Kwa Majasusi tu

Nashukuru MDAU kwa hoja zako, ambazo nitajitahidi kuzijibu kama ifuatavyo.

1. Mimi sitambui kuwa kuna makundi ndani ya TISS, na endapo yapo basi Naibu Mkurugenzi Mkuu angebainisha hayo. Mie ninachodhani ni kwamba hizo taarifa alizotoa Mheshimiwa Slaa zilikuwa cooked na watu ambao huwa wanampatia taarifa mbali mbali ikiwemo nyaraka za Serikali.

2. Kuhusu Ufisadi, mimi sidhani kuwa ni suala la kujadiliwa zaidi kwa kipindi hichi kwa vile ni masuala yaliyopo mahakamani. Sio vyema kujadili sana masuala yaliyopo Mahakamani, na ni TISS ndio waliofanya kazi ya kuwasilisha mashitaka hayo Mahakamani kufuata taratibu husika.

3. Dk Slaa alizitoa tuhuma NZITO dhidi ya TISS hadharani na imepaswa ajibiwe hadharani. Hii ni kwa faida ya Watanzania kwa nia ya kuwahaakikishia Wananchi kuwa TISS haifanyi shughuli zozote zinazoweza kupelekea uvunjaji wa amani ikiwemo KUCHAKACHUA KURA.

4. TISS sio chombo cha SIRI ndio maana kuna Sheria ya Bunge ambayo muanzilishi wa Thread hiii aliinukuu. Utendaji wa TISS huwa haujitokezi hadharani kwa kuwa kwa TISS ni kazi tu, kwengine ndio Majungu. Hata hivyo, TISS wametoa maelezo hadharani kwa nia ya kutekeleza DHAMIRA ya TISS ie Utunzaji wa AMANI na USALAMA nchini.
 
Ni kweli hawa jamaa wamekosa uzalendo wa kweli....namfahamu afisa usalama wa wilaya moja huko kaskazini alikuwa anajitapa baada ya kupata maji ya ngano kuwa iwe isiwe lazima jimbo la karatu libebwe na sisiem...kwani wamejipanga ilivyo kuwasaidia.

Je wameajiliwa na na sisiem au taifa. Undugunazation kwenye taasisi hiii ndo usiseme... jamaa yangu alimpachika mimba mtoto wa member wa TISS by then hakuwa na ajira...basi yule baba akafaiti jamaa yangu akaienda mafunzoni na sasa ni mwanaTISS...uweledi huko si sana bali umimi na kufanya kama ulivo agizwa
 
Nashukuru MDAU kwa hoja zako, ambazo nitajitahidi kuzijibu kama ifuatavyo.

1. Mimi sitambui kuwa kuna makundi ndani ya TISS, na endapo yapo basi Naibu Mkurugenzi Mkuu angebainisha hayo. Mie ninachodhani ni kwamba hizo taarifa alizotoa Mheshimiwa Slaa zilikuwa cooked na watu ambao huwa wanampatia taarifa mbali mbali ikiwemo nyaraka za Serikali.

2. Kuhusu Ufisadi, mimi sidhani kuwa ni suala la kujadiliwa zaidi kwa kipindi hichi kwa vile ni masuala yaliyopo mahakamani. Sio vyema kujadili sana masuala yaliyopo Mahakamani, na ni TISS ndio waliofanya kazi ya kuwasilisha mashitaka hayo Mahakamani kufuata taratibu husika.

3. Dk Slaa alizitoa tuhuma NZITO dhidi ya TISS hadharani na imepaswa ajibiwe hadharani. Hii ni kwa faida ya Watanzania kwa nia ya kuwahaakikishia Wananchi kuwa TISS haifanyi shughuli zozote zinazoweza kupelekea uvunjaji wa amani ikiwemo KUCHAKACHUA KURA.

4. TISS sio chombo cha SIRI ndio maana kuna Sheria ya Bunge ambayo muanzilishi wa Thread hiii aliinukuu. Utendaji wa TISS huwa haujitokezi hadharani kwa kuwa kwa TISS ni kazi tu, kwengine ndio Majungu. Hata hivyo, TISS wametoa maelezo hadharani kwa nia ya kutekeleza DHAMIRA ya TISS ie Utunzaji wa AMANI na USALAMA nchini.

nashukuru mdau, nimekusoma naomba nikujibu hivi kufuatana na point zako
1) Taasisis kama hiyo inatakiwa kuwa na kauli na mwongozo mmoja, lakini inapofikia kitu sensitve hata siri za serikali zinafuja, basi ujue kuna makundi, ndio kuna makundi, lipo kundi tiifu kwa CCM na ndio wako bize kuipigania na kuna kundi ambalo liko against na CCM na siasa zake, na ndio hao wanaotoa taarifa zote za siri zinazofanywa na cCM wakishirikiana na Usalama wa Taifa

2)Swala sio kesi kuwa mahakamani, bali walipashwa kuzuia huo wizi wa EPA on spot kwa sababu ulikuwa ni hatarishi kwa usalama wa TAifa la Tanzania, hizo ni fedha za walipa kodi wote wa Tanzania (wa CCM, Chadema, CUF na wengine wasiokuwa na vyama), sasa ilikuwaje (UWT) wakanyamaza hizo fedha za umma ziende CCM, yaani unataka kuniambaia watu wa usalama kazi yao ni kupeleka kesi mahakamani?

