Kwa kuwa Wizara ya Fedha si Swala la Muungano, Hizi RUZUKU hulipwa vipi??

Hivi una maana kuwa CCM na CUF wanapata rudhuku mara mbili ama?? Yaani wanapata za ZNZ then za serikali ya muungano?? Kutokana na katiba yetu hii inawezekana kabisa iwapo ZNZ kama nchi wakaamua kuvilipa vyama kutokana na wawakilishi wake kwenye balaza la wawakilishi na selrikali ya muungano ikawalipa pia kutokana na wabunge wao kwenye jamuhuri.

Hayo ndiyo yatakuwa ni mapungufu ya katiba. Unless ZNZ kama hawatoi rudhuku.

Tulia kidogo na ukapitie post za wenzetu walizozitundika humu juu ya hoja hii kabla haujaanza kuonekena kuuliza mambo ambayo wenzetu wameshazitolea majibu humu. Naamini, kwa misingi ya uungwana hautokaa kimya bila kutujuza kama jibu lako limo tayari humu au laa.

tuendelee na mjadala.
 
Asante kwa maelezo mkuu. Ila nafikiri hujanijibu swali langu la msingi. Selikari ya ZNZ haitoi rudhuku kwa vyama kupitia idadi ya wawakilishi??

Nadhani ruzuku hawatoi ila wanalipwa lakini mishahara ya uwakilishi kama sijakosea.
 
mkuu,

Hapo kwenye red, huyo profesa kama umemkariri kama alivyosema basi alikudanganya, urudi kwake akuekee sawa hilo suala.

Mkuu kuteleza tu hakumaanishi sijamuelewa vizuri ni Muungano wa zanzibar na Tanganyika (ingawa inaitwa Tanzania Bara)
 
UFAFANUZI ZAIDI HOJA YA SERIKALI YA UBIA & ULIPAJI RUZUKU

Ndugu usipate taabu sana katika hili la wabunge, ubunge wao na ulipaji RUZUKU kwa vyama. Mwana-JF mmoja, Ndg Ng'wanangwa alishatutahadharisha juu ya KUPIGANA NA FIKRA ila kupingana nalo ni ruksa kabisa.

Bora ugombane na mtu lakini usigombane na HOJA maana kama lipo, lipo tu na litajisimamia na kujieleza lenyewe tu bila kupendezeshwa na watu. Nitatoa mfano rahisi tu kutufanya kuliona hili jambo uzuri sana hapa chini.

1. a) Hebu chukulia kwamba SMZ inayo jumla ya Wa-Tanzania wanaitwa wabunge 100.

b) Na kwamba kati ya hao wabunge 100, kati yao 80 ni wa Bunge la wawakilishi Z'br.

c) Na kwamba wabunge wengine 20 ndio wa kwenda Bunge la SJMT Dodoma.

d) Itambulike wazi kwamba wakati KATIBA ya SJMT inaelekeza kwamba vyama vyote vya siasa nchini ni lazima viwe ni vyenye sura ya KIMUUNGANO (yaani ujumla maeneo yote ya iliokua Tanganyika, Pemba na Unguja) hivyo kupata haki ya KU-SHARE sehemu ya ile idadi ya wabunge 100 (ikiwa na maana kwamba kwa siasa za ushindani, kila chama kitawania idadi fula kati ya wa 80 kwenye bunge la Wawakilishi Zanzibar na hivyo hivyo kati ya wa 20 kwenye bunge la SJMT kule Dodoma).

LAKINI katiba hiyo hiyo inatoa baraka ya uwepo na uhalali wa SMZ kule na SJMT huku bila kuingiliana kiutendaji ila tuu katika yale MAENEO YA KI-MUUNGANO tu.

Basi dira inayotolewa na KATIBA SJMT inabaini kwamba kwa kujitegemea kule kule, SMZ itawafurahia haki yake ya kujitegemea katika maeneo husika na vile vile KUWAJIBIKA KUGHARAMIA haki hizo, na SJMT nayo hivo hivo.

