barabara za Wilaya hadi kufikia tarehe 30 Juni 2023 Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor H. Seff ameeleza kuwa utekelezaji wa kazi umefikia asilimia 85 ambapo jumla ya Shillingi Bilioni 621 zimetumika kati ya Shillingi Billioni 653 zilizopokelewa.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Dennis Londo ameipongeza TARURA kwa kazi zinazofanyika katika kuimarisha miundombinu ya barabara na kwamba kazi hizo zinaonekana katika maeneo mbalimbali ya nchi.
 
Hiyo bajeti imejumuisha na pesa za misaada?!
Tupo kwenye Pd wodi ikae sawa kwanza usihamishe gori. waongeaji ni Watanganyika sio sio chadema
 
Hiyo bajeti imejumuisha na pesa za misaada?!
Tupo kwenye Pd wodi ikae sawa kwanza usihamishe gori. mie sio chadema
Ona jinga hili,Misaada ya wapi wewe nyumbu? Tufanye ni misaada swali la msingi hiyo misaada Kwa nini haikutolewa awamu zilizotangulia hasa awamu ya 5?

Kwa hiyo Wazungu Wana hela za kuchezea za kukupa wewe Msaada Kila siku au siyo? 😁😁
 
Nawakumbusha tuu Machadema na Haters wengine kwamba Rais Samia ni generous wa Masuala ya Uongozi..

Wakati anachukua madaraka mwaka 2021 alikuta Bajeti ya TARURA ya mwaka mzima ni Bilioni 272 tuu na hali ya Barabara za Vijijini zilikuwa mbaya na hazipitiki.Lakini miaka 2 na ushee Ameipaisha Bejeti kutoka Bil.272 Hadi Trilioni 1.2 mwaka huu..

Kwa wale wanaosafiri Vijijini watakuwa ni mashahidi wa jinsi Vijiji sana vinafikika Kila Kona na ndio maana hakuna mwanakijiji Kwa Sasa utamlalia bei maana Wanunuzi wanafuata mazao huko huko Vijijini..

Kwa mwendo huu niwakumbuehe Chadomo na Sukuma gang kwamba kura zoote za Vijijini ni za Samia na ndio maana hutokaa usikie kelele za shida ya Barabara kama ilivyokuwepo hapo miaka ya nyuma..

Hii ni sekta Moja tuu ya Barabara ila Hali Iko hivyo sekta zoote za Uchumi.

My Take
Hakuna Rais aliyewahi ku deliver mambo makubwa Kwa mda mfupi kama Rais Samia.Buyu Rais aendelee kugombea Hadi achoke mwenyewe maana ataleta Mageuzi makubwa sana.

Hii mikataba ya kugawa misitu, bandari na kadhalika pia ni sehemu ya mafanikio yake
 
Ona jinga hili,Misaada ya wapi wewe nyumbu? Tufanye ni misaada swali la msingi hiyo misaada Kwa nini haikutolewa awamu zilizotangulia hasa awamu ya 5?

Kwa hiyo Wazungu Wana hela za kuchezea za kukupa wewe Msaada Kila siku au siyo? 😁😁

misaada =mikopo awamu ya 5 ilikuwepo mingi sema mlituficha
 
Tunazungumzia awamu ya 6,acha kuropoka Samia hana wa kumlinganisha Kiongozi Tanzania hii..

Lini Tanzania iliacha kupata mikopo na misaada mbona hatukuwahi kuona Bajeti za kutengeneza Barabara Vijijini?
 
Nawakumbusha tuu Machadema na Haters wengine kwamba Rais Samia ni generous wa Masuala ya Uongozi..

Wakati anachukua madaraka mwaka 2021 alikuta Bajeti ya TARURA ya mwaka mzima ni Bilioni 272 tuu na hali ya Barabara za Vijijini zilikuwa mbaya na hazipitiki.Lakini miaka 2 na ushee Ameipaisha Bejeti kutoka Bil.272 Hadi Trilioni 1.2 mwaka huu..

Kwa wale wanaosafiri Vijijini watakuwa ni mashahidi wa jinsi Vijiji sana vinafikika Kila Kona na ndio maana hakuna mwanakijiji Kwa Sasa utamlalia bei maana Wanunuzi wanafuata mazao huko huko Vijijini..

Kwa mwendo huu niwakumbuehe Chadomo na Sukuma gang kwamba kura zoote za Vijijini ni za Samia na ndio maana hutokaa usikie kelele za shida ya Barabara kama ilivyokuwepo hapo miaka ya nyuma..

Hii ni sekta Moja tuu ya Barabara ila Hali Iko hivyo sekta zoote za Uchumi.

My Take
Hakuna Rais aliyewahi ku deliver mambo makubwa Kwa mda mfupi kama Rais Samia.Buyu Rais aendelee kugombea Hadi achoke mwenyewe maana ataleta Mageuzi makubwa sana.

Hizo ni namba tu huwa zinaandikwa, na ukae ukijua hizo pesa HAZIPO.

Inategemea zaidi Makusanyo yatakavyokuwa.

Ndio maana nchi hii budget ni upuuzi tu, wa karatasi tuna Wala haijawahi kutekelezwa kwa asilimia angalau 50.
 
Tunazungumzia awamu ya 6,acha kuropoka Samia hana wa kumlinganisha Kiongozi Tanzania hii..

Lini Tanzania iliacha kupata mikopo na misaada mbona hatukuwahi kuona Bajeti za kutengeneza Barabara Vijijini?
taratibu, wewe ndio ulioingiza hoja awamu 5 sasa turudi kwa Dp-wodi, hii mada yako nitaendelea tukisawazisha huko
 
taratibu, wewe ndio ulioingoza awamu zingine. sasa turudi kwa Dp wodi, hii mada yako nitaendelea tukisawazisha huko
Au ulikuwa unanyonya Kwa hiyo hujui kitu? mambo haya sio Siri taarifa zote ziko kwenye tovuti za serikali na taasisi husika
 
Hizo ni namba tu huwa zinaandikwa, na ukae ukijua hizo pesa HAZIPO.

Inategemea zaidi Makusanyo yatakavyokuwa.

Ndio maana nchi hii budget ni upuuzi tu, wa karatasi tuna Wala haijawahi kutekelezwa kwa asilimia angalau 50.
Sasa hazipo kwani nini maana ya serikali kupitisha Bajeti?
20230705_184207.jpg
 
Back
Top Bottom