3) Kama alitoa hizo tuhuma adharani basi ilipaswa Jeshi la Polisi lingezungumzia hicho kitu na wala sio Mtu wa usalama, hiyo sio taasisis ya kupayuka kwenye vyombo vya habari, na mwisho wa siku tutashindwa kuitofautisha hiyo na Polisi

4) Ni kweli UWT sio chombo cha Siri, lakini pia ni ukweli ulio wazi kuwa UWT sio chombo kinacho fanya kazi zake hadharani, chombo hicho kinafanya kazi zake kwa usiri mkubwa, kinafatilia info kwa usiri mkubwa na sio kupayuka kwenye vyombo vya habari, na ndio maana ni shida mno kuwatambua wafanyakazi wa hiyo idara, nadhani asilimia kubwaya watanzania nikiwemo mimi tulikuwa hatumjuhi Nzoka na hata kama nilikuwa namwona nilikuwa sijuhi anafanya nini, lakini Juzi ndio nilimjua rasmi, kutojulikana kwa bwana Nzoka ni kutokana na nature ya Kazi yake, NI KWELI UWT SIO CHOMBO CHA SIRI LAKINI KINAOPERATE/FANYA KAZI ZAKE KWA SIRI
 
Kuna thread iliwahi kuongelea kuhusu hao watu wa TISS na kufanyiwa mabadiliko ili isiendeshwe kizamani. Kwa sasa kama utakuwa pamoja nami wengi wa waajiriwa wa pale ni watu wa karibu wa wanasiasa, marais wa sasa na wazamani, mawaziri, vigogo wa ndani ya system na marafiki wa vigogo hao. Kimsingi hata hao vigogo ndani ya hiyo system ni zao la viongozi na hapo kuna suala la kulindana kati ya mtu na mtu na sio maslahi ya nchi na mipaka yake. Hata hivyo katika kundi hilo hilo, wapo wale ambao wameingia hapo kwa mkono wa MUNGU hawana uhusiano wowote na kubebwa ili wapate ajira na hapo lazima kuwe na struggle kwani wanaona mambo hayaendi kama yalivyo. Na sasa wao wanachotaka ni kujua Slaa anapata wapi taarifa ili wamdake panya wao anayevujisha siri. Kwa namna fulani hiyo kauli ya bwn. Nzoka ni trick ya kujua nini kipo ndani ya vidole vya Slaa kwa sababu anajua kwa vyovyote vile watu wake wanavujisha siri na kukiwa na mgawanyiko katika chombo nyeti kama hicho ni hatari. Kumbe wao toka mwanzo walisahau kitu inayoitwa "Meritocracy". Ilikuwa kazi sana zamani kumjua TISS lakini sikuhizi wapo tu na ni waropokaji wazuri wa siri za huko Ikulu vijiweni. Hakuna siri tena ni wao ambao wanaeleza kwamba JK anaishi na waganga wa kienyeji Ikulu. Mwambie na hiyo Nzoka kama atabisha.
Mhhhh! bado nafikiria hapo kwenye red. Kwa mtindo huu, hakuna iri tena!!
 
jamani dr slaa akurupuki nakama ni mkurupukaji awezi kukurupuka na kukishambulia chombo kikubwa kama TISS ni lazima anayoongea ni ya kweli na ndio mana TISS wamekosa la kufanya wakaona wajikoshe kwa watu kwanza kufuta hyo dhana ila awana lolote lile kama ingekuwa ni uongo lazima wangeshamshugulikia tena fasta na kutangaza lakini wanaona kwa ushaidi wa dr slaa auchakachuliwi
 
Makame naomba uendelee kujibu hoja, mpaka sasa majibu hayaridhishi......ile sheria iliyotajwa pale inasema ni Director General tu ndio anatakiwa kufahamika......hata mimi Nzoka nilikuwa simjui mpaka alipoamua kutoa speech. Hivi kweli ni ruksa TISS kutoa speech?......hizi speech sio zitolewe na Polisi na Wizara na Rais mwenyewe tu?

Halafu kulikuwa na thread nyingine ya "kazi ya usalama wa taifa ni nini".....naona imefutwa sasa kwa sababu ilikuwa inaanza kuwa "nyeti" sana......sasa wewe unasema kuwa TISS sio siri, sasa mbona majadiliano yanafutwa?

Mwisho ni sipendagi majungu na umbea, napenda ukweli.....nimesikia lile jengo pale St. Peters, nyuma ya DSTV ni mjengo wa TISS.....hivi ni kweli au ni vijistory vya mtaani tu?
 
Back
Top Bottom