Hii inaleta maana kwamba kati ya wabunge 100 SMZ italazimika kwa mujibu wa KATIBA ya SJMT kulipa RUZUKUZOTE zitokanazo na wale wabunge 80 ambao lengo la kuchaguliwa kwao na pia eneo lao la kazi ni katika ofisi inayoitwa Bunge la Wawakilishi kule visiwani. Wajibu huu unatakiwa kutekelezwa SMZ vyama vya siasa ambavyo vimefanikiwa kupata wabunge kule.

Sasa tuiweke hivi, kati ya wabunge 80 wale wanaotumikia kule Visiwani tu na wala si katika Bunge na maswala ya Muungano Dodoma, tuseme:


CCM kimefanikiwa kujinyakulia wabunge 33,
CUF wabunge ................................ 32,
CHADEMA wabunge .........................10,
TLP wabunge ................................. 03
TPP Maendeleo, Mbunge ................... 01
NCCR-Mageuzi, Mbunge .................... 01
Jumla ya Wabunge SMZ ............ 80


Gharama ya Wabunge hawa 80 zilipwe, siku zote na SMZ kama ambavyo KATIBA ya SJMT inavyotambua uwepo wa serikali hii na kwa kuzingatia ukweli kwamba serikali hii inafurahia huduma za hawa waheshimiwa wabunge kule Visiwani kwa mambo ambayo si ya Ki-Muungano, ukiachilia mbali tofauti za kiitikadi za kisiasa na vyama vyao wabunge hawa.

Kwa upande wa pili, miongoni mwa wale Wabunge 20 kutoka kule Tanzania visiwani kuja kwa ajili ya kazi waliochaguliwa kwa mujibu wa KATIBA ya SJMT kule Bungeni Dodoma na kwamba KWA UHAKIKA SJMT inaendelea kufurahia haki ya kupata huduma toka kwa waheshimiwa wabunge hawa pale Dodoma na basi SJMT nayo inawajibika moja kwa moja kugharamia ulipaji RUZUKU kwa vyama vya siasa vile vile na kwa misingi ile ile ya idadi ya wabunge ambao kila chama kitakua kimejinyakulia kati ya wale 20.

Labda nayo tukaiweke hivi:


IDADI YA WABUNGE NA WANAKOWAJIBIKA

WABUNGE: VISIWANI BARA JUMLA

CCM kimefanikiwa kujinyakulia wabunge .... 08, ............ 220 ...................... 228
CUF wabunge ................................ ......06, .............. 21 ...................... 27
CHADEMA wabunge ............................... 02, ............. 50 ....................... 52
TLP wabunge ....................................... 01 .............. 08 ....................... 09
TPP Maendeleo, Mbunge ......................... 01 .............. 02 ........................ 03
NCCR-Mageuzi, Mbunge .......................... 02 .............. 10 ....................... 12
Jumla ya Wabunge SJMT ........... 20 ............ 311 ...................... 331

Sasa ndugu zangu Wa-Tanzania walipa kodi, Wana-JF tunaojadiliana, na Wageni wetu mnaotutembelea hapa jamvini, HOJA HAPA NI KWAMBA kwa kuwa SERIKALI YA MUUNGANO NI SERIKALI YA KI-UBIA, KATI YA Serikali mbili ambayo mbia mwingine (Tanganyika) ama alikufa au kapumzika bado usingizini, na basi walipakodi Tanzania wakafurahie ubia huu na haki zake zote na vile vile tukubali kuwajibika kugharamia furaha zetu hizo tunazozinuna kutoka kwenye ubia wenyewe hadi pale ambapo MKATABA WETU WA UBIA unavyotuelekeza.

Hii ina maana ya kwamba kwa msingi wa mfano wa kinadharia hapo juu, walipakodi upande wa Tanganyika wanaelekezwa na KATIBA ya SJMT wakagharamie kwa peke yao kulipa vyama vya siasa RUZUKU kutoka Wizara ya Fedha ya Tanganyika hadi idadi ya wabunge 311.

