Tarehe 27- 29 August mwaka jana tulikuwa na conference ya siku tatu ya Social Accountability Practitioners katika hotel ya Whit
e Sand. Moja ya watoa mada alikuwa Zitto, kwa upande wa Ccm alikuwepo Jerry Slaa na Yahya Nayanda mkuu wa wilaya ya Iramba wengine walikuwa Jaji Manento, Abuu Riyoba na wageni wengine wa kimataifa. Warsha hiyo ilifunguliwa na Naibu waziri ofisi ya Waziri mkuu TAMISEMI Agrey Mwanri.
Wakati wa kujibu maswali Zitto aliulizwa ni nini msimamo wake kuhusu mchakato wa katiba kuhodhiwa na wanasiasa. Katika majibu yake pamoja na mambo mengine alisema ni vizuri wanaharakati wakachukua nafasi yao kwenye mchakato huo maana vyama vya siasa vinaangalia zaidi agenda zao na hasa zitakozovinufaisha kisiasa "msituamini wanasiasa kufanya kila kitu maana vyama vyetu vina agenda zake.... hatutaweza kusimamia kila kitu"
Kilichonishangaza hata kabla ya kutoka ukumbini ilishapostiwa Jf kwamba Zitto alisema wanasiasa wasiaminiwe hata kama ni wa upinzani!! Nilishindwa kuelewa maana aliyoongea Zitto kama ungependa kupost yalikuwepo mengi ya maana, kama utakumbuka kipindi hicho ndo kulikuwa na sakata la fedha zilizopotea wizara ya ujenzi. Alilieleza vizuri jinsi alivyomshitaki Maghufuri kamati ya haki na kinga za bunge. Nimefanya kazi za uandishi wa habari kwa miaka mitano huko nyuma na nilidhani hiyo ndo ingekuwa habari!
Nilichojifunza siku hiyo ni kwamba pamoja na matatizo ya Zitto ndani ya chama, bado Ccm wanamchonganisha na chama chake. Swali nililobaki najiuliza ni je Zitto mwenyewe haoni hali hiyo? Kwa nini hachukui hatua za kujibu tuhuma kama hizo moja kwa moja? Nilijua kwamba kwa sababu yeye haonyeshi kushiriki vizuri issue ya katiba basi tuhuma kama hiyo ninayomini ilitengenezwa na wanaccm itamchafua mbele ya viongozi wake, lakini kwa nini asikanushe?
Zitto ni mwanachama wa Jf naamini atasoma uzi huu na labda aseme kwa nini alikaa kimya kuhusu hili.