Na kwa upande mwingine Wabia wengine wa SJMT yaani walipa kodi Zanzibar nao wakagharamie kwa peke yao kulipa vyama vya siasa nchini RUZUKU kutoka Wizara ya Fedha ya Zanzibar hadi kwenye idadi ya wabunge 80.

Na kwamba kwa msingi huo, SJMT ambayo sasa ndio sura halisi ya SERIKALI YA KI-UBIA uliko nayo pia ifurahie haki ya utumishi na huduma za wabunge wa MUUNGANO kwa kuomba walipakodi wa pande mbili za SERIKALI YA KI-UBIA na kulipa vyama vya siasa kama RUZUKU mpaka idadi ya wabunge wa Muungano unakokomea.

Hii inatuelekeza kwamba wale wabungu 20 toka Zanzibar kwenda Bunge la Muungano ni kwa gharama ya kushirikiana ambayo SJMT lazima ilipe. Hii ina maana kwamba Walipa kodi wa mbia anayeitwa Tanganyika nao ni SHARTI WAKATUWEKEE MEZANI NA TUJUE WABUNGE WAO WA MUUNGANO ni akina nani, na wako wangapi ili nao gharama zao zikaingizwa kila mara kwenye hundi inayoandikwa na na SJMT.

Na kama wabunge wa muungano kwa upande wa Tanganyika hawapo basi ni juu ya huyu mbia MZEMBE na wala hilo halimuondolei wajibu wa kuendelea kuwalipa wabunge waliopo kwa jina la SJMT wale 20 toka Zanzibar.

Sasa, hapo awali niliomba maafisa wetu mbali mbali kuitikia hoja ya mlipa kodi mimi kwa kukagua taratibu za ulipaji ruzuku kwa vyama vya siasa nchini kwa msingi wa wabunge na ubunge wao kama ambavyo KATIBA zetu zinavyotuelekeza na waone kama kuna mlipaji RUZUKU fulani au vyama vinavyolipwa ruzuku hizo kama kweli mambo yote yanakwenda kwa USTAHILI WA UBIA WETU??? Lakini hata Mwana-JF alio na taarifa katika hili akatuwekee hapa jamvini.

Sasa, wewe mwana-JF mwenzangu uliekua na waswali kifuani ambayo kidogo yalionekana kutopatiwa majibu basi endelea kuwauliza wanajamvini na kama TUNAO UWEZO wa kulijibu basi tutajitahidi. Karibu sana.

Mkuu hebu jaribu kuchunguza zaidi kabla ya kutoa estimates zisizo na maana kaka. Pia wale wawakilishi sio wabunge na hilo ni swala tofauti. Kwakuwa makubaliano ya muungano yalikuwa ni kuiacha zanzibar kuwa nchi inamaana wana baraza lao la kutunga sheria. Ingelikuwa zanzibar imekubalia kuachia sovereign state yake basi ungelikuwa na hoja venginevyo hoja yako haina msingi.
 
Hivi una maana kuwa CCM na CUF wanapata rudhuku mara mbili ama?? Yaani wanapata za ZNZ then za serikali ya muungano?? Kutokana na katiba yetu hii inawezekana kabisa iwapo ZNZ kama nchi wakaamua kuvilipa vyama kutokana na wawakilishi wake kwenye balaza la wawakilishi na selrikali ya muungano ikawalipa pia kutokana na wabunge wao kwenye jamuhuri.

Hayo ndiyo yatakuwa ni mapungufu ya katiba. Unless ZNZ kama hawatoi rudhuku.

Za wakati ndugu,

He kapitie posti namba 19 kwa ufafanuzi zaidi unaoendana na swali lako. Asante kwa udadisi wako juu ya hoja hii hapa.
 
Back
Top Bottom